Maajabu ya lugha ya kingereza (sehemu ya pili). Kwanini wazungu hatuwaelewi?

Maajabu ya lugha ya kingereza (sehemu ya pili). Kwanini wazungu hatuwaelewi?

Meneja CoLtd

Senior Member
Joined
Mar 6, 2021
Posts
122
Reaction score
143
Baada ya kuisoma asili ya lugha ya kingereza katika makala ya kwanza leo tutatoa jawabu la swali ambalo wapenzi wengi wa lugha ya kingereza wamekua wakijiuliza,

KWANINI WAZUNGU HATUWAELEWI WAKIONGEA BAADHI YA MANENO KWA KINGEREZA?

Jawabu la swali hili ni rahisi tu, kwanza unatakiwa uwe na kamusi kubwa "OXFORD au LONGMAN" napia inabidi uwe unazifahamu vizuri Alfabeti za lugha ya kingereza ambazo zimeazimwa kutoka katika lugha ya kiratini ili uweze kusoma vineno vidogo vinavyofundisha utamkaji katika kamusi hiyo,
IMG-20240523-WA0000.jpg

Picha inaonesha utamshi sahihi wa neno YOUR ( 1 utamshi wa kizungu, 2 utamshi wa kimarekani)

Neno hili "YOUR" wengi wanakosea kilitamka.
Na Utamkaji sahihi ni "YO"
Mfano:
This is your car = dhis iz yo kaa.

Huo ni mfano mdogo tu nautaona ni kwanini wazungu hatuwaelewi kwasababu wao wanafamka maneno kwa usahihi.

Somo lijalo tutaona ni jinsi gani ya kusoma vokali na herufi za kingereze ambazo hutumika kufundisha jinsi ya kusoma kwenye kamusi.
 
Kiingereza kama lugha zingine, kina lafudhi nyingi, rejesta na lakabu.

Huwezi kukijua kiingereza kupitia kamusi, kile ndo fasihi lakini sicho kinachoongelewa mitaani

Mimi naona njia nzuri ya kujua kiingereza ni kuangalia media za kizungu kama filamu na miziki, lugha ya humo ndo lugha wanayoitumia mitaani
 
Juzi kati kiingereza cha kimarekani kimemtoa jasho Ruto hakuelewa kitu, tena alikuwa anaongea na mkenya mwenzake anayeishi marekani. Kumbe wakenya hawajui kuongea american english!
 
Kingereza rasmi lazima ujifunzie sehemu rasmi ikishajua ndo uende kujifunza kingereza cha huko mitaani, ushauri wangu lakini
 
Juzi kati kiingereza cha kimarekani kimemtoa jasho Ruto hakuelewa kitu, tena alikuwa anaongea na mkenya mwenzake anayeishi marekani. Kumbe wakenya hawajui kuongea american english!
Hh mtu anayeishi marekani anaweza kukukomesha akakuchanganyia na kimarekani cha uswahilini na maneno ya msimu yaloyozuka huko. Mfano Mtanzania akikwambia demu, mpaka usemeee. Kama wewe kiswahili chako cha darasani huwezi kutoboa
 
ndio kilichotokea kwa Ruto, alichanganyiwa neno kidogo tu akapotea.
 
Back
Top Bottom