MAAJABU: Nyama kutoiva baada ya kuchemshwa masaa 4.45

MAAJABU: Nyama kutoiva baada ya kuchemshwa masaa 4.45

bampami

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2011
Posts
5,699
Reaction score
4,117
Habarini za saa hizi wandugu?

Leo nilienda kununua nyama ya ng'ombe buchani yapata robo kilo kutokana na mlaji niko peke yangu getto. Maajabu ni kuwa nilianza kuchemsha kwa jiko la gas mida ya kumi na mbili jioni.

Lakini mpaka sasa nazungumza mida ya saa nne na robo nyama kila nikionja haijaiva japokuwa nilikatia tangawizi ndani na kukamulia limau .Nimepatwa na mshtuko kidogo kwanini?

Wataalam wa mapishi, naomba msaada wenu nimekosea nini? ningeweza kuuliza majirani zangu ila tunaishi kila kila mtu kivyake jamani.

Ahsanteni
 
Mara nyingi wanasema ukiona nyama inachelewa kuiva basi ujue ni ya mtu,umeinunua ya ng'ombe kama kiini macho pole sana mkuu.
 
Mie nisingeila.
Kama umeila una moyo aiseee.
Na hilo bucha nisingenunua tena.
 
Umekosea bucha mkuu.. nadhani badala ya kwenda bucha la nyama ng'ombe wew umeenda la punda[emoji1787]
 
Nashukurj ile nyama sikuila niliitupa kwenye kidastibini changu nje. Leo naenda kuicheki yaani hata haijaoza iko vile vile..kibaya zaidi kuna paka wengi sana maeneo haa sijaona hata paka wakifungua dastibini kuila....Dah[emoji24]
 
Back
Top Bottom