Maafisa wa Arsenal, waanza ziara yao Tanzania

Maafisa wa Arsenal, waanza ziara yao Tanzania

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
stones..-722x400.jpg


KLABU ya Arsenal leo imeanza mazungumzo rasmi na makampuni 20 ya hapa nchini kwa lengo la kufungua mahusiano ya kibiashara lakini katika mpango huo makocha wa timu hiyo na baadhi ya nyota waliowahi kutamba watapata fursa ya kudhuru hapa nchini.

Mapema mwenyeji wa wageni hao, Afisa mtendaji mkuu wa EAG Group, Bw Imani Kajura, alisema hii ni fursa sahihi kwa makampuni ya Tanzania kuchangamkia ili kutambulika kimataifa, na kutoa fursa kwa Nchi, kunufaika na miradi ya kijamii itakayoendeshwa kwa ubia, endapo Arsenal itafanikiwa kupata wabia katika sekta ya biashara.

Akizungumza jijini leo, Mkurugenzi wa mahusiano ya kimaendeleo ya klabu hiyo Sam Stone amesema ujio wao nchini unalengo la kutaka kufungua milango ya kibiashara na baadhi ya makampuni makubwa na madogo nchini.

Mkurugenzi wa maendeleo na mahusiano wa klabu ya Arsenal ya England, inayoshiriki ligi kuu ya EPL, Sam Stone akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa uwekezaji wa klabu hiyo nchini, pamoja naye ni meneja wa kitengo hicho Daniel Willey.

Stone ambaye ameambatana na meneja wa kitengo hicho Daniel Willey amesema katika mpango huo pia Arsenal itawaleta nchini makocha wao wa soka la vijana kuja nchini kusaidia kukuza wachezaji vijana huku pia wachezaji wa zamani wa timu hiyo wakiwemo Thiery Henry,Robert Pires na Martin Keown wanaweza kuja nchini kutembelea miradi hiyo.

"Tutaanza kwanza kuzungumza na makampuni hayo ambayo yameonyesha kuhitaji kuonana nasi kati ya hayo wapo pia viongozi wa soka hapa nchini Tanzania,tumeona ni vyema tukaanzisha mahusiano haya baada ya kuona muamko wa Tanzania katika maeneo hayo,"alisema Stone.

"Tukikamilisha kila kitu kuhusu mahusiano haya wakati utekelezaji ukianza kuna uwezekano mkubwa wa makocha wetu wa vijana kuja hapa lakini pia wachezaji wetu wa zamani kama Pires,Henry na Keown wanaweza kuja hapa kama tulivyofanya nchi za Afrika Kusini, Uganda, Kenya, Misri."


TanzaniaSports
 
watembelea Makao makuu ya PSPF
*wafanya mazungumzo na Mkurugenzi mkuu Bw Adam Mayingu

Mabosi wa Mabingwa wa Kombe la FA wa England, Arsenal, waliopo nchini kwa ziara ya kikazi wameanza kutikisa, ambapo kampuni nyingi zinataka ushirikiano na klabu hiyo.
Maofisa waliopo nchini ni pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo na Ushirikiano, Sam Stone na Meneja Maendeleo na Ushirikiano, Daniel Willey wanatarajiwa kukutana na uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jumanne hii.
Tayari kampuni kubwa zaidi ya 20 zimetaka ushirika na Arsenal, na majadiliano ya kibiashara yanatarajiwa kuanza mara moja, kuona ni katika maeneo gani na kwa mfumo upi watashirikiana.
Katika ziara hiyo inayoratibiwa na Imani Kajula ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, benki mbalimbali zimetaka kufanya biashara na Arsenal, lakini pia Quality Group, kampuni inayomilikiwa na Rais wa Yanga, Yusuf Manji.
Stone amewaambia waandishi wa habari Jumatatu hii jijini Dar es Salaam kwamba wamejizatiti na japokuwa wamekuja kibiashara, milango ipo wazi iwapo kuna kampuni za michezo zinazotaka kushirikiana nao na kwamba zinaweza kunufaika.
Ujumbe huo umetua nchini huku hali ya hewa kisoka kwa klabu na timu ikiwa shwari, baada ya Arsenal kuwafunga Manchester City mabao 2-0 Jumapili hii kwenye Uwanja wa Etihad unaomilikiwa na mabingwa hao watetezi wa England.
Mabao ya Santi Cazorla na Olivier Giroud yakichanganywa na ulinzi mahiri wa kitimu, vilitosha kuzikonga nyoyo za washabiki wa Arsenal ndani na nje ya England, ambapo nchini Tanzania pia washabiki wao walionekana wakitamba mitaani, licha ya kwamba ilikuwa usiku.
Stone alisema jijini Dar Jumatatu kwamba wanaichukulia Tanzania kwa umuhimu mkubwa, kutokana na ukubwa wake kijiografia, mvuto wa watu wake kwenye soka na uwapo wa kampuni kubwa na zinazoweza kushirikiana na Arsenal.
Tayari Arsenal wana uhusiano na kampuni na taasisi nchini Kenya, Uganda, Rwanda, Afrika Kusini na Nigeria.
 
Back
Top Bottom