Maajabu Jimbo la Igalula kata ya Loya, Taasisi za umma na Serikali kutounganishwa kwa umeme

Maajabu Jimbo la Igalula kata ya Loya, Taasisi za umma na Serikali kutounganishwa kwa umeme

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2019
Posts
9,863
Reaction score
20,806
Wananchi

Poleni Sana nimepata malalamiko yenu Kuwa taasisi za umma kama msikiti,makanisa,shule ya msingi Loya Bondeni,shule ya sekondari Loya na cha ajabu kabisa hata kituo cha polisi cha Loya eti hakuna umeme!
Nilipo jaribu kuwahoji wahusika wanaotokea kata Hiyo tatizo hasa ni nini!!?

"Surveyor wa Tanesco aliekuja alifanya survey eneo la Kati hapo pekee kwenye wafanyabiashara wa maduka halafu kwingine aliacha kabisa ndio Maana umeme umeishia senta pekee hata baadhi ya mitaa HAINA umeme kabisa ikiwemo Taasisi za umma na serikali kwa ujumla""

Kwa taarifa nilizonazo ni Kuwa nyumba NYINGI hazina umeme kuliko zenye umeme na shirika linahujumiwa kwa kukosa wateja wa UMEME.

Katika kata Hiyo UMEME umefanywa kuwa dili kwa uuzaji holela wa nguzo HIZO kwa wenye uwezo wa kuzinunua kuliko ilivyo utaratibu wa KAWAIDA.

Nimuombe Mbunge mwenye dhamana afanye hima kuwapigania wananchi wake wapate huduma hiyo kwa haraka Ili Tanesco wapate mapato ya kuendeleza miradi ya uzalishaji umeme nchini.

Ni matumaini yangu kuwa Mbunge wa Igalula venant Protas BADO ana ari ya kuwapigania wananchi wa Jimbo lake.

Asanteni kwa kusoma.
 
Pia viongozi wa CHAMA Tawala kata ya Loya tangulizeni uzalendo!kama hata mnashindwa kuwapigania wananchi na Taasisi za umma kupata umeme!!?ni nini mnachoweza kufanya!!?
Badilikeni hasa Diwani,katibu wa ccm kata na VIONGOZI wengineo pambanieni wananchi!!!
 
Mbunge pia alipe madeni yake kule Arusha. Kun mjane nilimkuta anamlalamikia sana mpaka analia machozi. Venaa baba lipa watu Ili upate baraka, usiwatishe. Yule mama ni mjane
 
Mbunge pia alipe madeni yake kule Arusha. Kun mjane nilimkuta anamlalamikia sana mpaka analia machozi. Venaa baba lipa watu Ili upate baraka, usiwatishe. Yule mama ni mjane
Hata mimi nimesikia anawatisha watu wakimhoji KWENYE mikutano yake! sijajua tatizo ni Nini!!!!! Halafu kuna Jamaa washaanza kupiga jeramba KWENYE Jimbo hilo!!
 
Si mlishaambiwa hakuna umeme wa 27,000
Au bado mnaota jiwe..
NAJUA! LAKINI UMEME unapoletwa eneo husika kipaumbele kinakuwa TAASISI za umma na survey kufanyika ipasavyo Ili umeme uwafikie wananchi Sasa survey ya hovyo nguzo hazijasimikwa mtu unaingizaje UMEME Sasa!!!?Nguzo zinauzwa KWA watu kiholela Hadi 150000/=unafikiri watu wa kawaida wanapataje umeme kama unahitajika nguzo Hata tano au sita alipo mteja!!?
 
Back
Top Bottom