Maagizo kwa Mbunge wangu wa Jimbo la Lulindi

Maagizo kwa Mbunge wangu wa Jimbo la Lulindi

Wamonyo

New Member
Joined
Dec 13, 2020
Posts
3
Reaction score
3
Kwanza kabisa nataka kukupongeza kwa ushindi wa kishindo ambao umeupata,wewe pamoja na raisi wako wa JMT Raisi JPM kwa ushindi wenu na chama kwa ujumla. Najua unakazi ngumu sana ya kulijenga na kulitetea jimbo lako kwa miaka mingine tena 2025-2030 kama mwenyezi mungu atakujalia. Japo najua haikua raisi kupata huo ushindi ndani ya chama chetu cha mapinduzi CCM lakini mwenyezi mungu katupa ushindi wa kihistoria ambao umetufanya mpaka sasa tufike hapa tulipo.

Lengo langu nikutaka kukumbusha ju ya changamoto ambazo zipo ndani ya jimbo letu ambazo tangu mfumo wa vyama vingi umeanza tumepata wabunge ambao wameshindwa kutimiza matakwa ya wana lulindi na ambao wametufanya kuwa na changamoto nyingi sana na baadhi yao walikua ata viongozi wakubwa ndani ya serikari.

ukiwa kama mbunge mambo yafuatayo kayasimamie.

(1) Kusimamia suala la elimu hasa kuhakikisha unaboresha miundombinu ya shule mfano shule ya msingi Mtakuja iliyopo kata ya lulindi nyumba za walimu zinatia aibu.

(2) Barabara ya kutoka Masasi kwenda Newala kipande kidogo cha lami kimebaki ambacho Raisi JPM alikiahidi atakimarizia nadhani Mh Raisi analitambua ilo.

(3) Huduma ya umeme vijiji REA kunabaadhi ya vijiji mpaka leo havijawashiwa umeme na nguzo zimepita muda mrefu sana mfano kijiji cha chiwambo mpaka leo haijajulikana umeme utawashwa lini.

(4) Huduma ya daraja ambalo linaunganisha kati ya Lulindi na Chiwambo ni daraja ambalo lilijengwa enzi za mama Anna Abdallah na kwa sasa ukilitazama mda wowote laweza sababisha maafa

By OMARY NAKANGA RAIA MTIIFU
[email protected]
 
Kwani Kama ni mbunge wako,hupajui ofisini kwake hadi uje hapa jamvini kutoa povu?
 
Kuna sehemu umeme umepita haujawashwa umeenda kuwashwa vijiji vya mbele
 
Back
Top Bottom