GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
1. Si kubwa kama jiji la Dar Es Salaam, lakini ningeambiwa nichague pa kuishi, ningepapendelea Kampala kutokana na hali yake ya hewa nzuri
2. Lugha ya Kiganda ndiyo imetawala kuanzia kwenye maredio na mitaani. Kizungu hutumika kinapohitajika
3. Kuna maeneo kuna Waswahili pia. Kuna mahali nimepita leo kwenye gesti moja nikakuta watu wanaongea Kiswahili. Nikipata muda nitaenda kuwauliza kama ni Watz au la. Kwenye ubao wa matangazo wa hiyo gesti, matangazo yamewekwa kwa lugha ya Kingereza na Kiswahili
4. Kuna mitaa pikipiki ni nyingi sana. Uliiona zikipita barabarani unaweza kufukiri zipo kwenye maadamano ya "chama"
6. Huenda boda boda wa huku nao wapo rafu katika uendeshaji pikipiki kama wa Bongo. Nimeshuhudia zikipuuzia kuzingatia taa za kuongozea magari. Ni tofauti na boda boda wa Kigali ambao inasemekana ni watiifu sana wa Sheria za barabarani
7. Inawezekana ndilo jiji la Afrika Mashariki linaloongoza kwa mabinti kuvaa vimini. Unakuta mwingine kimini chake ni kifupi sana kiasi kwamba akitaka kupanda boda boda inamlazimu awe na koti la kufunikia mapaja ili kujisitiri. Sijui ni utamaduni wao au ni "Uzungu" umewakolea?
8. Watu ni wachapa kazi. Ni kawaida kukuta maduka yaliyo pembezoni mwa mji yameshafunguliwa saa kumi na mbili Asubuhi, na muda huo mama lishe naye ameshaivisha chakula
9. Utamaduni wao kwenye matumizi ya Vyuo unaweza kuendana na Wakenya, ingawa Wakenya wanaweza wakawa "more advanced". Katika gesti kadhaa nilizolala, hakuna kopo la chooni wala toilet paper. Uzoefu wangu kwenye gesti za Kenya ni kwamba vyoo, hata vile vya umma(vya kulipa), lazima viwe na toilet paper. Lakini kwa Waganda sikuziona toilet paper wala kopo. Nazungumzia gesti za gharama nafuu na siyo mahoteli
10. Gesti za kawaida zinagharimu wastani wa Ugx 20,000 mpaka 30,000. Lakini ukienda nje ya mji, unaweza kupata mpaka Ugx 20,000 (self) na Ugx 13,000 (single)
11. Ndizi (matoke) ni chakula "common" huku
12. Wali wa huku ni kama pilau. Nimeshakula pilau zaidi ya mara moja, lakini mara zote nilipoagiza wali, nililetewa "pilau"
13. Kwa baadhi ya niliongea nao, hasa wale waliokwishafika Tanzania, wanaamini Serikali ya Tanzania inawajali raia wake kuliko ya Uganda😄. Mfano mojawapo waliotumia ni gharama za Internet. Wanadai internet ya Tanzania ni nafuu sana ukilinganisha na ya Uganda
14. Nimeshangazwa pia na chipsi mayai za huku. Chipsi kavu zilipashwa kivyake na mayai yakakaangwa kivyake. Sijui ndiyo kawaida ya huku au ni kwangu tu ndiyo waliamua kufanya hivyo!
NB. Ni "maajabu" kwangu tu ambaye bado "mgeni"