KERO Maafisa wa Wilaya ya Chemba hawajui kutoa elimu kwa Wafanyabiashara, wanajua kutoza faini tu

KERO Maafisa wa Wilaya ya Chemba hawajui kutoa elimu kwa Wafanyabiashara, wanajua kutoza faini tu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wilaya ya Chemba Mkoa wa Dodoma wanaohusika na kukusanya kodi wanatuumiza sana wananchi, wanakuja kwenye duka hata kama umefungua jana yake uko na siku moja tu, wanakupiga faini ya Sh 50,000 na wanakupa siku saba kulipa kodi.

Unakuta huna uelewa hata na hiyo kodi, kodi kwa biashara yangu ni Sh 45,000 wamesema ila mtaji wangu ni Sh 90,000 najikuta nafunga ofisi tu, wao hawana shida sana na kodi kipaumbele chao ni faini tu ambayo ni Sh 50,000.

Mfano kama umefungua biashara jana, wakija kukupiga faini ya elf 50 wanasema kosa ni kutowajuza, na ukiwaambia hauna uelewa na jambo la kodi basi ndiyo kosa zaidi. Ukipigwa faini elfu 50 wanakupa siku saba ulipe tena pesa ya leseni, ikiwa biashara ni mpya.
 
Back
Top Bottom