Maajabu ya jiji la Kampala

Mashuleni wanavaaje? Perhaps wanazoea toka huko ni kama utamaduni kama south Africa vile

Imagine watoto wa Tz wanavovaa masketi marefu mashuleni, hata akikua ni ngumu kuanza vaa vimini
 
Tembelea maeneo ya Kitintale,Rugezi mpaka Port Bell wabongo wapo wengi. Miaka ya nyuma kuna club inaitwa Wheel House karibu na Bandari ya Port Bell ilikuwa zaidi ya Sodoma na Gomora, Wafanyakazi wa Marine Service enzi hizo waliweka heshima Bar mpaka leo ukienda ukasema Mtanzania unapewa kipaumbele.
 
Sente meke- Bei gani, Usule Bulunji-Usiku mwema, mtwalo- elfu 10, lusamvu-elfu 7, nyoo -sana
Kumbe ndicho alichokuwa anamaanisha 😄😄😄

Nilimwuliza mtu anielekeze zilipo gesti, akaniambia zipo za mtaro 2, nikajua anamaanisha self contained, kumbe ni elfu ishirini za Kiganda? "Ujinga" unatesa!

Kwa hiyo ishirini na tano ni mtwalo mbili na nusu?

Halafu mimi nilifikiri inatamkwa MTARO, kumbe ni MTWALO?🤣
 
Ndio saizi huwezi kupigwa, elfu 1 nadhani wanaita Lukumi. Polepole ni mpola mpola, hao boda usiku wengi wanakuwa maji unakuta anakuita sebo(mwanaume) tugende(twende). Wewe unamuita Janguu(njoo) sebo
 
Nilishasikia sana neno Port Bell likitamkwa, nikafikiri ni mji kwenye nchi fulani mbali na Afrika Mashariki, kumbe mji wa "hapa hapa" kwenye Nzengo?
 
Nilishasikia sana neno Port Bell likitamkwa, nikafikiri ni mji kwenye nchi fulani mbali na Afrika Mashariki, kumbe mji wa "hapa hapa" kwenye Nzengo?
Ni mji karibu na Ziwa Victoria kuna bandari kubwa inaitwa Port Bell, meli za kutoka Tanzania(Mwanza,Bukoba,Mara),Kenya( Kisumu) zinashusha mizigo na abiria hapo.

Sio mbali na Kampala, ukiwa na nafasi weekend ukatembee kuna waganda wanafanya booking boat za kuwatembeza ziwani na hapo ndio utakutana na wafanyabiashara kutoka Mwanza na Bukoba wakileta bidhaa na kutoa mizigo huko kuja Tanzania
 
Uganda wanajua kula nyama ng'ombe ambayo kwa sehemu kubwa hukaushwa kwanza kwa kubanikwa ndipo inapikwa.

Pia wanachakula chao kinaitwa Luwombo ambacho kinapikwa kikiwa ndani ya majani ya mgomba mfano Luwombo ya nyama ya ng'ombe ni tamu sana.

Hata hivyo, maajabu yapo nchi kama vile Poland ambako mgahawani unakuta chakula cha nyama mbichi, saladi ya mbogamboga ilichochanganywa na vipande vipande vya samaki wabichi au Singapore kwenye supu ya konokono. Nchi zinatofautiana tamaduni inakuwa ni maajabu pale unapokutana na tamaduni ngeni katika mawanda tofautitofauti.
 
Asa
Ubarikiwe sana Mkuu
Nimejifunza vitu vingi kupitia uzi huu!

Nauli ya basi kutokea Dar ni Bei gani? Na hupitia mikoa Gani hadi kufika huko?
 
1. Uwombo ni "matokeo" (ndizi)?
2. Majani ya migomba nimeona yanatumika kufunikia hata ugali ili usipoe
3. Hao wanaokula nyama mabichi wamezidi😀 Najua hata Tanzania kuna jamii zinazokula nyama mabichi, lakini sikutarajia na jamii "zilizoendelea" kama Wapoland" nao wawe na utamaduni kama huo.
 
Asa

Ubarikiwe sana Mkuu
Nimejifunza vitu vingi kupitia uzi huu!

Nauli ya basi kutokea Dar ni Bei gani? Na hupitia mikoa Gani hadi kufika huko?
Sijui nauli ya kutokea Dar. Kama unataka "kuja" Kampala, panda basi hadi Mwanza ukashangae kwanza miamba ya jijini Mwanza ndipo uendelee na safari ya Kampala.

Na kama utaanzia safari Mwanza kwa magari ya kuunga unga kama nilivyofanya, utapanda gari kutoka Mwanza hadi Katoro (Geita) Tsh 8,000/=.

Katoro hadi Bukoba Tsh 20,000/=

Kutoka Bukoba Mjini utachkua daladala hadi Mutukula Tsh 4,000/=.

Mutukula ukishagongewa mihuri, unaweza ukavuka mpaka kwa miguu kuingia upande wa Uganda kwenda ziliko hiace (Waganda huziita taxi), au uchukue bodaboda Tsh 1,000/= au Tsh 2,000/=, lakini wakikuona wewe ni wa kuja, bodaboda wanaweza wakakuambia hata Tsh 5,000/=.

Kabla ya kuvuka kwenda upande wa Uganda, ni vizuri ukabadilisha hela upate za Kiganda, na pia ukasajili line ya Uganda, mfano MTN (Vodacom). Kama una passport kubwa (siyo EMERGENCY TRAVEL DOCUMENT) unaweza ukasajili line yako kwa jina lako hapo hapo Mutukula upande wa Tanzania, gharama ni Tsh 3,000/=, lakini kama unatumia EMERGENCY TRAVEL DOCUMENT, watakupatia line iliyokwishasajiliwa kwa jina la mtu mwingine kwa Tsh 10,000/=, ila wakikuona wewe ni mtoaji mzuri watakuambia Tsh 15,000/=.

Ukishaingia upande wa Uganda, utapanda "taxi" kwa hela ya Kiganda Ugx 40,000 Mutukula hadi Kampala. Ingawa nauli ni Ugx 40,000/= , mimi nililipa Ugx 35,000/=, na mtu mwingine alilipa Ugx 30,000/=. Wakati wa kurudi nitabargain hadi na mimi nipande kwa Ugx 30,000/=.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…