Maagizo kutoka juu, yamfanya Mhadhiri UDOM kusota mahabusu

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Chama cha Wanataaluma cha Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) kimeenda Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kupinga kushikiliwa kwa muda mrefu bila dhamana kwa mhadhiri mwenzao, Melkisedeki Kitunzi Kaijage, anayetuhumiwa na Jeshi la Polisi kuhamasisha maandamano kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa ya ndani iliyotolewa na Katibu Mkuu wa UDOMASA tarehe 18 Julai, 2026, Kaijage aliripoti Kituo cha Polisi UDOM tarehe 8 Julai akitakiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO). Baadaye alihamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na kisha Kituo Kidogo cha Chang'ombe ambako anaendelea kushikiliwa hadi sasa.

UDOMASA inaeleza kuwa jitihada zao za kumsemea dhamana ziligonga mwamba baada ya maafisa wa polisi kueleza kuwa kuna "maagizo kutoka juu" ya kumrejesha mahabusu, licha ya kukiri kuwa kosa linalomkabili linadhaminika kisheria:

"UDOMASA inatambua na kusimamia haki za wafanyakazi, na tunapinga na kulaani vikali ukiukwaji wowote wa taratibu za kisheria unaomnyima mfanyakazi uhuru wake. Chini ya sheria za nchi yetu, mtuhumiwa anapaswa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 24," ilieleza taarifa hiyo.

Soma Pia: Mhadhiri UDOM akamatwa kisa Maandamano ya Sabasaba

Baada ya juhudi za dhamana kukwama, UDOMASA kupitia jopo lake la wanasheria ilifungua shauri Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma tarehe 12 Julai, 2026.

Shauri hilo lilisikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe 17 Julai na linatarajiwa kuendelea tena kesho Jumanne, Julai 21, 2026, majira ya saa 3:00 asubuhi. Uongozi wa UDOMASA umewataka wanataaluma kuwa watulivu wakati taratibu za kisheria zikiendelea.
 
Kazi shilaga wanasema wasukuma.Hivi ukiwa rais inabidi watu wote waseme au wafanye unachopenda.

Maagizo kutoka juu my foot! Huyu home boy issue yake si nasikia ilikuwa kauli za kuhusu maandamano? Ni kwamba alikosea sana kwenye kauli zake kiasi cha kutiwa heka heka namna hii?

Viongozi basi jifanyeni wafalme tujue moja.
 
Kaacha kazi ya kuelimisha jamii kageukia kuelimisha jinsi ya kukiwasha kuitengua kiuno Jamii ✍️
 
Sasa ndio wanamshtaki
uyo maagizo kutoka juu❗️
 
Kaacha kazi ya kuelimisha jamii kageukia kuelimisha jinsi ya kukiwasha kuitengua kiuno Jamii ✍️

Chawa! Imeandikwa hutaishi kwa mkate peke yake, ila kwa kila neno litokalo kichwani mwa Bwana. Angalia ndege wa angani ya kwamba hawapandi wala hawavuni wala hawakusanyi ghalani na Baba yako wa mbinguni huwalisha hao. Wewe je? si bora kupita hao?

Amelaaniwa mtu yule amtegemeae mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake na moyoni mwake amemwacha Bwana.

Chawa, Je shomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? lakini hata mmoja wao haanguki chini pasipo Baba yako kujua, lakini wewe hata nywele za kichwa chako zimehesabiwa zote. Usiogope basi, kwamba utakufa ukikosa buku 7 ya ujira wa dhambi, wewe ni bora kuliko mashomoro wengi.
 
Wakigoma na kususa kufundisha au kuwafelisha wanachuo,,, mwenye hasara ni mzazi aliyepeleka mtoto hapo kusoma.
 
Kwa Katiba yetu hii mbovu ipo siku naamini Rais atatoka Upinzani,Haijalishi itachukua muda gani lakini itatokea siku!

Marekani imewachukua miaka mingi sana kumpata Rais mwenye asili ya Afrika naamini hata Tanzania iko siku tu isiyokuwa na jina,Kwenye sheria mbovu na katiba mbovu hii iko siku!

Nadhani baada ya hapo waliokuwa madarakani watakaposhughulikiwa na sheria mbovu ambazo watu walipaza sauti zisitumike vibaya na ikiwezekana zibadilishwe wao walikuwa wakikenua meno kwa furaha!,Hapo ndipo vilio vya kubadilishwa kwa sheria mmbovu kitasikika kila kona!

Bila walioko madarakani kuonja joto la Ubovu wa Katiba na sheria mbovu hawawezi elewa!,Kwasasa wanaona kama wao ndiyo wamiliki halali wa hili Taifa,Watu wengine wote wanapaswa kufa!

Sheria iko wazi,Kwamba mtuhumiwa anapokamatwa apelekwe mahakamani ili mahakama ikaone kama anayo hatia au hana,Ila kwa kiburi kwa kuvunja sheria wanaamua kuendelea kumtesa mtuhumiwa wakiamini hakuna wa kuwafanya lolote!

Naomba Mungu hata siku nikifa hii comment ibaki kama ushahidi wa nilichokisema!

Iko siku isiyokuwa na jina sheria hizi na katiba hii itawaumiza wao,hapo ndipo watalia na kusaga meno!
 
Chama cha Wanataaluma cha Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) kimeenda Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kupinga kushikiliwa kwa muda mrefu bila dhamana kwa mhadhiri mwenzao, Melkisedeki Kitunzi Kaijage, anayetuhumiwa na Jeshi la Polisi kuhamasisha maandamano kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa ya ndani iliyotolewa na Katibu Mkuu wa UDOMASA tarehe 18 Julai, 2026, Kaijage aliripoti Kituo cha Polisi UDOM tarehe 8 Julai akitakiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO). Baadaye alihamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na kisha Kituo Kidogo cha Chang'ombe ambako anaendelea kushikiliwa hadi sasa.

UDOMASA inaeleza kuwa jitihada zao za kumsemea dhamana ziligonga mwamba baada ya maafisa wa polisi kueleza kuwa kuna "maagizo kutoka juu" ya kumrejesha mahabusu, licha ya kukiri kuwa kosa linalomkabili linadhaminika kisheria:

"UDOMASA inatambua na kusimamia haki za wafanyakazi, na tunapinga na kulaani vikali ukiukwaji wowote wa taratibu za kisheria unaomnyima mfanyakazi uhuru wake. Chini ya sheria za nchi yetu, mtuhumiwa anapaswa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 24," ilieleza taarifa hiyo.

Soma Pia: Mhadhiri UDOM akamatwa kisa Maandamano ya Sabasaba

Baada ya juhudi za dhamana kukwama, UDOMASA kupitia jopo lake la wanasheria ilifungua shauri Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma tarehe 12 Julai, 2026.

Shauri hilo lilisikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe 17 Julai na linatarajiwa kuendelea tena kesho Jumanne, Julai 21, 2026, majira ya saa 3:00 asubuhi. Uongozi wa UDOMASA umewataka wanataaluma kuwa watulivu wakati taratibu za kisheria zikiendelea.
Hii ni migogoro isiyo ya lazima, serikali ijitafakali!
 
Inatakiwa wanataaluma wa vyuo vikuu vyote kugoma nchi nzima kukataa kupokonywa uhuru wao wa kujieleza na wakuchochea fikra tunduizi si tu kwa wanafunzi wa vyuo bali kwa jamii pana iliyopo nje ya kuta nne za ma hall ya vyuoni.

Prof. Mohamed Janabi anafanya darasa huru nje ya kuta nne za madarasa ya vyuo vya juu kuhusu raia kutambua afya zao na kuzilinda

Na huyu mhadhiri Melkisedeki Kaojage naye anafanya kazi kubwa kwa jamii pana isiwe goigoi kupokea hotuba za wanasiasa bali wawe na fikra tunduizi kufanya bongo zao kuweza kutoa maoni kwa kuandika, maandamano au kuposti fikra zao huru.

Big Up mhadhiri Melkisedeki Kaijage wa the University of Dodoma College of Humanities and Social Sciences

​

Melkisedeki Kaijage
Research Assistant/Consultant - Political Party Database; Everyday Humanitarianism; Democratic Accountability (DALP II)

I consider myself an emerging academic, closely investigating African politics while struggling to grow my research network in and beyond Africa. I thus have a BA in Politics, MA in Politics and soon-to-be PhD candidate in Politics. God bless me!
 
Hii nchi ina uonevu mwingi sana. Watu wenye akili timamu wamegeuzwa kuwa maadui halafu machawa na wendawazimu ndiyo wamegeuka kuwa marafiki wa watawala.
 
Chama cha Wanataaluma cha Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) kimeenda Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kupinga kushikiliwa kwa muda mrefu bila dhamana kwa mhadhiri mwenzao, Melkisedeki Kitunzi Kaijage, anayetuhumiwa na Jeshi la Polisi kuhamasisha maandamano kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa ya ndani iliyotolewa na Katibu Mkuu wa UDOMASA tarehe 18 Julai, 2026, Kaijage aliripoti Kituo cha Polisi UDOM tarehe 8 Julai akitakiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO). Baadaye alihamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na kisha Kituo Kidogo cha Chang'ombe ambako anaendelea kushikiliwa hadi sasa.

UDOMASA inaeleza kuwa jitihada zao za kumsemea dhamana ziligonga mwamba baada ya maafisa wa polisi kueleza kuwa kuna "maagizo kutoka juu" ya kumrejesha mahabusu, licha ya kukiri kuwa kosa linalomkabili linadhaminika kisheria:

"UDOMASA inatambua na kusimamia haki za wafanyakazi, na tunapinga na kulaani vikali ukiukwaji wowote wa taratibu za kisheria unaomnyima mfanyakazi uhuru wake. Chini ya sheria za nchi yetu, mtuhumiwa anapaswa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 24," ilieleza taarifa hiyo.

Soma Pia: Mhadhiri UDOM akamatwa kisa Maandamano ya Sabasaba

Baada ya juhudi za dhamana kukwama, UDOMASA kupitia jopo lake la wanasheria ilifungua shauri Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma tarehe 12 Julai, 2026.

Shauri hilo lilisikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe 17 Julai na linatarajiwa kuendelea tena kesho Jumanne, Julai 21, 2026, majira ya saa 3:00 asubuhi. Uongozi wa UDOMASA umewataka wanataaluma kuwa watulivu wakati taratibu za kisheria zikiendelea.
Uonevu wa hali juu,halafu mnasema,mnaamani,kama kafanya kosa si apelekwe mahakamani
 
Kwa Katiba yetu hii mbovu ipo siku naamini Rais atatoka Upinzani,Haijalishi itachukua muda gani lakini itatokea siku!

Marekani imewachukua miaka mingi sana kumpata Rais mwenye asili ya Afrika naamini hata Tanzania iko siku tu isiyokuwa na jina,Kwenye sheria mbovu na katiba mbovu hii iko siku!

Nadhani baada ya hapo waliokuwa madarakani watakaposhughulikiwa na sheria mbovu ambazo watu walipaza sauti zisitumike vibaya na ikiwezekana zibadilishwe wao walikuwa wakikenua meno kwa furaha!,Hapo ndipo vilio vya kubadilishwa kwa sheria mmbovu kitasikika kila kona!

Bila walioko madarakani kuonja joto la Ubovu wa Katiba na sheria mbovu hawawezi elewa!,Kwasasa wanaona kama wao ndiyo wamiliki halali wa hili Taifa,Watu wengine wote wanapaswa kufa!

Sheria iko wazi,Kwamba mtuhumiwa anapokamatwa apelekwe mahakamani ili mahakama ikaone kama anayo hatia au hana,Ila kwa kiburi kwa kuvunja sheria wanaamua kuendelea kumtesa mtuhumiwa wakiamini hakuna wa kuwafanya lolote!

Naomba Mungu hata siku nikifa hii comment ibaki kama ushahidi wa nilichokisema!

Iko siku isiyokuwa na jina sheria hizi na katiba hii itawaumiza wao,hapo ndipo watalia na kusaga meno!
Yaani umeongea vizuri sana. Mh Polepole enzi za Magufuli kipindi akina Tundulisu wanatunguliwa kwa risasi yeye alikuwa anawakebei Watanzania na kuwauliza kama wanayajua Magari ya V8... Zamu yake ilipowadia Kikamlamba vizuri....
 
Back
Top Bottom