Maajabu Uchaguzi Kenya!

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Katika hali ambayo imenistaajabisha sana tume inayoitwa huru ya Kenya IEBC imetumia Dolla za Kimarekani millioni 226 ($ 225 mill.) au Dolla 16 ($16) kwa Mpiga kura, kwa kulinganisha tu Marekani pamoja na mbwembwe zao zote wanatumia chini ya Dolla 1 ($1) kwa mpiga kura, Ghana senti 70 (Dolla) na Uganda dollar 4 ($ 4) kwa kila Mpiga kura, na pamoja na ughali wote huo bado watu wanakataa Matokeo na wanataka Uchaguzi urudiwe! Duh!
 
Waafrica tuna hela tatizo ni jinsi ya kupanga matumizi.. hahaa kazi ipo
 
Demokrasia ni gharama ndugu. Kwahiyo unataka kusema hata katiba ikivunjwa (inayotetea demokrasia) kwa namna yoyote ile ikiwemo wizi wa uchaguzi,basi iwe funika kombe mwanaharamu apite? Hayo yapo Tanzania tu. Waache Wakenya iwagharimu,ndo mwanzo wa maendeleo.
 

Sio lazima kuingia gharama yote hiyo kwa nchi Maskini kwa kisingizio cha Demokrasia, na Wala kuwa na Demokrasia sio lazima uingie gharama kubwa kiasi hicho, mbona Ghana wamejaribu kwa ndogo kabisa?

 
Ndio maana kuna usemi "kupanga ni kuchagua"...

Na kweli naona jamaa wamechagua, inanikumbusha yule Mwanasiasa aliyesema ikibidi hata nyasi tutakula lkn lazima Mpendwa wetu Raisi tumnunulie ndege!
 
Sio lazima kuingia gharama yote hiyo kwa nchi Maskini kwa kisingizio cha Demokrasia, na Wala kuwa na Demokrasia sio lazima uingie gharama kubwa kiasi hicho, mbona Ghana wamejaribu kwa ndogo kabisa?

Ni sawa. Unaelewa kwanini gharama imekuwa kubwa hivyo? Mazingira ya Kenya na Ghana ni tofauti. Sababu kubwa mojawapo iliyofanya gharama kuwa kubwa ni BVR system. Hii ilitumia almost tsh 180 Billion,(9billion Ksh). Ukifatilia kuna makumpuni yaliomba tenda hiyo kwa a half the cost, lakini muda wa maandalizi ulikuwa mfinyu,hivyo wakaangukia kwenye figure hiyo. Pili, mazingira ya kutoaminiana yaliyosababisha machafuko yale, so they had to implement some mechanism,to avoid uncertainty!
 

Mkuu,

Usishangae, kosa lako ni kulinganisha uchaguzi huu, amabao ni wa kwanza wa aina hii kwa KE, na chaguzi zingine ambazo hazijabadilika kwa muda fulani.
Ukitaka kulinganisha fairly, basi chukua uchaguzi kutoka marekani au Ghana ama wengine amabao ulikuw baada ya kubadilisha sera au kubadilisha mitambo ya uchaguzi.

Mimi naamini gharama ya uchaguzi KE kuwa juu inatokana na mitambo mipya waliyonunua (sisemi ni mizuri wala sisemi hapakuwa na wizi / ufisadi). Yaani ninalo sema ni kuwa wakati wowote ule nchi inapo badilisha miundombinu ya uchaguzi gharama itapanda kwa uchaguzi unaofuata. Baadaye gharama inaonekana kuwa ndogo kwani mitambo mingi yenye kutumiwa imeshalipiwa tayari.
 

Lakini bado uncertainties zimetawala tu ktk Uchaguzi wote, na si ajabu ukarudiwa tena, nani anajua labda kwa gharama tena mara mbili ya hiyo, kwa upande wangu mimi mtu akiniuliza kama Uchaguzi ni aghali hivyo ni bora kuufuta tu na kuwekeza hizo pesa TPDC na kuchimba Mafuta wenyewe kuliko kupeleka kwenye uchaguzi ambao hata hivyo utaibiwa tu!
 
Kijakazi unawaza upuuzi gani ndugu? Kwahiyo unataka kusema Taifa liongozwe namna gani? Unaposema demokrasia (yaani mfumo wa utawala ) ni gharama kubwa, na hivyo utupiliwe mbali, unataka iweje? Wakikuyu waendelee kutawala (ipendavyo)milele? CCM iendelee kutawala milele (ipendavyo)?? Look here, even if it is going to cost half a trilion, yet let it be for the sake of A country. Watu walichinjana mwaka ule, au umesahau? Either Democracy or Dictatorship!
 
Last edited by a moderator:

Tatizo ni kwamba hiyo Demokrasia unayoiongelea haiwezi kupatikana kwa njia ya Uchaguzi hata siku moja, watafanya wanavyotaka lkn kila siku watakuwa wanapata matokeo yale yale kama sio mabaya zaidi, watatumia Mabilioni kwa ajili ya uchaguzi lkn bado, hawatapata matokeo tofauti!

Hao jamaa wanapiga kura kikabila, wamekuwa hivyo, wako hivyo na bado wataendelea kuwa hivyo, mpaka pale watakapokuja kutambua kwamba ili waondokane/kupunguza hilo tatizo ni lazima warudi nyuma na waangalie ni nini kimewafikisha hapo, ni kwa nini wako hivyo, watagundua kwamba Kenya ni product ya Divide and Rule ya Wazungu, kama ilivyo Rwanda Watusi na Wahutu, Zimbabwe Washona na Wandebele au Iraki Shia na Suni, ni lazima watumie njia ile ile waliyoitumia Wazungu kuwagawanya ili waweze kurekebisha, na hapo ndipo wanapopaswa kuanzia, lkn kufanya Uchaguzi ni ngazi ya mwisho!

Uchaguzi huu walifikiri wamepata Mwarobaini wa ukabila wao, lkn matokeo yamewasononesha sana pamoja na juhudi zote, Mtoto wa Kikuyu tangu mdogo anajua na anafundishwa kwamba Mjaluo ni adui na huwezi kutawaliwa na Mjaluo na Mtoto wa Kijaluo hivyo hivyo, sasa hilo huwezi kuliondoa kwa kufanya uchaguzi wa sijui electronic voting system blah blah blah....

 
Kwa Afrika kuna demokrasia gani, ningekuwa na katiba yangu napiga marufuku chaguzi Afrika nzima, pesa za chaguzi zitumike kwa maendeleo

Naungana na wewe 1000%, mimi nasema kila siku tunalalamika uwekezaji tunapata 3% ya mapato yote ya Dhahabu yetu, kisa hatuna pesa za kuchimba wenyewe Dhahabu yetu, sasa angalia Mgodi wa Buzwagi wa Barrick una thamani ya Dolla za Kimarekani $ 300 million, Uchaguzi wa Kenya umegharimu 225 million $ na bado kuna malalmiko lukuki watu wanataka urudiwe, sasa hiyo pesa kwa nini wasiitumie kuwekeza kwenye kuchimba Mafuta na kutoa ajira na kumilika Mafuta badala ya kuwapa Wazungu?

 
Sio lazima kuingia gharama yote hiyo kwa nchi Maskini kwa kisingizio cha Demokrasia, na Wala kuwa na Demokrasia sio lazima uingie gharama kubwa kiasi hicho, mbona Ghana wamejaribu kwa ndogo kabisa?


Marekani wanatumia hela ndogo kwa kuwa taasisi zake zinazoshughulika na maswala ya uchaguzi zimeimarishwa kitambo sana. Ghana pia ninaweza kusema wana 'mature' electoral system na hata haya mambo ya biometric kits wameiga wakenya kutoka ghana. Kenya ndo mara ya kwanza kununua hivyo vifaa. Uchaguzi ujao iwapo vitakuwepo basi gharama itakuwa ndogo.
 

Sio kweli Waghana hawatumii huo mfumo kama wa Wakenya na moja ya sababu kubwa ndio hiyo Gharama kubwa, ambayo haiendani na hali halisi ya Uchumi wao!

Pia sio kweli kwamba Wamarekani wanatumia gharama ndogo kwa sababu eti wameanza zamani, bali wanatumia gharama ndogo kwa sababu wametafuta jinsi ya kutumia gharama ndogo, ili pesa inayobaki iende sehemu nyingine, kwa kifupi Wakenya wangekuwa na akili hawakupaswa kutumia huu mfumo kwani walipaswa kujua kabla kwamba una gharama kubwa sana!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…