Maajabu ya madikteta wa Turkmenistan

Maajabu ya madikteta wa Turkmenistan

Saparmurat Niyazov​


Kuanzia mwaka 1985-2005 Turkmenistan ilikuwa chini ya dikteta Saparmurat Niyazov. Alifanya maajabu haya.

- Alijenga sanamu yake kubwa sana. Sanamu hiyo ilikuwa inazunguka ili muda wote iwe inatazama jua

- Aliandika kitabu, kitabu hicho kiliingizwa kwenye mitaala ya shule, kwenye usaili wa kazi na hata kwenye mafunzo ya udereva

- Alibadilisha majina yashule, miji nk, na kuvipa majina yake na ya familia yake.

- Alibadili majina ya miezi na siku kuwa yake, familia yake, kitabu chake nk.

- Alifunga hospital zote nje ya mjii mkuu, kwamba mtu akiumwa aende mji mkuu

- Alifunga maktaba zote, akisema vitabu vya kusoma ni Quran na alichoandika

- Alijiingiza kwenye wimbo wa taifa

- Piga marufuku mbwa kwenye mji mkuu

- Alikataza ndevu na nywele ndefu kwa wanaume

- Alikataza watangazaji kupaka make up

- Neno mkate akalitoa na kuweka jina la mama yake

Alikufa mwaka 2006 kwa tatizo la moyo. Hapo akaingia kituko mwingine.

Gurbanguly Berdimuhamedow​


Huyu alikuwa Rais toka 2006 hadi 2022 alipomuachia urais kijana wake. Ni daktari wa meno kwa taaluma. Alibadilisha upuuzi mwingi wa mtanngulizi wake, lakini nae akaongeza wake.

-Huyu anapenda sana farasi. Ametengeneza sanamu lake kubwa sana akiwa amepanda farasi. Lipo mji mkuu.
-Aliamuru video inayomuonyesha akianguka na farasi isitolewe.
-Alipiga marufuku magari yasiyo na rangi nyeupe kukanyagamji mkuu.
-Aliamuru majengo yote ya mji mkuu kuwekwa cladding ya vigae vyeupe.
-Ni mwanamuziki wa hiphop
-Vitu vingi amevipa majina ya baba na babu yake.

Ashgabat, mji mkuu wa Turkmenistan

View attachment 2192912
hawakuwahi kushiriki katika kudhurumu haki ya kuishi ya raia wao kama wafanyavyo maditketa wa nchi za afrika?.
 
Mji mkuu wao mzuri

Madikteta wanaletaga maendeleo sanaa
ie Hitler,Mao,Putin Gadaffi nk
 
Back
Top Bottom