Maafisa Biashara Nchini watakiwa kuonesha matokeo chanya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Ujumbe huo umetolewa alisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mkoani Mara, Juma Chikoka wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Maafisa Biashara kutoka mikoa 10.

Maafisa walioshiriki katika mafunzo hayo ni kutoka mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Kigoma, Arusha, Manyara, Kilimanjaro na wenyeji Mara.

DC Chikoka amesisitiza maafisa biashara kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu, Sheria na maadili ya kazi yao pamoja na kuwasisitiza kuwa ni vizuri wakaoneshe matokeo Chanya ya kile wanachokifanya.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na yanafanyika katika Ukumbi wa Uwezeshaji, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.
 
Wakala wasumbufu wa biashara za watu.

Ukiwapa wao hata genge la nyanya kusimamia week moja tu chaliii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…