MAAJABU: Nyama kutoiva baada ya kuchemshwa masaa 4.45

MAAJABU: Nyama kutoiva baada ya kuchemshwa masaa 4.45

Nakumbuka Kuna story nlikuwa naisikiliza RFA kwenye kile kipindi Cha sito sahau,kunajamaa walikuwa wanajenga huko gambushi sa kuna siku walikuwa wakipika nyama ikawa haiivi inawezekana mkuu Upo pande hzo 😀.
 
Nashukurj ile nyama sikuila niliitupa kwenye kidastibini changu nje. Leo naenda kuicheki yaani hata haijaoza iko vile vile..kibaya zaidi kuna paka wengi sana maeneo haa sijaona hata paka wakifungua dastibini kuila....Dah[emoji24]
Ushauziwa mbwaa kama sio pakaaa..[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
  • Thanks
Reactions: amu
Nashukurj ile nyama sikuila niliitupa kwenye kidastibini changu nje. Leo naenda kuicheki yaani hata haijaoza iko vile vile..kibaya zaidi kuna paka wengi sana maeneo haa sijaona hata paka wakifungua dastibini kuila....Dah[emoji24]
Tupe updates kesho tena asubuhi.
 
Binafsi naogopa hasa mie mpenda kula kula nyama nikiwa safarini.
Huwa naona safe kula nyama choma kuliko kuna mavyakula mengine.
 
Habarini za saa hizi wandugu?

Leo nilienda kununua nyama ya ng'ombe buchani yapata robo kilo kutokana na mlaji niko peke yangu getto. Maajabu ni kuwa nilianza kuchemsha kwa jiko la gas mida ya kumi na mbili jioni.

Lakini mpaka sasa nazungumza mida ya saa nne na robo nyama kila nikionja haijaiva japokuwa nilikatia tangawizi ndani na kukamulia limau .Nimepatwa na mshtuko kidogo kwanini?

Wataalam wa mapishi, naomba msaada wenu nimekosea nini? ningeweza kuuliza majirani zangu ila tunaishi kila kila mtu kivyake jamani.

Ahsanteni

Labda unapika maharage katika ulimwengu wa koroho.
 
Nyama ya ng'ombe kuanzia lisaa limoja tu unaweza kula supu!! Nyama ya "NGUBI" aka Chairfire nusu saa unatafuna vizuri tu!!
 
Back
Top Bottom