Kinaeleweka
Senior Member
- Nov 10, 2014
- 153
- 121
Poleni na majukumu mbalimbali ndugu zangu,
Bila kuwapotezea muda,napenda kutoa ushuhuda juu ya umuhimu wa maji ya kunywa kama tiba katika kutibu tatizo la Vidonda vya tumbo na Bawasiri.
Tatizo la vidonda vya tumbo,kwangu lilikuwa ni la zaidi ya miaka mitano ,licha ya kujitahidi kutumia dawa mbalimbali za hospital lakini pia za asili za mimea nilizokuwa nikishauriwa na watu mbalimbali.Tatizo serious la vidonda vya tumbo lilikuwa halitokei mara kwa mara(labda mara moja kwa miezi 2) lakini lazima linipeleke hospital hata iwe usiku wa manane, nako nikifika naishia kuchomwa sindano ya kutuliza maumivu na dawa ambazo nadhani hazikuwa na msaada wowote.
Pia,niliwahi kupata changamoto ya Bawasiri na nikawa napata shida sana licha ya kushauriwa kutumia dawa za hospital na asili ili kutibu lakini sikufanikiwa kumaliza tatizo.
Tokea nimeanza kunywa maji kila siku glasi 2-3 matatizo tajwa hapo juu sijawahi kuyapata tena kwa kipindi cha miaka 2 iliyopita sasa.Licha ya kuendelea na ratiba yangu ya kutokula mchana mara kwa mara. Na pia naamini natibu magonjwa mbalimbali maana kiafya nimezidi kuwa imara.
Baada ya kugundua hilo, nimekuwa nikiwashauri watu mbalimbali kuhusu umuhimu wa kunywa maji
katika kutibu hayo magonjwa na nawahurumia sana watu wanaopoteza fedha nyingi kutafuta tiba mbalimbali za hayo magonjwa na hali hayo magonjwa yanatibika kwa maji tu.
Ndugu zangu,tujenge mazoea ya kunywa maji mara kwa mara hakika ni tiba kubwa sana kwa maradhi mbalimbali.