John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 71
- 119
Maagano ya Ukoo Yalitoka Wapi
Chanzo cha maagano ya ukoo kwa kifupi
Katika biblia, Yohana 8:36 inasema, “Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”
Hebu tujiulize, ni kwa nini Bwana Yesu alipokuwa anakata roho pale msalabani, alisema neno moja tu. Alisema “imekwisha” (Yohana 19:30). Hakusema “yamekwisha”. Ukilifahamu hilo, utajua ndiyo sababu kwa nini, katika biblia, huwezi kuona maneno kama laana za ukoo, laana za kifamilia, laana za mababu, laana za mapepo, vifungo vya kikabila n.k. Ni kwa sababu, hayo yote yamejumuishwa katika hicho kitu kimoja kilichokwisha pale msalabani, nacho ni “dhambi”, yaani “dhambi ilikwisha”, yaani “kuwa huru kweli kweli”.
Dhambi ndiyo mzizi wa matatizo. Yaani, dhambi imefananishwa na ugonjwa wa ukimwi, ambao vijidudu vyake vinafanya kazi moja tu, nayo ni kwenda kushambulia kinga ya mwili, basi, havileti madhara mengine yoyote mwilini. Havisababishi kutokwa na vidonda. Havisababishi kutapika.
Havisababishi kuugua. Havisababishi kukohoa. Hapana. Lakini vinaua kinga ya mwili. Ile kinga ikishakufa, ina maana kuwa mwili hauna ulinzi tena. Hapo ndipo kila aina ya ugonjwa unapata nafasi ya kuingia mwilini. Mara malaria, mara kifua kikuu, mara mkanda wa jeshi, mara homa ya ini, n.k. Na hivyo ndivyo mwisho wa siku vinakwenda kummaliza mtu.
Dhambi nayo ndivyo inavyofanya kazi, Adamu na Hawa walipoasi pale Edeni, dhambi iliingia ndani yao (Mwanzo 3:6, 3:23). Dhambi hiyo ikaimaliza kinga yao yote ya ulinzi Mungu aliokuwa amewawekea pale Edeni. Ghafla mambo mabaya yote yakaingia. Uuaji ukaingia, dhuluma ikaingia, magonjwa yakaanza, uchawi ukaanza. Laana zikaingia. Vita vikaingia. Matabaka yakaingia. Na matambiko yakajitokeza.
Ndipo maagano yote ya ukoo yakatokea huko huko n.k. Na hili likawa ni tatizo lisilokuwa na tiba kwa vizazi na vizazi, kwa karne na karne. Ni kwa sababu kinga ya ulinzi wa Mungu, haikuwepo tena. Dawa ya dhambi haikupatikana kwa zaidi ya maelfu ya miaka, kama vile dawa ya ukimwi ilivyochukuwa muda mrefu kupatikana.
Dhambi ya asili iliondolewaje
Bwana Yesu alipokuja miaka takriban 2000 iliyopita, hakuja kushughulika na katawi kamoja cha dhambi, labda tuseme maagano ya ukoo, au laana za kifamilia, au uchawi. Hapana. Angefanya hivyo, tatizo lote lisingeondoka.
Bwana Yesu alikuja kuung’oa mzizi wote wa dhambi, kiasi kwamba mtu aking’olewa mzizi huo ndani yake, basi hakuna vimelea vyo vyote vya laana yo yote ile itakayomwandama. Alifanya hivyo kwa kufa msalabani kwa ajili yetu. Na akasema, “imekwisha”.
Dhambi zilizotendwa baada ya kifo cha Yesu Zinaondolewaje
Baada ya Bwana Yesu Kristo kufa msalabani, binadamu wameendelea kuasi na kutenda dhambi mbalimbali. Hiyo ni pamoja na kufanya maagano ya ukoo. Jambo ambalo baadhi ya watu hawafahamu, ni kuwa, kwenda kuombewa au kufanyiwa maombi fulani ya muda mrefu labda tuseme ya kufunga, na kukaa milimani na kutumia masaa mengi kuomba na kukemea, ndiyo kunaondoa laana na maagano ya ukoo au maagano ya kifamilia.
Wengine wanadhani kutoa sadaka fulani maalum ndiyo kunaondoa maagano ya kiukoo. Hapana. Mtu anaweza akafanya hivyo na bado hayo mambo yasiondoke ndani yake, kama ikiwa bado yupo nje ya wokovu.
Kama mtu hajakusudia kweli kuokoka, mambo hayo hayawezi kuondoka, yataendelea kumfuata tu. Ni lazima kuokoka. Ukisema mimi na dhambi basi, nimeamua kujitwika msalaba wangu na kumfuata Yesu popote atakapotaka mimi niende, sirudi nyuma tena. Ukatubu kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako zote.
Kisha ukatii agizo la ubatizo kwa jina la Yesu Kristo, sawasawa na Matendo 2:38, ili upate ondoleo la dhambi zako. Na kuanzia wakati huo, ukawa unaishi maisha ya mkristo aliyeokoka, siyo tu maagano ya ukoo yatafutwa juu yako, bali pia hata na yale maagano mengine usiyoyajua ya kipepo yaliyokuwa juu yako, yote hayo yatafutwa.
Hakuna haja ya kuhangaika kwenda kuombewa huku na kule. Ukifika kule kila mmoja atakuambia hiki, mwingine kile. Kumbuka kuwa wokovu ni muujiza mkubwa, ambao unatokana na neema ya Kristo tunaoupata bure bila kujisumbua, wala kugharamia chochote, Wewe ni kutii tu. Pale ulipotubu tu, fahamu kuwa vyote vimefutika. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuvunja maagano ya ukoo.
Biblia inasema ulipo moyo wa mtu ndipo ilipo hazina yake (Mathayo 6:21, Luka 12:34). Kama huna madhabahu maalum unajichelewesha bure, ni lazima ujue madhabahu yako ni ipi na ukishaijua utatenda sawasawa na madhabahu hiyo. Unaweza ukawa umeokoka lakini umeshikiliwa na magonjwa sababu ya madhabahu iliyokushikilia.
Kama maisha yako ya wokovu yapo mbali na Kristo, halafu unatafuta njia mbadala ya kuondoa tatizo hilo, kumbuka hayo mambo yalishafwa na mababu zamani, na yakashindikana. Hivyo, na wewe pia usijaribu kuyarudia hayo hayo, bali mkaribishe Yesu maishani mwako, awezaye kuondoa mzizi wote wa dhambi na laana zake zote. Na kukufanya kuwa kiumbe kipya. Na hakika atayavunja maagano yote ya ukoo, babu zako, na mababu zako waliyoingia na kuapa iwe ni katika afya, au mafanikio, au furaha, vyote vile, vitakwisha ndani yako.