Maajabu kwenye biashara ya jeans

BAMIZER

Member
Joined
May 2, 2022
Posts
52
Reaction score
62
Nimepata utata baada ya kugundua suruali za jeansi zinauzwa MAKAMBAKO elfu 16 Kwa bei ya jumla. Lakini Dar zinauzwa elfu20kwa (bei ya jumla ) na kuendelea. Ivi hapo Siri ni nini naombeni tujadili kidogo
 
Biashara ni ujanja sana, lakini kodi ya pango kkoo ni kubwa kuliko huko makambako ndani ndani, angalia quality pia. Hata hivyo kuwa makini nyingine za wizi.
Qualiti ni Ile Ile. Lakini nadhani huku Makambako wakinga wanatumia mfumo ule wa kuvunja bei. Yaani anauza pic nyingi lakini Kwa faida ndogo per item. Ukizingatia pic anazo ziuza so inalipa Sana. Tofauti na mtu anaye uza bei ya juu lakini anauza kidogo
 
Nime pata utata baada ya kugundua suruali za jeansi zinauzwa MAKAMBAKO elfu 16 Kwa bei ya jumla. Lakini dar zinauzwa elfu20kwa (bei ya jumla ) na kuendelea. Ivi hapo Siri ni nini naombeni tujadili kidogo
 
Labda na mimi niongeze kitu.
Kuna dada alikuwa anauza nguo online, wakati wa kupiga story kasema

Ananunua.
1. Shati 12000
2. T-shirt 12000

Sasa nikamuuliza wewe unachukulia wap?? Kasema kariakooo!

Kuna siku nikamwomba nimpeleke kariakoo nikamwoneshe machimbo.

Nikampeleka sehemu ambazo
1. Shirt na t-shirt ni 8000

Ninachotaka kusema ni kwambaa biashara ni siri na kila mtu anajua sira ya kile anachokifanya.

Mfano. Fred vunja bei, sio kwamba ety mchawi hapana, yeye anataka faida ndogo na vitu vyake ni quality.
 
Acha upambe unasifia mpaka bossi anaona unaharibu

Anaquality ipi ya jeans huyo uliomtaja

Sent from my nokia JamiiForums mobile app
 
Nime pata utata baada ya kugundua suruali za jeansi zinauzwa MAKAMBAKO elfu 16 Kwa bei ya jumla. Lakini dar zinauzwa elfu20kwa (bei ya jumla ) na kuendelea. Ivi hapo Siri ni nini naombeni tujadili kidogo
Me najua jinsi zipo za 8000, 10000, 12,000, 15000 na 16000
Hapa inabidi uwe unajua chimbo maana jinsi ya 12 na 16 ukiangalia kwa haraka haraka hazina tofauti ki vile
 
Nime pata utata baada ya kugundua suruali za jeansi zinauzwa MAKAMBAKO elfu 16 Kwa bei ya jumla. Lakini dar zinauzwa elfu20kwa (bei ya jumla ) na kuendelea. Ivi hapo Siri ni nini naombeni tujadili kidogo

Dar gani kaka unasemea na jinsi za aina gani? Tunanunua jeans elfu 6 jumla dar zile za kike skin jeans boyfriend jeans shorts za jeans na vigaun vya jeans kila moja ukichukua mzigo mkubwa jumla ni elfu 6 kwa pc moja
Rejareja elfu 7 kwa pic moja na bado mkoan hata nikiuza 15 inalipa
 
Kama quality ya nguo ni Ile Ile Jibu ni jepesi tu ilo duka la dar uliloenda kununua jeans 20000 Kwa bei ya jumla ni duka na jumla wanalouza nguo rejareja Yani Hilo sio sio duka la jumla ni duka la rejareja ila.wanakudanganya wanauza jumla.na inawezekana wanunua mzigo Kwa mtu wa jumla anayeuziwa jumla.mfano ukienda kununua mzigo Kwa Fred vunja wa jumla bei atakayekuuzia Fred vunja bei sio sawa na bei ambayo ungeenda kununua mzigo Kwa boss anayemuuzia mzigo Fred vunja ndio maana wanaweka bei kubwa.ili wapate faida.na Hilo duka la makambako analouza nguo.jumla 16 uyo atakua anunua mzigo.kwa wale.manguli kabisa Yani ananua mzigo Kwa wale masupplies wa jumla kabisa wanatoa mzigo china kwahyo anachukua mzigo mkubwa Kwa bei ndogo au yawezekana anaagiza china moja Kwa moja
 
Nimepata utata baada ya kugundua suruali za jeansi zinauzwa MAKAMBAKO elfu 16 Kwa bei ya jumla. Lakini Dar zinauzwa elfu20kwa (bei ya jumla ) na kuendelea. Ivi hapo Siri ni nini naombeni tujadili kidogo

Hujui machimbo kkoo mbona mpk 14500 kkoo mzee
 
Acha upambe unasifia mpaka bossi anaona unaharibu

Anaquality ipi ya jeans huyo uliomtaja

Sent from my nokia JamiiForums mobile app

[emoji28]

Vunja bei hovyo kabisa izo nguo anazo zatangaza wanavaaga sijui watu gan aisee na wamavaaga wakiwa wanakwenda wapi Mana ni full hovyoo

Lkn quality mbona anauza bei sanaaa
 
Nguo za vunjabei ukifua mara mbili tu nguo hiyo huwezi kuivaa kwenye tukio muhimu

Kwanza manguo yake utayavalia wap mzee maisha kwenda mara mbili dukan kwake sikuona chakununua aisee [emoji28]
 
Kariakoo Jeans quality kuanzia elfu 15 mpaka 22 kwa bei ya jumla. Ukiona jeans inauzwa makambako kwa jumla elfu 16 basi ujue kwamba atakuwa anaagiza mwenyewe kutoka china. Unaweza kuta mtu ana duka kariakoo na huko makambako pia. Lakini pia kama jeans inauzwa bei hiyo jumla inawezekana ilinunuliwa SALE kutokana na kuwa mda mrefu dukani.

Kwa sisi ambao tumefanya kazi kariakoo mda mrefu bei zake elfu 15 to 22 jumla, ila zilishawahi ingia kadeti elfu 25 jumla. Kariakoo pia kuna nguo jumla elfu 30 usishangae kwa sababu inawezekana kampuni kubwa au brand za mataifa mengine (sio china). .

Kuna wafanyabiashara wanaenda kuchongesha nguo china, ikitokea nguo ikapendwa utaona wanaenda kutengeneza. Angalia tofauti kubwa kwenye majina ya kampuni na miundo ya mifuko. .
 
Nimepata utata baada ya kugundua suruali za jeansi zinauzwa MAKAMBAKO elfu 16 Kwa bei ya jumla. Lakini Dar zinauzwa elfu20kwa (bei ya jumla ) na kuendelea. Ivi hapo Siri ni nini naombeni tujadili kidogo
Tupeane connection
 
mzima dada mekufta inbox naitaji msaada wako kdgo
 
Nimeacha kusoma uzi kwa hasira baada ya kusema vitu vya Fred vunja bei ni quality [emoji276]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…