Maajabu Uchaguzi Kenya!

Maajabu Uchaguzi Kenya!

Sio kweli Waghana hawatumii huo mfumo kama wa Wakenya na moja ya sababu kubwa ndio hiyo Gharama kubwa, ambayo haiendani na hali halisi ya Uchumi wao!

Pia sio kweli kwamba Wamarekani wanatumia gharama ndogo kwa sababu eti wameanza zamani, bali wanatumia gharama ndogo kwa sababu wametafuta jinsi ya kutumia gharama ndogo, ili pesa inayobaki iende sehemu nyingine, kwa kifupi Wakenya wangekuwa na akili hawakupaswa kutumia huu mfumo kwani walipaswa kujua kabla kwamba una gharama kubwa sana!


Fanya utafiti. Biometric registration wakenya walisoma Ghana. Bado nasisitiza systems, materials zinazotumika hasa voting machines za wamarekani wamewekeza kitambo, yao ni maintenance. Kenya wamenunua, awali ni debe na counter books!
 
Katika hali ambayo imenistaajabisha sana tume inayoitwa huru ya Kenya IEBC imetumia Dolla za Kimarekani millioni 226 ($ 225 mill.) au Dolla 16 ($16) kwa Mpiga kura, kwa kulinganisha tu Marekani pamoja na mbwembwe zao zote wanatumia chini ya Dolla 1 ($1) kwa mpiga kura, Ghana senti 70 (Dolla) na Uganda dollar 4 ($ 4) kwa kila Mpiga kura, na pamoja na ughali wote huo bado watu wanakataa Matokeo na wanataka Uchaguzi urudiwe! Duh!

Afadhali wakenya wanaweka wazi kila kitu hata kama kiko gharama kiasi gani, Bongo ni balaa, hatujui uchaguzi wetu ulighalimu Shn'gapi kwa kichwa, hatujui Mkuu wa kaya analipwa ngapi, hatujui mikataba ikoje..kila kitu ni siri sirini!
 
Back
Top Bottom