Maajabu ya jiji la Kampala

Maajabu ya jiji la Kampala

Watu mna mauzoefu na majiji ya watu mapema basi😄

Hivi hayo mavyakula yao tukiyafanyia "marketing" Bongo hayatakubalika?
Hapana wabongo sio wapenzi wa aina ya vyakula vya uganda, wabongo wanapenda vitu vilivyokaangwa mno, lakini mimi niko tofauti baadhi ya vyakula naipenda hasa vile natural wanachemsha, vingine wanapika wanaunga Karanga hawatumii mafuta ndio maana wanamilili cheki kinamama masokoni wanavyobeba mizigo mizito ambayo huku anabeba kuli
 
Kesho asubuhi pita tu road side upate kiazi kikubwa kabisa kama boflo cha kuchemsha na uji wa soya kikombe nusu lita, utazurura siku nzima utakula jion nakwambia vyamoto kimefunikwa na majani tu ya mgomba
 
Kwa jinsi nionavyo,
1. Dar kumeendelea zaidi ya Kampala, ingawa Kampala kumepangika vizuri zaidi. Labda kwa vile sijatembelea maeneo yote, ila mpaka sasa sijayaona mazingira ya "Uswahilini". Nafikiri naeleweka nikisema "Uswahilini"
2. Watu wa huku ni wachapa kazi. Wapo busy sana.
3. Sijui kama kuna watoto wa "mitaani", sijakutana nao huku. Labda sijafika mitaa wanapopendelea
4. Ni waelewa. Ukimwuliza mtu kitu, kama anafahamu, atakuelekeza vizuri
Watoto wa mitaani wapo sana Kampala , mimi niliwashuhudia Kabalagala
 
Umenikumbusha mbali MNO!!
Kuna bar mojo ilikua mjini kati ikiitwa SEX PUB palikua ni fire 🔥. Kampala murunjinyo ssebo!!
Nitarudi.
KAZI ni kipimo cha UTU
Kuna wadada walikuwa wanacheza uchi, dah nilikulaga ada kwasababu ya starehe za KLA
 
Hapana wabongo sio wapenzi wa aina ya vyakula vya uganda, wabongo wanapenda vitu vilivyokaangwa mno, lakini mimi niko tofauti baadhi ya vyakula naipenda hasa vile natural wanachemsha, vingine wanapika wanaunga Karanga hawatumii mafuta ndio maana wanamilili cheki kinamama masokoni wanavyobeba mizigo mizito ambayo huku anabeba kuli
Waganda wana miili aisee! Kuna chakula fulani sijui kinaitwaje vile, mboga ni karanga zilizosagwa na kugeuzwa kuwa mchuzi!
 
Kesho asubuhi pita tu road side upate kiazi kikubwa kabisa kama boflo cha kuchemsha na uji wa soya kikombe nusu lita, utazurura siku nzima utakula jion nakwambia vyamoto kimefunikwa na majani tu ya mgomba
🙏🙏🙏
 
Hivi ushamba ndiyo ukoje lakini? Kama ni mtu aliyetoka shamba, basi mimi siwezi kuachana nao kwa sababu nikifika tu Tz, nitaenda kutumia siku kadhaa shambani kwangu kabla ya kuelekea "Mjini". Lakini kama ni "mshangao", sidhani kama utaniisha kwa sababu karibia kila ninakoenda, iwe Tz au kwingineko, sikosi vya kushangaa:
1. Nilipofika Mbeya kwa mara ya kwanza, nilishangazwa na ukijani mzuri wa huo mji. Nilipoenda Chunya, nilibaki mdomo wazi jinsi barabara ilivyochongwa huko milimani
2. Njombe nilishangazwa na tabia ya watu wa huko ya uchapa kazi, ukarimu, ujasiri, na ulaji kitimoto. Japo hata Mimi huwa ninakula mara chache, utofauti wangu na watu wa Njombe ni kuwa mimi huwa "naonja" ila wao "wanakula"

3. Zanzibar niliduwaa kukuta kuna baa na kitoweo cha kitimoto

4. Nairobi niligundua huko hakuna makopo vyooni badala yake kuna toilet papers

5. Kigoma nikashangazwa kugundua kuwa vijana wa huko wasio na kazi hawapendi vibarua vya kulima, badala yake, vibarua wanaotegemewa ni Warundi, mpaka wenyeji wa huko wanawakejeli kwa kuwaita matrekta

6. Maeneo ya Kasanda wilayani Kakonko mkoani Kigoma niliikuta ardhi nzuri sana kama ya Njombe. Sikutegemea kukuta ardhi nzuri kama hiyo maeneo hayo

7. Mwaka huu, kwa Neema ya Mungu, nitafika Dubai na Cape Town! Utashangaa nikikuambia nimeshaanza kuyashangaa hayo majiji hata kabla sijafika?

Naamini hata ukinikaribisha kwako, sitakosa cha kushangaa. Na hii ni kwa sababu ninapenda "kujifunza"
I love it, nipo mkoa wa 16 sasa, 2026 nitaanza East Africa countries
 
I love it, nipo mkoa wa 16 sasa, 2026 nitaanza East Africa countries
Kama kuna tuzo zinazotolewa kwa waliofika mikoani nchini Tanzania huenda na mimi ningepata chochote, japo siyo rahisi pia. Nimebakiza mikoani miwili tu: Lindi na Mtwara ili nimalize mikoani yote ya Tanganyika! Kwa Zanzibar nimeishia Unguja. Bado sijafika Pemba!
 
1. Uwombo ni "matokeo" (ndizi)?
2. Majani ya migomba nimeona yanatumika kufunikia hata ugali ili usipoe
3. Hao wanaokula nyama mabichi wamezidi😀 Najua hata Tanzania kuna jamii zinazokula nyama mabichi, lakini sikutarajia na jamii "zilizoendelea" kama Wapoland" nao wawe na utamaduni kama huo

NI KWAMBA KUNA MTOTO WA WAZIRI ALITUALIKA KULA CHAKULA CHA JIONI KATIKA MOJA YA MGAHAWA WA WARSAW (MJI MKUU WA POLAND) AKATUWEKEA ODA HIYO IKIWA NI MENU YA HESHIMA ILIKUWA SAVED NA MAJANI NADHANI NI SPINACHI PAMOJA NA KIPANDE CHA MKATE. MIMI NILIKULA MAJANI NA MKATE TU. HIYO NYAMA SIKUDHUBUTU KUILA KWA SABABU HAIKUWA UTAMADUNI WANGU
 
Hongera pia kwa kiua "majani" kama ng'ombe!😄

Ila kama ningekuwa wewe, inawezekana ningejaribisha hata kakipande kadogo ka nyama mbichi nione ladha yake🤣
 
Hivi Kampala kuna mitaa ya slums kama ilivyo kwa Nairobi?
Ipo lakini si kama Nairobi ni kama dar nyumba sio za mabati ni tofali nzuri za block, shida ni tope lile jekundu linanasa kwakua mvua ni muda wote mwaka mzima
 
1. Si kubwa kama jiji la Dar Es Salaam, lakini ningeambiwa nichague pa kuishi, ningepapendelea Kampala kutokana na hali yake ya hewa nzuri

2. Lugha ya Kiganda ndiyo imetawala kuanzia kwenye maredio na mitaani. Kizungu hutumika kinapohitajika

3. Kuna maeneo kuna Waswahili pia. Kuna mahali nimepita leo kwenye gesti moja nikakuta watu wanaongea Kiswahili. Nikipata muda nitaenda kuwauliza kama ni Watz au la. Kwenye ubao wa matangazo wa hiyo gesti, matangazo yamewekwa kwa lugha ya Kingereza na Kiswahili

4. Kuna mitaa pikipiki ni nyingi sana. Uliiona zikipita barabarani unaweza kufukiri zipo kwenye maadamano ya "chama"

6. Huenda boda boda wa huku nao wapo rafu katika uendeshaji pikipiki kama wa Bongo. Nimeshuhudia zikipuuzia kuzingatia taa za kuongozea magari. Ni tofauti na boda boda wa Kigali ambao inasemekana ni watiifu sana wa Sheria za barabarani

7. Inawezekana ndilo jiji la Afrika Mashariki linaloongoza kwa mabinti kuvaa vimini. Unakuta mwingine kimini chake ni kifupi sana kiasi kwamba akitaka kupanda boda boda inamlazimu awe na koti la kufunikia mapaja ili kujisitiri. Sijui ni utamaduni wao au ni "Uzungu" umewakolea?

8. Watu ni wachapa kazi. Ni kawaida kukuta maduka yaliyo pembezoni mwa mji yameshafunguliwa saa kumi na mbili Asubuhi, na muda huo mama lishe naye ameshaivisha chakula

9. Utamaduni wao kwenye matumizi ya Vyuo unaweza kuendana na Wakenya, ingawa Wakenya wanaweza wakawa "more advanced". Katika gesti kadhaa nilizolala, hakuna kopo la chooni wala toilet paper. Uzoefu wangu kwenye gesti za Kenya ni kwamba vyoo, hata vile vya umma(vya kulipa), lazima viwe na toilet paper. Lakini kwa Waganda sikuziona toilet paper wala kopo. Nazungumzia gesti za gharama nafuu na siyo mahoteli

10. Gesti za kawaida zinagharimu wastani wa Ugx 20,000 mpaka 30,000. Lakini ukienda nje ya mji, unaweza kupata mpaka Ugx 20,000 (self) na Ugx 13,000 (single)

11. Ndizi (matoke) ni chakula "common" huku

12. Wali wa huku ni kama pilau. Nimeshakula pilau zaidi ya mara moja, lakini mara zote nilipoagiza wali, nililetewa "pilau"

13. Kwa baadhi ya niliongea nao, hasa wale waliokwishafika Tanzania, wanaamini Serikali ya Tanzania inawajali raia wake kuliko ya Uganda😄. Mfano mojawapo waliotumia ni gharama za Internet. Wanadai internet ya Tanzania ni nafuu sana ukilinganisha na ya Uganda

14. Nimeshangazwa pia na chipsi mayai za huku. Chipsi kavu zilipashwa kivyake na mayai yakakaangwa kivyake. Sijui ndiyo kawaida ya huku au ni kwangu tu ndiyo waliamua kufanya hivyo!

NB. Ni "maajabu" kwangu tu ambaye bado "mgeni"
15 --wapika chips mitaani 90% ni wanawake.
 
Hivi ushamba ndiyo ukoje lakini? Kama ni mtu aliyetoka shamba, basi mimi siwezi kuachana nao kwa sababu nikifika tu Tz, nitaenda kutumia siku kadhaa shambani kwangu kabla ya kuelekea "Mjini". Lakini kama ni "mshangao", sidhani kama utaniisha kwa sababu karibia kila ninakoenda, iwe Tz au kwingineko, sikosi vya kushangaa:
1. Nilipofika Mbeya kwa mara ya kwanza, nilishangazwa na ukijani mzuri wa huo mji. Nilipoenda Chunya, nilibaki mdomo wazi jinsi barabara ilivyochongwa huko milimani
2. Njombe nilishangazwa na tabia ya watu wa huko ya uchapa kazi, ukarimu, ujasiri, na ulaji kitimoto. Japo hata Mimi huwa ninakula mara chache, utofauti wangu na watu wa Njombe ni kuwa mimi huwa "naonja" ila wao "wanakula"

3. Zanzibar niliduwaa kukuta kuna baa na kitoweo cha kitimoto

4. Nairobi niligundua huko hakuna makopo vyooni badala yake kuna toilet papers

5. Kigoma nikashangazwa kugundua kuwa vijana wa huko wasio na kazi hawapendi vibarua vya kulima, badala yake, vibarua wanaotegemewa ni Warundi, mpaka wenyeji wa huko wanawakejeli kwa kuwaita matrekta

6. Maeneo ya Kasanda wilayani Kakonko mkoani Kigoma niliikuta ardhi nzuri sana kama ya Njombe. Sikutegemea kukuta ardhi nzuri kama hiyo maeneo hayo

7. Mwaka huu, kwa Neema ya Mungu, nitafika Dubai na Cape Town! Utashangaa nikikuambia nimeshaanza kuyashangaa hayo majiji hata kabla sijafika?

Naamini hata ukinikaribisha kwako, sitakosa cha kushangaa. Na hii ni kwa sababu ninapenda "kujifunza"

Mbeya Mbeya Mbeya sio kwa ubaya...
Ila pale ni dust city.
Huo ukijan hua mnauonea wap na mimi niende.
 
Back
Top Bottom