Maajabu: Kamati yataka Malinzi apitishwe bila kuwepo

Hizo ni dalili tu za kutaka kuonyesha umma kwamba hata tufanyeje hatumuondoi Malinzi.
Huyo bwana ameanza kujijenga kipindi kirefu na ametengeneza himaya kubwa miongoni mwa wanaofanya maamuzi ya soka.
Na ukionyesha mawazo tofauti unatupwa nje ya ulingo wa soka. Wenyewe wanadai wao ndo watu wa mpira!
Hawa wajumbe wasisikilizwe, wanachangia sana kuharibu na kuvuruga soka kwa kutuwekewa viongozi wasiostahili, utanismehe mkuu kama Malinzi hata ukimwangalia tu anaonekana ni mweupe kwenye soka
 
Kuna vitu vingine vinatia hasira. Malinzi anataka kujifanya kota pini ya baiskeli!
 
Hao wanaotaka Malinzi apitishwe bila uwepo wake ni kwa sababu walikuwa wanakula naye sahani moja, majambazi wanateteana siku zote.
 
Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa TFF, Revocatus Kuuli amesema yuko tayari kujiuzuru baada ya kutofautiana na wajumbe wake juu ya hatma ya rais anayemaliza muda wake Jamal Malinzi.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ina wajumbe watano kati ya hao watatu na Makamu mwenyekiti Domina Madeli wanataka Malinzi apitishwe bila ya kuwepo jambo linalopigwa na mwenyekiti Kuuli.

Katika usahili huo wagombea 70 wamepitishwa kati ya 72, lakini ilipofika wakati wa kujadili jina la Malinzi ndipo wajumbe walipotofautina.

Akizungumza baada ya kuvunja kikao hicho Kuuli alisema usahili ulienda vizuri kwa wagombea wote, uamuzi wa kutumika busara kwa rais Malinzi umesababisha kutoelewana kwa wajumbe na kusababisha amvunja kikao hicho hadi kesho, Jumapili.

Kuuli alisema baadhi ya wajumbe wametaka busara itumike kwa wagombea ambao hawapo yaani Malinzi kuwa apitishwe hata kama hayupo na vielelezo vyake viletwe na mtu mwingine.

Kuuli alisema anaheshimu mawazo ya wenzake ila dhamira yake inamtuma kusimamia ukweli.

"Mtu hawezi kupitishwa wakati hakuwepo katika usahili na huo ndiyo msimamo wangu na kesho

Jumapili litaendelea kujadiliwa katika kikao hiki.

"Tukishindwana basi mimi nitajiuzuru kuwa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa TFF kwa sababu nina kazi nyingine za kufanya," alisema Kuuli.

WAPITISHWA KUWANIA NAFASI MBALIMBALI TWFA

Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake (TWFA), imetangaza majina ya wagombea 11 waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika Agosti 5, mwaka huu mkoani Morogoro.

Majina ambayo yamepitishwa ni Amina Karuma, Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu, Theresia Mung’ong’o, Hilda Masanche, Salma Wajeso, Zena Chande, Triphonia Temba, Mwamvita Kiyogoma, Jasmin Soudy na Chichi Mwidege.

Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.
wanaofanya interview ya kuomba kazi hawapati kazi,,ambao hawafanyi interview wanapata kazi hahahaha
 
Huwezi kusailiwa bila kuwepo! Wakitaka waahirishe uchaguzi hadi Malinzi atoke ili wamsaili! Vinginevyo hicho ni kituko kinachopatikana bongo tu!
 
Malinzi alishatoa mwongozo kama mbwai na iwe mbwai.
Alishaandaa wajumbe kifikra na kifedha kuwa anastahili kuongoza TFF kwa miaka mingine minne.

Anahisi ni mchezo anachezewa wa kukamatwa siku chache kabla ya usaili na uchaguzi ili awe disqualified.

Sasa ameamua kutumia wajumbe ili kuleta sintofahamu. Naona ameshakuwa na ujasiri wa Ndolanga .....
 
Malinzi ni watuhumiwa, hawana kosa mpaka sasa huwezi kuwamosesha kuchaguliwa
 
Wakilazimisha kumchagua malinzi ndo wanamuangamiza maana serikali itampiga mvua ya miaka jela
 
Kwani uchaguzi mkuu wa 2015 Bw.Malinzi alikuwa upande gani vilee?
 
Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa TFF, Revocatus Kuuli amesema yuko tayari kujiuzuru baada ya kutofautiana na wajumbe wake juu ya hatma ya rais anayemaliza muda wake Jamal Malinzi.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ina wajumbe watano kati ya hao watatu na Makamu mwenyekiti Domina Madeli wanataka Malinzi apitishwe bila ya kuwepo jambo linalopigwa na mwenyekiti Kuuli.

Katika usahili huo wagombea 70 wamepitishwa kati ya 72, lakini ilipofika wakati wa kujadili jina la Malinzi ndipo wajumbe walipotofautina.

Akizungumza baada ya kuvunja kikao hicho Kuuli alisema usahili ulienda vizuri kwa wagombea wote, uamuzi wa kutumika busara kwa rais Malinzi umesababisha kutoelewana kwa wajumbe na kusababisha amvunja kikao hicho hadi kesho, Jumapili.

Kuuli alisema baadhi ya wajumbe wametaka busara itumike kwa wagombea ambao hawapo yaani Malinzi kuwa apitishwe hata kama hayupo na vielelezo vyake viletwe na mtu mwingine.

Kuuli alisema anaheshimu mawazo ya wenzake ila dhamira yake inamtuma kusimamia ukweli.

"Mtu hawezi kupitishwa wakati hakuwepo katika usahili na huo ndiyo msimamo wangu na kesho

Jumapili litaendelea kujadiliwa katika kikao hiki.

"Tukishindwana basi mimi nitajiuzuru kuwa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa TFF kwa sababu nina kazi nyingine za kufanya," alisema Kuuli.

WAPITISHWA KUWANIA NAFASI MBALIMBALI TWFA

Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake (TWFA), imetangaza majina ya wagombea 11 waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika Agosti 5, mwaka huu mkoani Morogoro.

Majina ambayo yamepitishwa ni Amina Karuma, Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu, Theresia Mung’ong’o, Hilda Masanche, Salma Wajeso, Zena Chande, Triphonia Temba, Mwamvita Kiyogoma, Jasmin Soudy na Chichi Mwidege.

Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.

Nakumbuka ya jangiri Hassan Hasanoo hivi hivi sijui kafia wapi Simba mnavibaka wengi wanaishi kiujanjaujanja
 
Back
Top Bottom