Shule ya Msingi Juma kisiwani iko kijiji cha Juma, Kata ya Katunguru, Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza ilianzishwa 1974. Shule hiyo licha ya kuwa na uhaba wa walimu pia haijawahi kuwa na mwalimu hata mmoja wa kike kwa zaidi ya miaka 40 sasa. Wadau wa Jf hivi shule inapokosa mwalimu wa kike kisaikolojia ya wanafunzi wa kike si wanaweza kuathirika? Hakuna Matroni pale shuleni maana yake ushauri kwa mabinti unatolewa na patrons. Wadau wa elimu wilaya ya Sengerema chukueni hatua kuondoa hili tatizo. Kuna siku mwandishi wa habari Jumanne Mabawa wa RFA aliwahi kulitolea taarifa hili japo hadi sasa halija tatuliwa. Mimi nimezaliwa hapo kijijini hivyo suala hili halihitaji source of information tena. Cha msingi tufuatilie kwanini haina?