Maajabu: Inawezekana vipi mashabiki wa kigeni kuwa wengi kuliko wenyeji?

Rhz4567

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2018
Posts
4,893
Reaction score
6,599
Mwenye macho haambiwi tazama Leo Taifa kwa ujumla wamepata aibu yaani kwenye mechi ya Taifa starz VS DR Congo.
Mashabiki wa congo wengi kuliko mashabiki wa Taifa Starz ndani ya uwanja wa nyumbani B.W.Mkapa stadium? Kweli?

Hivi ni kwasababu watanzania hawapendi timu yao ya Tanzania au wacongo kwasasa hapa Dar es salaam ni wengi sana?

Mtaani wacongo wamejaa wanatubeza sisi ni watoto hatujui mpira.
Eti wanasema sisi watatusaidia kufuzu afcon kwa kuwafunga Ethiopia na Guinea. Na sisi Tanzania tushinde mechi zote ndy msaada wao kwetu kama majirana wao . Wanatupenda

Tokos.
 
Ushindi umewafanya waonekane wengi ila kiuhalisia walikuwa wachache. Basi zilizowabeba zilikuwa kama 8 hivi.
65x8=520 ukichanganya na wengine hawafiki hata 1,000.

Ila wakongo wanajitoa sana kuisapoti timu yao licha ya baadhi yao kuzuiwa kuingia uwanjani.
 
Maajabu Mbona ni Mengi tu..!

Wananchi Walikuwa wanajinasibu kwamba Kwenye timu Wachezaji Wa Yanga ndio Wengi..., Ajabu Sasa baada ya Vichapo vya Mwana ukome nje ndani Wamepoa kimyaa kama sio Wao Walikuwa wanatupigia Kelele.
 
Wanaushabikia mkongo sio wakongo.

Wabongo waongo kikongo hawakijui wanaujua mkongo

Tuwakonge wakongo wabongo walohama kongo kuja bongo kwa hongo.

HII MISTARI INA VINA
 
Wengine hao ni ndugu zetu. Ni watanzania ila wenye asili ya Mataifa mengine pia. Damu nzito, unapima unaona uwatose kichwa cha mwendawazimu. Ushangilie bataokota benyewe kwa nyavu.
 
Mwenye macho haambiwi tazama Leo Taifa kwa ujumla wamepata aibu yaani kwenye mechi ya Taifa starz VS DR Congo.
Mashabiki wa congo wengi kuliko mashabiki wa Taifa Starz ndani ya uwanja wa nyumbani B.W.Mkapa stadium? Kweli?

Hivi ni kwasababu watanzania hawapendi timu yao ya Tanzania au wacongo kwasasa hapa Dar es salaam ni wengi sana?

Mtaani wacongo wamejaa wanatubeza sisi ni watoto hatujui mpira.

Tokos.
Yuleyule ambaye sifa huwa zinaenda kwake kipindi cha matokeo mazuri hata sasa lawama zimuendee popote alipo.
 
Wanaushabikia mkongo sio wakongo.

Wabongo waongo kikongo hawakijui wanaujua mkongo

Tuwakonge wakongo wabongo walohama kongo kuja bongo kwa hongo.

HII MISTARI INA VINA
Mshangazi.

Hili bonge la nyimbo.
 
Mwenye macho haambiwi tazama Leo Taifa kwa ujumla wamepata aibu yaani kwenye mechi ya Taifa starz VS DR Congo.
Mashabiki wa congo wengi kuliko mashabiki wa Taifa Starz ndani ya uwanja wa nyumbani B.W.Mkapa stadium? Kweli?

Hivi ni kwasababu watanzania hawapendi timu yao ya Tanzania au wacongo kwasasa hapa Dar es salaam ni wengi sana?

Mtaani wacongo wamejaa wanatubeza sisi ni watoto hatujui mpira.

Tokos.
RDC ....Eloko ya makasi
 
Ushindi umewafanya waonekane wengi ila kiuhalisia walikuwa wachache. Basi zilizowabeba zilikuwa kama 8 hivi.
65x8=520 ukichanganya na wengine hawafiki hata 1,000.

Ila wakongo wanajitoa sana kuisapoti timu yao licha ya baadhi yao kuzuiwa kuingia uwanjani.
Aleez ale Leopards
RDC Eloko ya makasi
Ni wazalendo kwa nchi Hadi timu yao
 
Back
Top Bottom