Tetesi: Maafisa Utumishi Njooni hapa: Nahitaji msaada juu ya hili

Tetesi: Maafisa Utumishi Njooni hapa: Nahitaji msaada juu ya hili

Redpanther

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2019
Posts
2,823
Reaction score
3,816
Habari gani wana Jamvi la Habari na Hoja mchanganyiko.

Acha niende kwenye Hoja moja kwa Moja. Nipo katika Harakati za kuomba Ajira za Wizara ya Afya. Kuna hiki kipengele cha Kudhibitisha Vyeti mahakamani au kwa Wakili.

Shida yangu kubwa haja nikutaka kujua, Je kuna shida yoyote nikiambatanisha nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria miaka mitatu nyuma na vikawa scanned kwa ajili ya kupakiliwa kwenye Tovuti husika wakati wa kuomba kazi?

Jambo hili linaweza pelekea kunyimwa kazi au Taratibu zinasemaje kuhusu kuthibitisha Nakala kwa Wakili ?

Ni baada ya muda gani nakala hizi nilizothibitisha Mwaka Jana zinaweza zisifae tena kuambatanisha wakati wa kuomba kazi?

Mtanisamehe kama kuna mahali nimechanganya mambo ila naamini nimeeleweka vyema.

Nawasilisha [emoji404]
 
Anaekihitaji Cheti ndio anatakiwa akiverify.. Sielewi huu upumbavu wa kuwahangaisha waombaji kazi kuverify vyeti vyao. Sababu kama ninakupa Cheti ambacho nimekiverify kwa mwanasheria Je na wewe(Mwajiri) huwa unaverify uhalali wa verification yangu Mwombaji??

Waswahili tuna mambo ya ajabuajabu sanaa
 
Dogo unapata wapi uvivu kama huna pesa nenda halmashauri omba uonane na mwanasheria wa halmashauri ukimuona muombe atakuthibitishia vyeti vyako, atafanya hivyo bure kabisa hii ni kwako na kwa wenzio wote wasumbukao.
 
Mmh Kwamba anathibitisha vyeti hivi bureee ??
 
Anaekihitaji Cheti ndio anatakiwa akiverify.. Sielewi huu upumbavu wa kuwahangaisha waombaji kazi kuverify vyeti vyao. Sababu kama ninakupa Cheti ambacho nimekiverify kwa mwanasheria Je na wewe(Mwajiri) huwa unaverify uhalali wa verification yangu Mwombaji??
Waswahili tuna mambo ya ajabuajabu sanaa

Hii ni Hoja nzito sana, Serikali kupitia wizara husika ya Ajira na Utumishi iliiangalie hili. Hebu waza tu, Kuthibitisha vyeti ni 1000@ na ukute una nakala kama 10 hivi maana yake unatakiwa uwe na 100k… Damnn it. Huyu ni Mtu ambaye hana Ajira ndio anaitaka hiyo ajira hivi hiyo Laki moja ya ku verify vyeti anaitoa wapi kama sio kutengeneza mazingira ya kum select out.

Ahsante sana kiongozi kwa mchango wako
 
Anaekihitaji Cheti ndio anatakiwa akiverify.. Sielewi huu upumbavu wa kuwahangaisha waombaji kazi kuverify vyeti vyao. Sababu kama ninakupa Cheti ambacho nimekiverify kwa mwanasheria Je na wewe(Mwajiri) huwa unaverify uhalali wa verification yangu Mwombaji??
Waswahili tuna mambo ya ajabuajabu sanaa
Nami nilidhani anayekihitaji ndiye anacross check na aliye kitoa kujiridhisha kama ni cheti halali, hivi wakili averify cheti kilichotolewa na chuo anajua details za vyuo vyote?
 
Ni Bora utuulize sisi wa kada nyingine.
Maafisa utumishi Wana roho mbaya utadhani wote baba zao wangoni na mama zao wapare.

Maafisa Utumishi si ndio wahusika wa mambo ya Kuajili watumishi kwenye Taasisi yoyote
 
Nami nilidhani anayekihitaji ndiye anacross check na aliye kitoa kujiridhisha kama ni cheti halali, hivi wakili averify cheti kilichotolewa na chuo anajua details za vyuo vyote?

Nahisi wanachothibitisha kuwa umiliki halali wa Nakala hiyo ya Cheti na sio kuthibitisha Viwango au Ubora wa Elimu ya muombaji wa Kazi.
 
Haina tatizo muhimu uwe na uhakika ni "certified true copy of the original "
 
Back
Top Bottom