Wanabodi,
Hii vita ya Corona Tanzania inakumbana na twists and turns za ajabu ajabu!, kwa vile huu ni mlipuko wa ugonjwa, ilitegemewa madaktari Bingwa ndio wangekuwa wakombozi wa taifa letu kwenye janga hili, lakini kwa Tanzania ni maajabu matupu, badala ya Madaktari Bingwa wa Tiba! kuwa wakombozi wa taifa letu, Mkombozi wa kweli wa taifa letu kwenye hii vita ya Corona ni Bingwa wa Kemia, ndiye ametoa ushauri bora kabisa wa Kikemia wa namna bora ya kuikabiliana na janga hili la Corona ili kushinda vita hii.
Je, bingwa huyu wa Kemia ni nani na ametoa ushauri gani?
Andamana nami.
1. Background, Professionalism
Tangu kuanza kwa janga hili la Corona, mimi kama Mtanzania mzalendo wa kawaida kabisa nimeshiriki kikamilifu katika vita hii katika maeneo 5
- Kama Mtanzania tuu wa kawaida
- Kama Mwana jf kwa kuposti mabandiko elimishi.
- Kama mwandishi wa habari mzoefu kuandika habari kulisaidia taifa kwa uzoefu wangu.
- Kama mtangazaji wa nguli wa TV kupitia a weekly program yangu ambayo huwa live
- Kama mtu mwenye exposure, kuitumia exposure yangu kumulikia wengine.
Hivyo kwenye hayo maeneo 5 nimeshiriki kwa kutoa maoni mbalimbali, miongoni mwake ni ule ushauri wangu wa mwanzo kuwa zipo wizara zinaweza kuongozwa na Waziri mwanasiasa yoyote, lakini kuna wizara zinazo deal na serious technical issues, zinapaswa kuongozwa na mawaziri ma professionals wa fani husika. Moja ya wizara hizi ni Wizara ya Afya, hii inadeal na Afya na uhai wa Mtanzania, ilipaswa kuongozwa na daktari bingwa na sio a layman kwenye medical field!.
Tulipoanza tuu vita hii ile siku Waziri wa Afya akitangaza rasmi janga la Corona huku akiwa ameandamana na daktari Bingwa wa epidemiology kwa jina la Janet akizungumzia kuvaa face mask, daktari huyo akiwa mbele ya Waziri wa Afya alisema face mask zitavaliwa na madaktari tuu wanaohudumia wagonjwa. Nikapandisha bandiko humu na kusema it's not right kwasababu kama inachukua siku 14 kuibaini Corona kwa aliyeambukizwa, how will one knows hivyo to be on a safe side ni watu wote wavae facemasks kama China. Waziri angekuwa daktari pale pale angejua.
Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best! - JamiiForums
2. Mazungumzo na Naibu Waziri wa Afya
Kuna siku nimezungumza na Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndugulile, kama ilivyo kawaida yangu, mimi huwa nina maswali magumu. Miongoni mwa maswali niliyomuuliza Dr. Ndugulile ni swali la kwa vile Corona haina dawa, jee anaweza kueleza hao wagonjwa kwenye vituo vya matibabu wanafanywa nini au wana hudumiwa huduma gani ili Watanzania wenye uwezo waweze kuwahudumia wagonjwa wao ambao hawajazidiwa ili kuzuia hospitali zisielemewe. Dr. Alinigomea!.
Kisha nikamuuliza kwa vile Corona ni mafua, kwanini Wizara ya Afya isihamasishe alternative medicine ya watu kujitibu ili wengine wamalizane nayo juu kwa juu bila kuisumbua serikali na kupelekwa vituo vya huduma?.
Pia swali hili alinigomea na kusisitiza kila mwenye dalili aripotiwe.
Kwa kutumia uzoefu wangu wa exposure, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndugulile alikuwa ana majibu yote tena ya kidakitari, lakini kwa vile yeye sio Msemaji rasmi, Msemaji rasmi ni Waziri wake, na Waziri sio daktari, Dr. Ndugulile aliogopa kusema akapishana na Waziri wake, lakini Waziri wa Afya angekuwa ni daktari Bingwa, Dr. Ndugulile angezungumza.
Vita Janga la Corona: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho watakuwa live JLNH-Star TV - JamiiForums
Star TV: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Wazuri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile, Wanazungumzia Corona - JamiiForums
3. Bingwa wa Kemia Aingilia Kati
Hayo maswali mawili magumu niliyo muuliza Naibu Waziri wa Afya Dr. Faustine Ndugulile ambayo yalitakiwa kujibiwa na madaktari Bingwa wa tiba, leo yamepatiwa majibu badala ya kupatiwa majibu na madaktari Bingwa wa tiba, kitu cha ajabu sana kuhusu mapambano dhidi ya janga la Corona nchini Tanzania, maswali hayo yamepatiwa majibu na Bingwa wa Kemia.
Tanzania tulizoea viongozi wetu wakuu wa kisiasa huwa ni wanasiasa, hivyo ulipo tokea Bingwa wa Kemia alipoutaka urais, kiukweli kuna watu humu tulimshangaa!, tangu lini Bingwa wa Kemia akawa kiongozi wa siasa kuwa mkuu wa nchi?.
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli - JamiiForums
4. Bingwa wa Kemia ametoa ushauri wa Kikemia kuwa vurusi vimeumbwa kwa cells za protein in nature na kuzungukwa fatty acid hivyo vinayeyushwa au kwa kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka au sanitizers ambazo kikemia ni alcohol ambazo zinawayeyusha kwa kuyasaga mafuta au mvuke wa nyuzi joto kubwa una destroy protein in nature inakuwa destroyed by heat.
Bingwa wa Kemia amewataka Watanzania kuendelea kufuata maelekezo ya kitaalamu ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona ila pia na kutumia tiba mbalimbali za asili na tiba mbadala kupambana na Corona kwa kunywa tangawizi, vitunguu swaumu, au hata kujifukiza, vitu ambavyo Watanzania walipaswa kufundishwa na madaktari Bingwa wa tiba, badala yake sasa ni Bingwa wa Kemia ndio amekuwa mkombozi wa taifa letu katika vita hii dhidi ya Corona.
Ushauri huu wa Bingwa wa Kemia ndio ukombozi wa Taifa letu dhidi ya janga la Corona, kwasababu naamini kuna wengi wameugua Corona na wakajitibia kwa njia za asili na tiba mbadala na wakapona, hivyo kama kila Mtanzania akiona tuu dalili kwa mbali akaanza na huduma ya kwanza ya homeopathy treatment kwa kutumia natural remedies na treatments na alternative medicine tunaweza kuliokoa taifa letu zaidi kuliko kuwategemea hawa madaktari Bingwa wetu wa tiba za kisasa mahospitalini ambao ni mabubu huku mabingwa wa Kemia ndio akilisaidia taifa!.
Mpaka hapa nilipofikia, je bado kuna haja ya mimi kumtaja huyu bingwa wa Kemia?. Kwa vile huu ni mwaka wa uchaguzi, na tayari tuna mabingwa miongoni mwetu, nashauri wakati muafaka ukifiki wa kufanya maamuzi, usijiulize, twende na timu gani zaidi ya kwenda na timu ya mabingwa!,
Asanteni
Paskali
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU YATOKANAYO NA RIPOTI YA KAMATI MAALUMU YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA KUFANYA TATHMINI YA UGONJWA WA COVID-19 NCHINI
DAR ES SALAAM 17 MEI, 2021
Ndugu wanahabari, mtakumbuka kwamba kupitia hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyoitoa tarehe 6 Aprili, 2021 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu kuunda Kamati ya kitaalamu ya kufanya tathimini ya ugonjwa wa COVID-19 na baadaye msisitizo alioutoa tarehe 22 Aprili, 2021 wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, naomba kuwajulisha kuwa Kamati hiyo imewasilisha rasmi ripoti yake kwa Mheshimiwa Rais leo tarehe 17 Mei, 2021.
Ndugu Wanahabari, Kamati ilifanyia kazi hadidu za rejea 12 zilizohusu maeneo mbalimbali ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa pamoja na afua za udhibiti wa COVID-19 ikiwemo chanjo hapa nchini, kikanda na kimataifa.
Ndugu Wanahabari, Tangu kuingia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini mwezi Machi 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika mataifa mengine duniani na kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini.
Ndugu Wanahabari, Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza yafuatayo:
1. Serikali ihuishe mipango ya dharura (Contigency and Response Plans) katika ngazi zote kwa ajili ya kukabiliana na majanga likiwemo janga la ugonjwa wa COVID-19.
2. Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga (interventions) katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.
3. Wataalamu wa afya watimize wajibu wao kitaalamu, kwa kuzingatia weledi, miiko na maadili katika kuelimisha, kukinga na kutibu ugonjwa wa COVID-19 nchini.
4. Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya kikanda na kimataifa iliyoridhia katika jumuiya za EAC, SADC, AU na WHO.
5. Kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19:
a. Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi;
b. Pamoja na mapendekezo haya, Kamati Huru ya Kitaifa ya Ushauri wa Chanjo (NITAG) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo;
c. Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 nchini kwa kuanzia kiwe katika makundi yafuatayo kwa umuhimu:
i. Wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma (frontline workers) mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji;
ii. Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50;
iii. Watu wazima wenye maradhi sugu mengine (comorbidities) mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo n.k.;
iv. Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; na
v. Wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.
d. Kufanya uhamasishaji na maandalizi ya upokeaji, utunzaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo na wananchi wawe huru kuamua kuchanja au la.
e. Serikali iratibu upatikanaji wa chanjo kwa watumishi wa taasisi za kimataifa walioko nchini.
6. Serikali ya Tanzania ijiunge na COVAX Facility kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa chanjo, kwa kutumia fursa inayotolewa na GAVI.
7. Serikali itumie fursa zilizopo wakati huu wa janga la COVID-19 kuanza mchakato wa uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza chanjo.
8. Serikali iimarishe huduma za uchunguzi kwa kuijengea uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na maabara nyingine nchini ili kupanua wigo wa upimaji wa ugonjwa wa COVID-19.
9. Serikali ijenge uwezo wa ndani wa utambuzi wa virusi anuai vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.
10. Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa COVID-19 kwa umma na Shirika la Afya Duniani ili wananchi wapate taarifa sahihi toka Mamlaka za Serikali na kuheshimu makubaliano na kanuni ambazo nchi iliridhia.
11. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikamilishe mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa wa COVID-19.
12. Serikali iendelee kuhakikisha kuwa matumizi ya tiba asili na tiba mbadala katika mfumo rasmi wa tiba za kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi.
13. Serikali iendelee kutoa fursa na kuwawezesha wanasayansi kufanya tafiti kwa kufuata miiko, maadili na taratibu zilizowekwa ili kuimarisha kinga, tiba, uchunguzi wa ugonjwa wa COVID-19 na athari zake katika jamii nchini.
14. Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa COVID-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia (lockdown) na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi.
15. Wizara yenye dhamana ya fedha na uchumi ifanye tathmini ya kina ya athari za janga la COVID-19 na kuweka mpango madhubuti wa haraka wa sasa, wa muda wa kati na wa muda mrefu unaotekelezeka ili kukuza uchumi wa nchi.
16. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ziendelee kushirikiana ipasavyo katika hatua zote za kukabiliana na janga la COVID-19 pamoja na majanga mengineyo ikiwemo utoaji wa nyaraka za kimataifa kama vile Travel Advisory Note.
17. Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu iendelee kutekeleza ipasavyo jukumu la uratibu na kutoa rasilimali husika wakati wa majanga ya kitaifa na kimataifa kama ugonjwa wa COVID-19 kwa kushirikisha ngazi na sekta zote.
18. Serikali ikamilishe malipo ya madeni ya watoa huduma na watumishi waliokuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ili kuongeza ari na tija ya udhibiti wa ugonjwa huo.
19. Serikali iendelee kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa COVID-19.
Ndugu Wanahabari,
Asanteni kwa kunisikiliza.
Hii ni C&P
Thanks for this!. Alale pema peponi!, sisi tulio duniani, lazima tuendelee kuishi, kama ili kuishi ni pamoja na kupindua misimamo ya kijima ya mtangulizi, then ni bingiribingira mpaka Makka!. Kuna mambo kwenye mapendekezo hayo akina sisi tulishauri, na sasa ndio yameshauriwa na wataalamu, tuachage siasa kwenye proffesionalism, tupige siasa kwenye siasa, tuache wataalam kwenye issues za kitaalamu.
Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best!
P