Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Shekhe Mwaipopo mbona Yuko Mtaani adunda!?Kaacha kazi ya kuelimisha jamii kageukia kuelimisha jinsi ya kukiwasha kuitengua kiuno Jamii ✍️
Kaacha kazi ya kuelimisha jamii kageukia kuelimisha jinsi ya kukiwasha kuitengua kiuno Jamii ✍️
Nabii una maana gani kwa maneno yako?Kaacha kazi ya kuelimisha jamii kageukia kuelimisha jinsi ya kukiwasha kuitengua kiuno Jamii ✍️
Hii ni migogoro isiyo ya lazima, serikali ijitafakali!Chama cha Wanataaluma cha Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) kimeenda Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kupinga kushikiliwa kwa muda mrefu bila dhamana kwa mhadhiri mwenzao, Melkisedeki Kitunzi Kaijage, anayetuhumiwa na Jeshi la Polisi kuhamasisha maandamano kupitia mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa taarifa ya ndani iliyotolewa na Katibu Mkuu wa UDOMASA tarehe 18 Julai, 2026, Kaijage aliripoti Kituo cha Polisi UDOM tarehe 8 Julai akitakiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO). Baadaye alihamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na kisha Kituo Kidogo cha Chang'ombe ambako anaendelea kushikiliwa hadi sasa.
UDOMASA inaeleza kuwa jitihada zao za kumsemea dhamana ziligonga mwamba baada ya maafisa wa polisi kueleza kuwa kuna "maagizo kutoka juu" ya kumrejesha mahabusu, licha ya kukiri kuwa kosa linalomkabili linadhaminika kisheria:
"UDOMASA inatambua na kusimamia haki za wafanyakazi, na tunapinga na kulaani vikali ukiukwaji wowote wa taratibu za kisheria unaomnyima mfanyakazi uhuru wake. Chini ya sheria za nchi yetu, mtuhumiwa anapaswa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 24," ilieleza taarifa hiyo.
Soma Pia: Mhadhiri UDOM akamatwa kisa Maandamano ya Sabasaba
Baada ya juhudi za dhamana kukwama, UDOMASA kupitia jopo lake la wanasheria ilifungua shauri Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma tarehe 12 Julai, 2026.
Shauri hilo lilisikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe 17 Julai na linatarajiwa kuendelea tena kesho Jumanne, Julai 21, 2026, majira ya saa 3:00 asubuhi. Uongozi wa UDOMASA umewataka wanataaluma kuwa watulivu wakati taratibu za kisheria zikiendelea.
Uonevu wa hali juu,halafu mnasema,mnaamani,kama kafanya kosa si apelekwe mahakamaniChama cha Wanataaluma cha Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) kimeenda Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kupinga kushikiliwa kwa muda mrefu bila dhamana kwa mhadhiri mwenzao, Melkisedeki Kitunzi Kaijage, anayetuhumiwa na Jeshi la Polisi kuhamasisha maandamano kupitia mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa taarifa ya ndani iliyotolewa na Katibu Mkuu wa UDOMASA tarehe 18 Julai, 2026, Kaijage aliripoti Kituo cha Polisi UDOM tarehe 8 Julai akitakiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO). Baadaye alihamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na kisha Kituo Kidogo cha Chang'ombe ambako anaendelea kushikiliwa hadi sasa.
UDOMASA inaeleza kuwa jitihada zao za kumsemea dhamana ziligonga mwamba baada ya maafisa wa polisi kueleza kuwa kuna "maagizo kutoka juu" ya kumrejesha mahabusu, licha ya kukiri kuwa kosa linalomkabili linadhaminika kisheria:
"UDOMASA inatambua na kusimamia haki za wafanyakazi, na tunapinga na kulaani vikali ukiukwaji wowote wa taratibu za kisheria unaomnyima mfanyakazi uhuru wake. Chini ya sheria za nchi yetu, mtuhumiwa anapaswa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 24," ilieleza taarifa hiyo.
Soma Pia: Mhadhiri UDOM akamatwa kisa Maandamano ya Sabasaba
Baada ya juhudi za dhamana kukwama, UDOMASA kupitia jopo lake la wanasheria ilifungua shauri Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma tarehe 12 Julai, 2026.
Shauri hilo lilisikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe 17 Julai na linatarajiwa kuendelea tena kesho Jumanne, Julai 21, 2026, majira ya saa 3:00 asubuhi. Uongozi wa UDOMASA umewataka wanataaluma kuwa watulivu wakati taratibu za kisheria zikiendelea.
Yaani umeongea vizuri sana. Mh Polepole enzi za Magufuli kipindi akina Tundulisu wanatunguliwa kwa risasi yeye alikuwa anawakebei Watanzania na kuwauliza kama wanayajua Magari ya V8... Zamu yake ilipowadia Kikamlamba vizuri....Kwa Katiba yetu hii mbovu ipo siku naamini Rais atatoka Upinzani,Haijalishi itachukua muda gani lakini itatokea siku!
Marekani imewachukua miaka mingi sana kumpata Rais mwenye asili ya Afrika naamini hata Tanzania iko siku tu isiyokuwa na jina,Kwenye sheria mbovu na katiba mbovu hii iko siku!
Nadhani baada ya hapo waliokuwa madarakani watakaposhughulikiwa na sheria mbovu ambazo watu walipaza sauti zisitumike vibaya na ikiwezekana zibadilishwe wao walikuwa wakikenua meno kwa furaha!,Hapo ndipo vilio vya kubadilishwa kwa sheria mmbovu kitasikika kila kona!
Bila walioko madarakani kuonja joto la Ubovu wa Katiba na sheria mbovu hawawezi elewa!,Kwasasa wanaona kama wao ndiyo wamiliki halali wa hili Taifa,Watu wengine wote wanapaswa kufa!
Sheria iko wazi,Kwamba mtuhumiwa anapokamatwa apelekwe mahakamani ili mahakama ikaone kama anayo hatia au hana,Ila kwa kiburi kwa kuvunja sheria wanaamua kuendelea kumtesa mtuhumiwa wakiamini hakuna wa kuwafanya lolote!
Naomba Mungu hata siku nikifa hii comment ibaki kama ushahidi wa nilichokisema!
Iko siku isiyokuwa na jina sheria hizi na katiba hii itawaumiza wao,hapo ndipo watalia na kusaga meno!