Maajabu! Wezi wakata mauno usiku kucha wakiwa uchi baada ya kuiba gari

Aise nimegugumia kicheko hadi mbavu zinauma. Naona na kijua kimeanza kukolea.....leo watu watapiga acrobatics hapo hadi washangae. Wadada naona wanashangilia tu kuona kengele za wadau...hahahahaa
 
Kwa hiyo wamechukuana wagonjwa wawili wa akili wakakuta gari wakavua nguo na kuanza kucheza au?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwangu ni rahisi kukubali kwamba mtu kategesha kitu kwenye gari kinachompa mwizi ugonjwa wa akili kuliko kuamini "uchawi".

Ukiniambia kuna madawa yametegeshwa katika gari kiasi kwamba mtu akija kuiba atasababisha ku trigger madawa hayo kuenea kwenye gari na kumharibu akili apaki gari na kuvua nguo na kuanza kucheza ngoma uchi, hilo linaweza kuwa explained biologically na chemically.

Ukiniambia gari lina uchawi itabidi unieleze huo uchawi unafanya kazi vipi.

Sent from my Kimulimuli
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] sio singeli mkuu
 
Uchawi ni nini?

Unajuaje kwamba upo?

Sent from my Kimulimuli
1.Uchawi (kwa Kiingereza "Witchcraft") ni nguvu zinazotumiwa na watu wenye maarifa maalumu yasiyo ya kisayansi katika jamiinyingi duniani (zikiwemo za Afrika, Asia, Ulaya n.k.), ingawa kuna tofauti nyingi kulingana na mahali au utamaduni.

Lengo lake ni kujaribu bahati ya mtu na kujilinda na maadui wengine kiimazingara, au kwa ajili ya kujifurahisha, japo wenye imani potofu hulichukulia maanani na kupandikiza chuki kwa ndugu jamaa hata jirani kuwa ni mchawi.

Kwa mujibu wa vitabu vya dini uwezo na nguvu zote za asili ni za Muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo, hivyo yeye anampa mwanadamu uwezo kadiri tofautitofauti kama apendavyo, kwa maana uwezo huo hufanya kazi katika hali ya kubahatisha, yaani ni bahati, hakuna mwenye mamlaka ya kuongoza uwezo huo wa asili ila Mwenyezi Mungu.

Kadiri ya dini mbalimbali watu wote wanaotumia nguvu hizo za asili katika hali (hasi) wapo kinyume na Mungu Muumbaji wa mbingu na dunia, hawajui kuwa yeye ndiye mwanzilishi wa nguvu zote za asili ikiwa ni pamoja na wanadamu.

2.Kuwepo kwa matukio yanayoendana na imani ya kichawi na ambayo siyo ya kawaida Katika jamii: mfano; Angalia hii video
 
Umejibu swali moja kwa kutupa swali jingine.

Nguvu hizo ni zipi? Unajuaje kama zipo kweli na si hadithi tu?

Sent from my Kimulimuli
 
Umejibu swali moja kwa kutupa swali jingine.

Nguvu hizo ni zipi? Unajuaje kama zipo kweli na si hadithi tu?

Sent from my Kimulimuli
Uchawi upo tangu enzi za musa. Sasa sijui unatokea wapi usijue kama uchawi upo
 
Umejibu swali moja kwa kutupa swali jingine.

Nguvu hizo ni zipi? Unajuaje kama zipo kweli na si hadithi tu?

Sent from my Kimulimuli
Una miaka mingapi? na unaishi wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…