Kenya 2022 Maafisa 8 wa Tume Huru ya Uchaguzi Kenya Wakamatwa

Kenya 2022 Maafisa 8 wa Tume Huru ya Uchaguzi Kenya Wakamatwa

Kenya 2022 General Election

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827

MAAFISA nane wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya (IEBC) wamekamatwa na Polisi na kusimamishwa kazi baada ya kukutwa wakifanya mkutano wa siri.

Maafisa hao wamekamatwa katika kaunti za Homabay, Kisumu na Bungoma ambapo walikutwa wakiwa na baadhi ya wagombea wa nafasi tofauti katika Uchaguzi Mkuu unaofanyika leo Agosti 9, 2022.

Maafisa wengine wanne wa tume hiyo ya uchaguzi wamesimamishwa kazi katika maeneo ya Bunge ambayo ni Ndiwa na Webuye Mashariki mwa nchi hiyo.

Maafisa hao wamesimamishwa baada ya kukutwa wakiwa wamekutana kwa siri na wagombea wa kiti cha wawakilishi wa Bunge la kaunti moja nchini humo na wagombea wa Ubunge.

Kwa mujibu wa ushahidi wa video uliotolewa na Polisi unaonyesha kwamba katika mojawapo ya tukio alionekana Naibu Msimamizi wa kituo cha kupigia kura akimshawishi mkubwa wake kukubali kwa lengo la kumsaidia mmoja wa wagombea kupata ushindi.

Baadhi ya maafisa wengine wa tume ya uchaguzi katika kaunti ya Bungoma wametoroka baada ya wenzao kukamatwa nyumbani kwa mmoja wa wagombea.

Hayo yamejiri baada ya wananchi kutoa taarifa kwenye kituo cha Polisi huku ikibainika kwamba mshukiwa aliyekamatwa amewekwa chini ya ulinzi katika kituo cha Polisi cha Webuye

Chanzo: TanzaniaWeb
 
Kwa maana yako huyu Mheshimiwa wetu mstaafu naye ni miongoni mwa hao 8! ?
Possible, amefanya haya nchini mwake, kuna uwezekano kujaribu kuyafanya kwa jirani zetu,welldone kenyans democracy in the making,nipo hapa na glass ya ulanzi na matokeo nayaona live!hayapelekwi kigamboni kwanza, then Zanzibar then....,was craze
 
Kumbe kuna vilaza wakubwa kama wewe humu . Kikwete ni mwangalizi , Kazi yake ni kutoa tathimi majukumku ya tume ya Kenya wewe unmpa kikwete , BAVICHA mmejaza nzi kichwani

USSR
Who told you kuwa kikwete kule ni candidate wa uchaguzi? Mr. Kikwete yupo compromised hawezi kusimamia uchaguzi wa haki wakati yeye ni mwizi wa kura, he rape our democracy, anapenda kusafiri na kula usd tu, matokeo ya uchaguzi mimi huku lingusenguse ninayaona live Mr. Kikwete hana la kufanya kule, huwezi kuhubiri upendo kwa familia ya jirani wakati yako ni ukatili mkubwa.
 
Kumbe kuna vilaza wakubwa kama wewe humu . Kikwete ni mwangalizi , Kazi yake ni kutoa tathimi majukumku ya tume ya Kenya wewe unmpa kikwete , BAVICHA mmejaza nzi kichwani

USSR
Kikwete ni compromised, hawezi simamia haki wakati ni mwizi wa haki, kwanza wa nini wakati matokeo ninayaona live?
 
Back
Top Bottom