Maajabu: Kamati yataka Malinzi apitishwe bila kuwepo

Maajabu: Kamati yataka Malinzi apitishwe bila kuwepo

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa TFF, Revocatus Kuuli amesema yuko tayari kujiuzuru baada ya kutofautiana na wajumbe wake juu ya hatma ya rais anayemaliza muda wake Jamal Malinzi.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ina wajumbe watano kati ya hao watatu na Makamu mwenyekiti Domina Madeli wanataka Malinzi apitishwe bila ya kuwepo jambo linalopigwa na mwenyekiti Kuuli.

Katika usahili huo wagombea 70 wamepitishwa kati ya 72, lakini ilipofika wakati wa kujadili jina la Malinzi ndipo wajumbe walipotofautina.

Akizungumza baada ya kuvunja kikao hicho Kuuli alisema usahili ulienda vizuri kwa wagombea wote, uamuzi wa kutumika busara kwa rais Malinzi umesababisha kutoelewana kwa wajumbe na kusababisha amvunja kikao hicho hadi kesho, Jumapili.

Kuuli alisema baadhi ya wajumbe wametaka busara itumike kwa wagombea ambao hawapo yaani Malinzi kuwa apitishwe hata kama hayupo na vielelezo vyake viletwe na mtu mwingine.

Kuuli alisema anaheshimu mawazo ya wenzake ila dhamira yake inamtuma kusimamia ukweli.

"Mtu hawezi kupitishwa wakati hakuwepo katika usahili na huo ndiyo msimamo wangu na kesho

Jumapili litaendelea kujadiliwa katika kikao hiki.

"Tukishindwana basi mimi nitajiuzuru kuwa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa TFF kwa sababu nina kazi nyingine za kufanya," alisema Kuuli.



WAPITISHWA KUWANIA NAFASI MBALIMBALI TWFA



Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake (TWFA), imetangaza majina ya wagombea 11 waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika Agosti 5, mwaka huu mkoani Morogoro.



Majina ambayo yamepitishwa ni Amina Karuma, Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu, Theresia Mung’ong’o, Hilda Masanche, Salma Wajeso, Zena Chande, Triphonia Temba, Mwamvita Kiyogoma, Jasmin Soudy na Chichi Mwidege.



Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.
 
anapitishwa kwa huruma za wana michezo! hili halinitii shaka!
 
Kile chama cha Mr Zero ndio watashangilia huu upuuzi wa mtu ambaye hakuwepo siku ya interview kuwa short listed
 
".....Kuuli alisema anaheshimu mawazo ya wenzake ila dhamira yake inamtuma kusimamia ukweli.

"Mtu hawezi kupitishwa wakati hakuwepo katika usahili na huo ndiyo msimamo wangu na kesho"...

SIKU ZOTE UKISIMAMIA UKWELI UTAONEKANA WA AJABU SANA
 
Back
Top Bottom