Maajabu: Niliamka katikati ya ndoto lakini bado nikabaki usingizini, na nikijaribu kujiamsha inashindikana kabisa

Maajabu: Niliamka katikati ya ndoto lakini bado nikabaki usingizini, na nikijaribu kujiamsha inashindikana kabisa

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Baada ya kujaribu mara kadhaa ili niamke na kushindikana nikaona isiwe tabu, wacha nitulie tu labda nitaamka mwemyewe tu, lakini ikawa inashindikana.

Baada ya kuwaza kidogo, nikaona nijaribu ku-imagine naendesha V8 nione itakuwaje, kweli bhana, kugeuza shingo naona V8 nyeusi kalii imeandikwa jina langu kwenye plate number, nikapanda na kuanza safari yangu kuelekea ikulu.

Hazikupita sekunde nyingi nikajikita nipo nafunguliwa geti la Ikulu, nikapaki na hata sikufahamu nimfuata nini hapo. Ilikuwa raha sana mule ndani ya ikulu, eti nikamuona Mwigulu wanajadili na mabeberu mpango wa kuanzisha tozo ya kuvuta hewa, kwamba eti tuwe tunalipia hewa tunayovuta kama vifurushi vya simu, bando lako la hewa likikata basi unaenda kurenew TRA, hahah. Na wakamwambia kama hufanyi hivyo hatuwezi kukupa tena mkopo.

Hahahah, nilishtuka na kuamka mwenyewe!
 
Mwigulu Babu tozo
Kumbe sio kwamba Mwigulu anapenda tozo, hata yeye hapendi hizi tozo, tatizo bi.mikopo anasukumiziwa mikopo ya ajabu ajabu, na hizo tozo ni moja wapo ya masharti ya mikopo.
 
Back
Top Bottom