KERO Responded Maafisa wa Wilaya ya Ikungi (Singida) wanafunga biashara zetu na kututishia

KERO Responded Maafisa wa Wilaya ya Ikungi (Singida) wanafunga biashara zetu na kututishia

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mkazi wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, kero yangu ni kuhusu watu wanaojiita Maafisa kutoka Halmashauri ya Wilaya, wanakuja Vijijini kudai leseni na wakikuta hauna bila kujali unauza nyanya au bidhaa wanakudai faini tena kwa kujikadiria wanavyotaka wao.
Screenshot 2026-05-11 171427.jpg
Kibaya ni kwamba hawataki kutoa vitambulisho vya kazi yao na ukibishana nao wanafunga biashara na kuanza kututishia.

Nimeona ni vyema ku-share hii kero maana nikisema niende halmashauri nitageuka kuwa adui yao.

Tukiwaambia mbona Waziri Mkuu kazuia biashara kufungwa wanajibu majibu wanayojua wao.

Pia soma ~ Mwigulu: Nimekuja, Nitawashikisha adabu wote wasio na Adabu, tuache kushikilia Mali ya Mtu anayedaiwa
 
Wasiliana na boss wao Mkurugenzi asipowawajibisha wasiliana na mbunge wenu.

Wanatakiwa kulinda mitaji yenu kwa namna yoyote
 
Huko si ndo ccm mbele kwa mbele ?
Ndo maana halisi ya kuisoma namba sasa
 
Nchi hii hauna pesa hauna bunduki, jifunze uchawi tu.
 
Kuna Mahala Tumekosea Hasa Hawa Wahuni Wa Chama
 
Huko si ndo ccm mbele kwa mbele ?
Ndo maana halisi ya kuisoma namba sasa
Tena pale ikungi kuna ofisi ya ccm watu wana jaa vibaya sana, siku moja nili jaribu kumu elewesha mama 1 hivi wa makamo akawa mbogo hata salamu tu ikawa shida.
 
Mkitaka kulipia mnagewa control number?

Msipogewa control number ila mkalipia mnagewa risiti ya EFD?

Halmashauri zinategemea wananchi kulipa Kodi ambayo ni sehemu ya mapato ya halmashauri.

Haya mapato yakiwa makubwa ndiyo wazawa wasio na ujuzi wataajiriwa kama vibarua wa usafi na mishahara itatoka hapo.

Haya mapato asilimia kadhaa hua sehemu ya ile mikopo ya vijana, mikopo ya vikundi au ile ya walemavu. Siyo ajabu halmashauri yenu kutokana na mapato ikajikuta ina milioni 10 kwaajili ya mikopo lakini halmashauri X ikawa ina bilioni moja.

Kama mkilipa mnagewa risiti ya EFD (namaanisha wana POS wanatembea nayo) swala hapo ni nyinyi kuelewashana nao. Hata hivyo ukienda ofisi zao kuuliza hakuna utakayekua adui yake.
 
Tena pale ikungi kuna ofisi ya ccm watu wana jaa vibaya sana, siku moja nili jaribu kumu elewesha mama 1 hivi wa makamo akawa mbogo hata salamu tu ikawa shida.
Acha waisome namba , wapuuzi kabisa
 
Back
Top Bottom