Maafisa Kazi wa Wilaya na Mikoa wanawasaidiaje wafanyakazi wa Kampuni binafsi?

Maafisa Kazi wa Wilaya na Mikoa wanawasaidiaje wafanyakazi wa Kampuni binafsi?

A

Anonymous

Guest
Habari zenu, Ujumbe au Maoni haya naomba yafike katika wizara husika ambayo ni WIZARA YA KAZI, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU, TANZANI.

Katika kila ofisi ya Wilaya na Mikoa yetu ya Tanzania, Wizara yetu imejaribu kueka maofisa wa Idara ya Kazi kwa lengo la kuratibu na kufuatilia utendaji pamoja na kuhakikisha ya kwamba haki na wajibu wa Wafanyakazi katika Mashirika na Makamouni ambayo yako katika wilaya na Mikoa Husika Unazingatiwa na kutekelezwa kwa mujibu wa sheria za Nchi yetu kwa kuzingatia Sheria na Kanuni zilizo wekwa na Wizara.

Kinachonisikitisha ni kwamba utakuta Baadhi ya makampuni yanakiuka na kupitindisha kwa makusudi Haki na wajibu kwa waajiriwa wao.

Mfano:
Kuna baadhi ya makampuni yanadiriki kufanya ubaguzi wakati wa kufanya alipo ya Mishahara ya Wafanyakazi, Kuna Kundi huwa linalipwa kila Mwezi lakini kuna Kundi wao huwa hawalipwi kabisa na inafikia mpaka miezi zaidi ya mitano bila ya kilipwa Mishahara.

Maoni yangu ni kwamba Regional and District Officers wajaribu kufanya utaratibu wa kuwawajibisha wakurugenzi wa Makampuni Binafsi yote ya kila Wilaya na Mikoa kuwa wanawajibika kuwa wanapeleka PAYROLL LISTS ambazo zimeshafanyika malipo kwa wafanyakazi wa kampuni husika, pamoja na ufuatiliaji wa karibu ili kujiridhisha ya kwamba ni kweli wafanyakazi hao wameshalipwa mishahara yao au la.

Nazungumza kwa uchungu na kusema watanzania wenzetu hasa wanaofanya kazi katika Makampuni ya wawekezaji wa ndani na wa nje ambao wana asili za kigeni wana nyanyasika sana.

Napenda kuwasilisha hoja.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom