Kaka kuwa na diploma sio tatizo hata darasa la saba anaweza, kuna katibu mkuu ndie injini ya wizara katika utendaji. Tatizo ni kwamba hata katibu mkuu si mtu alie bobea kwenye mambo ya elimu yeye ni mwanasheria, waziri wa elimu kawambwa yeye si mwalimu pia ni mhandisi. Rais alishindwa kujua kwamba Mhadhiri si lazima awe mwalimu? Hawa ni wahadhiri na si walimu? Mwl ni yule alie soma ualimu ngazi mbali mbali kama cheti, diploma, shahada, masters, phd na kufundisha s/msingi au sekondari au chuo cha ualimu na si tu kuwa mhadhiri. Hapa rais aliingizwa chaka na washauri wake kumpa mchome wizara ya elimu!!! Hakuwaona akina Prof. OSAKI?