KERO Maafisa wa Ilala wanachukua leseni dukani kwa lengo la kuhimiza ulipaji wa service levy, ni sahihi?

KERO Maafisa wa Ilala wanachukua leseni dukani kwa lengo la kuhimiza ulipaji wa service levy, ni sahihi?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Maafisa wa Manispaa ya Ilala wanapita kudai service levy, lakini kwa wale ambao hawajalipa, wanadaiwa kuchukua leseni za maduka na kuziondoa pamoja na fremu zake ukutani. Wanasema leseni hizo zitakuja kukutwa Misitu–Kivule.

Biashara ipo maeneo ya Maneno, Magole mwisho, ambapo mimi ndiye mmiliki. Ninathibitisha taarifa hii kwa sababu maafisa hao walipofika, kabla ya kuondoka na leseni pamoja na fremu zake, walinipigia simu kunijulisha. Nilipomkataza dada anayeuza dukani kutoka nje, walipitisha mkono na kuchukua leseni hizo pamoja na fremu zake.

Sikuwa na video ya tukio hilo, lakini kwa kuwa wanaendelea kupita kila siku, naamini watapita tena. Nimeprint leseni nyingine kupitia Tausi Portal na kuziweka dukani, kwa sababu madai ya levy hayahusiani na kuondoa leseni dukani.

Tunaomba sauti yetu isikike: Je, ni sahihi kwa afisa kuchukua leseni za maduka kwa lengo la kuhimiza ulipaji wa service levy? Wakija tena, tutarekodi video na kuwaripoti.
 
Back
Top Bottom