Maafisa TPA watuhumiwa kupokea rushwa ya $800,000 kutoa tenda ya $6.6m

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mamlaka za Marekani zimeipiga faini ya dola milioni 222 kampuni ya programu kwa kutoa rushwa katika nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Tanzania, nchi nyingine ni Kenya, Afrika Kusini, Ghana, Malawi. Pia zipo Azerbaijan na Indonesia.

Maafisa wa mamlaka ya bandari Tanzania(TPA) wanatuhumiwa kupokea bilioni 2.1($ 800,000) kama rushwa ili kuipa tenda yenye thamani ya $ 6,635,000 kampuni inayojihusisha na programu(software) Tenda ilihusisha kutoa leseni na huduma, tenda hiyo ilipewa kampuni ya Twenty Third Century Systems ambayo imesajiliwa Zimbabwe.

Maafisa hao wanadaiwa kupokea pesa hizo kwenye sanduku. Pamoja na kampuni hiyo kulipwa $ 4,000,000 kampuni hiyo ilishindwa kutimiza chochote. Mwaka 2022 Tanzania ilibatilisha mkataba baina yao ulioingiwa mwaka 2014/15 na kuwafungulia kesi maafisa waliohusika.

Inaaminika pia kampuni hiyo iliweka gharama mara mbili ya gharama za kukodi program hiyo, TPA ililipa $ 404,029 badala ya gharama halisi ya $ 190,643.

Pia Mwezi Septemba 2019 TPA ililipa kampuni hiyo hiyo kutoka Ujerumani $400,000 kupitia kazi zake zilizofanywa na kampuni yake iliyosajiliwa Zimbabwe. Pia TPA iliipa mkataba mwingine wenye thamani ya $ 997,647 kutoa huduma ambayo haikutajwa.
 

Halafu kuna watu walikuwa wanaamini kabisa kuwa wakati wa Mwendazake watu walikuwa hawapokei Rushwa .....!!
 
Halafu kuna watu walikuwa wanaamini kabisa kuwa wakati wa Mwendazake watu walikuwa hawapokei Rushwa .....!!
Nchi ina vitengo vingi sana ,wajanja ni wengi sana hata uwe smart sana hao jamaa ni pandikizi la mfumo ,watu wachukue pesa ndefu hivyo sio kitoto .

Channel ni ndefu ukifuatilia kuna wastaafu kibao wazee weny heshima nchini wamepata mgao...
 
Hii nchi Rushwa, Ujinga na Kutokuwa na Viongozi sahihi kwenye nafasi sahihi ndo mambo yatakayoufanya iendelee kuwa maskini hadi mwisho wa dunia
 
Usione v8 ya 2022 na range za 2023 na kuota kila eneo hizo ni kodi zetu ndugu na hicho ni kidogo sana

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Sio TPA pekee, huko TANAPA rushwa zinatembea sana kuuza space za kujenga Hoteli Polini, na huko TAWA inatembezwa rushwa kuuza vitalu vya uwindaji, fikiria watu wanapojea rushwa watu wanapewa vitalu kwa miaka 99 then tuko humu kushangilia kwamba wacha wale.
 
Suala hili linanikumbusha Rada...
Hii ni aibu kubwa kwa Serikali...wakati mamlaka za Marekani zinachukua hatua kama hizi...sisi kimyaaa..
Hii kesi ya hawa wapigaji inatajwa tu na hakuna hatua yoyote inachukuliwa.... huku hao wahusika wanaponda tu raha.....
 

Hiyo kampuni ndo hao hao waliochukua rushwa, ni mkono wa kulia na kushoto, mtu ni yule yule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…