Maajabu ya Mimba

Maajabu ya Mimba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
MAAJABU YA MIMBA HONGERA KWA KUPATA MIMBA PART -1




Hongera

Kwa Kupata Mimba!

Ujauzito ni mojawapo ya nyakati za ajabu na kufurahisha
sana, kumkamilisha mwanamke katika maisha yake. Unapokuwa
na kiumbe kidogo kunapoanza kutengenezwa ndani ya mwili wako
utaanza kupata mabadiliko mengi kimaumbile na kihisia. Unaweza

kujiandaa vema katika kuikabili hali hii ya kuvutia ukitambua kuwa
kipo kiumbe kinachokua ndani ya tumbo lako na jinsi unavyoweza
kukitunza. Ukijitunza vema kwa kufuata mwongozo wa lishe bora
wakati wa ujauzito, unaweza kumpa mtoto nafasi nzuri ya kuwa na
afya nzuri.

Kijitabu hiki kitakusaidia kufahamu mlolongo wa utatanishi
unaoendelea ndani ya mwili wako na kukuelezea utarajie nini
katika kila hatua wakati wa ujauzito. Utajifunza pia namna ya
kuchagua lishe iliyo bora na iletayo afya kwako na mtoto wako
mchanga kabla na baada ya kuzaliwa. Majedwali ya virutubisho
na vidokezo vyenye kukufaa vimetolewa katika kiambatisho ili
kukusaidia katika wakati huu muhimu sana.

Kijitabu hiki kimekusudiwa kuwa kama mwongozo na silaha
unayoweza kuitumia wakati wote wa ujauzito na ulezi. Lakini
kumbuka kwamba hakijakusudiwa au kuwa ukione cha maana
badala ya daktari. Daktari ni mtu muhimu sana katika matatizo
yako na kukupa ushauri.

Kuanza Kwa Maisha Mapya
Kila mwezi, vichocheo vya mwili wako vinafyatua mlolongo
wa matukio yanayosababisha kuruhusiwa kwa yai kutoka katika
ovari kiasi cha siku 14 kabla ya mzunguko wa hedhi yako. Yai

linaondoka kwenye ovari na kuanza safari yake mpaka kwenye mji
wa uzazi. Njiani linakutana na mbegu za baba zinazoingia wakati
wa kutana mwilini. Mojawapo ya mbegu inajiunga na yai, na

kuanzisha chembe mpya. Hii inagawa na kujiongezeka kwa upesi
wakati wa safari yake kufika tumbo la uzazi. Linapofika katika
tumbo la uzazi, na baada ya kuelea kwa siku tatu inajifungia na
tabaka ya tumbo la uzazi. Inachukua malisho yake kutoka kwa
mishipa ya damu ya mama inayopita, na inaanza kutengeneza
kondo. Ndani ya miezi mitatu kiinitete (embryo) huwa

kimeshakamilika ni kazi ya kukua tu inayobaki. Mimba ya
kawaida hukua katika kipindi cha siku 280, au majuma 40 (miezi
tisa ya kalenda) kuanzia siku ya kwanza kilipomalizikia kipindi cha
siku za hedhi. Miezi tisa imegawanyika katika hatua, au vipindi
vitatu vya ukuaji.

Katika miezi mitatu ya mwanzo ya ukuaji wa mimba kiumbe
kilichoko tumboni huitwa kiinitete (embryo). Katika awamu ya
kwanza ni muhimu kuwa makini na viungo muhimu. Katika hatua
hizi za awali, ingawaji ni kweli kuwa yaweza kuwa hivyo hivyo

katika muda wote wa ujauzito, mtoto aweza kudhurika kutokana na
mazingira na maumbile inayokuathiri wewe pia. Ni vizuri kuepuka
kila inapowezekana, kujilinda na magonjwa ya milipuko, X-rays na
dawa. Kama unahitaji matibabu, mwambie Daktari kwamba una
mimba. Hata hivyo, ni muhimu kutibu homa mapema usiathiri
mtoto.

Katika miezi mitatu ya awamu ya pili, kiinitete kinakua zaidi
na hapa huitwa kwa kitaalamu fetus. Kuanzia mwezi wa sita,
mtoto aliyeko tumboni hukua haraka haraka zaidi kuliko nyakati
zilizotangulia, huhitaji chakula zaidi. Baadaye katika kijitabu hiki
utajifunza kwa nini lishe inahitajika kuboreshwa zaidi kwa mama na
mtoto katika kipindi hiki.

Wakati wa ujauzito, mwili wako hutengeneza viungo viwili
vya kushangaza ili kumbeba mtoto na kumlisha akiwa tumboni:
chupa (amniotic sac) na kondo la nyuma. Mtoto huishi na hukua
Mwongozo wa Kukupatia Viini Rishe - Unavyohitaji Mwilini
Mwongozo wa Vyakula Mwilini Faida Zake
Maziwa, siagi, mboga za kijani, spinachi
kabichi, mchicha, mhilile, kisanvu,
matembele, mlenda
Hutupatia
kalsiamu
Ini, nyama, kuku, mayai, mkate,
maharage na aina za mtama
Tunapata madini
ya chuma

Samaki, nyama ya ngombe, kuku, nyama
ya nguruwe, siagi, kumbikumbi, ndege,
nyama ya mbuzi, bata, kanga na kondoo
Tunajenga
mwili
Maziwa, samaki, maini, mboga za
majani
Tunapata

Vitamini A

Vyakula vya aina ya cha-chu, ngano,
mtama, ini
Tunapata

Vitamini B (B1hadi B12)

Machungwa, nyanya, ndizi, ubuyu,
Ukwata, ngwelu, ngukwe, mapapai,
malimau, ndimu, madansi, matango
Tunapata

Vitamini C
Jibini, maziwa ya mgando, mafuta ya
samaki, joto la jua
Tunapata

Vitamini D
Vyakula vya punje, mtama, mahindi,
karanga njugu mawe
Tunapata

Vitamini E
Nyama, ini, kuku, bata, maziwa, njugu
mawe mchele, mtama
Tunapata
vitamini ya
niacin

Mboga za majani, mchicha, kisanwu,
matembele, spinachi, kabichi, (mhilile)
majani ya maboga
Kuongeza
damu kusaidia
mifupa

Maumivu ya
Mgongo


Kaa mkao mzuri nyonga zikiwa zimekaa vema.
Unapokuwa umesimama mahali pamoja, kunja
magoti kiasi, badili uzito wako kutoka upande
mmoja kuelekea upande wa pili. Muone
daktari wako akushauri jinsi mnavyoweza

kufanya mazoezi madogo madogo kupunguza
maumivu ya mgongo.
Mkakamao
wa misuli ya
miguu

Nyanyua miguu. Wakati mwingine ongeza
kula vyakula vyenye kalisi na magadi ili
kuongeza nguvu ya mifupa. Kila mara
wasiliana na daktari wako.
Ngozi yenye
mafuta,
mabadiliko
ya ghafla
kwenye
ngozi, ngozi
kukauka.

Kunywa vinywaji vingi vya maji maji kwa ajili
ya ngozi inayo meremeta kwa mafuta; tumia
dawa ya kusababisha tishu laini kujikunyata na
kubana mishipa ya damu inayopendekezwa;

mwone daktari kama maumivu yakizidi. Kwa
ngozi iliyokauka: kunywa majimaji mengi na
utumie dawa iletayo unyevunyevu
iliyopendekezwa. Ili kupunguza mikunjo ya

ngozi, lainisha maeneo yote yaliyoathirika kwa
kupaka cocoa butter (siagi ya kokoa) au
mafuta ya vaseline kila siku.
Matamanio
ya chakula

Tosheka kwa kujipatia vitafunwa vilivyorutubishwa.

akiwa ndani ya chupa, akielea huku na huku katika maji maji yenye
chumvi chumvi. Maji maji haya huzuia ukuta wa nyumba ya uzazi
usimbane mtoto, hivyo anakuwa na nafasi ya kukua. Chupa pia
huzuia mitikisiko yoyote -- iwapo utapigwa tumbo, mtoto atakingwa
na maji maji yaliyomzunguka ndani ya chupa.

Kondo la nyuma husaidia mfumo wa uhai wa mtoto. Likiwa

limeunganishwa katika ukuta wa nyumba ya uzazi, kondo hutumika
kupitisha chakula cha mtoto pia kama njia ya kutolea uchafu.
Mbadilishano wa Oksijeni (hewa safi), viini lishe na ulinzi dhidi ya
maambukizi ya magonjwa hufanywa na chembe chembe
zinazolinda mwili ambazo hupitia katika mkusanyiko wa seli za
kondo la nyuma na kitovu. Kondo hili kweli ni la ajabu sana kwa

maana linafanya kazi kama mapafu ya mtoto, figo, utumbo na ini.
Matukio ya Mimba Kila Wiki:
Tunahesabu mimba kuanzia siku ya kwanza ya kuingia
mwezini kwa mara ya mwisho. Kwahiyo, mimba yenyewe inaanza
wiki ya tatu baada ya kuona siku zako.
Wiki Mendeleo ya Mtoto na Mama Wakati wa Ujauzito
Wiki yaTatu

Yai limeondoka kwenye ovary na kuanza safari yake
mpaka tumbo la uzazi. Njiani linakutana na mbegu za
baba zinazoingiza wakati wa kukutana mwilini.
Mojawapo ya mbegu inajiunga na yai, na kuanzisha
chembe mpya. Hii inagawa na kujiongezeka kwa haraka
wakati wa safari yake kufika tumbo la uzazi.
 

Attachments

MAAJABU YA MIMBA HONGERA KWA KUPATA MIMBA PARTI- 2



Wiki ya Nne






Wiki
ya
Nne


· Bado huwezi kujisikia tofauti kuliko kawaida.
· Yai lililochavushwa limefika katika tumbo la uzazi, na
baada ya kukaa kwa siku tatu linajifungia na tabaka la
tumbo la uzazi. Linachukua lishe yake kutoka kwenye
mishipa ya damu ya mama ambayo inapita pale, na
inaanza kutengeneza kondo.




Wiki
ya
Tano

· Umekosa siku za mwezi, lakini huna hakika bado. Matiti
yanaweza kuwa mepesi kuumia na kuongezeka vipimo
kidogo. Unaweza kutaka kukojoa mara nyingi kuliko
kawaida.
· Mimba imefika milimeta 2 - ungeweza kuona ungeweza
kuangalia ndani ya tumbo la uzazi. Kiumbe kina uti wa
mgongo wake na ubongo wake una sehemu mbili




Wiki Mendeleo ya Mtoto na Mama Wakati wa Ujauzito


Baadhi ya Adha Ambazo ni Kawaida kwa Wajawazito
Adha/Kero Namna ya Kuondoa
Kuchefukwa
roho
asubuhi;
kichefuchefu,
na mchefuko
wa tumbo
baadaye
mchana
Kula kitu chochote mara tu uamkapo. Kula
kidogo mara kwa mara vyakula vya wanga au
matunda au biskuti wakati wa mchana. Epuka
kukaa na njaa.
Kufunga
choo
Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi, vyakula vya
nafaka, matunda mabichi na mbogamboga na
vyakula vya jamii ya kunde (maharage na
nyegere). Kunywa angalau bilauri (au
vikombe) saba hadi vinane vya majimaji
(usihesabu kahawa au chai) kila siku. Fanya
mazoezi kiasi kila siku.
Kuvimbiwa/
Kujaa Gesi
Jaribu kujilegeza, hasa wakati wa kula
chakula, usile chakula kwa pupa. Kula milo
sita kidogo kidogo kwa siku. Epuka vyakula
vinavyotengeneza gesi kama vile maharage,
kabichi na vitunguu.
Kiungulia
Epuka vyakula vilivyokaangwa, vyenye mafuta
mengi, nyama ya mbavu. Usitumie krimu kali,
vileo, soda, kahawa. Jilegeze. Vaa mavazi
yasiyobana kiuno. Lala chali.
Uangalizi wa
Matiti
Vaa sidiria ili kulinda matiti, hata wakati
unapolala.
Kuvimba
Epuka vyakula vyenye chumvi nyingi, lakini
usiache kuweka chumvi kwenye chakula
chako.
Uchovu
Kula chakula chenye virutubishi vya kutosha.
Pata muda wa kutosha kupumzika, lala
angalau kidogo wakati wa mchana.


vile vichomi, kikohozi, mafua na polio. Chakula hiki cha ajabu
ambacho wewe unatengeneza, maziwa yako, ndicho chakula
pekee anachohitaji mwanao katika kipindi cha miezi sita ya
mwanzo ya uhai wake. Usimpe kitu chochote kingine kwa miezi
minne ya kwanza hata maji, au uji, au mchuzi wa machungwa,
maana vinaweza kusumbua tumbo lake. Tumbo lake linahitaji
maziwa tu mpaka afike umri wa miezi minne.
Wakati wa matunzo ya mwanao, kumbuka, unachokula
hujionyesha katika maziwa yako. Ukila chakula fulani ambacho
mtoto wako kinamletea madhara, ni wazi madhara yataonekana.
Kama mtoto wako umnyonyeshaye akishindwa kuvumilia maziwa
yako, daktari wako atakushauri kuacha kula aina fulani ya chakula
unachokula.
Lishe Inayofaa Wakati wa Ujauzito:
Kumpa mtoto nafasi nzuri ya kukua vema na afya bora
Jambo moja jema unaloweza kufanya kwa ajili ya mtoto
wako mchanga kabla hajazaliwa ni kula lishe bora na kuhakikisha
unampa mtoto mlo ambao unaviini-lishe ambavyo mtoto anahitaji ili
azidi kukua. Hii haina maana kuwa unakula mlo wa watu wawili.
Ina maana kuwa huna budi kula kwa afya ujihadhari kuwa wewe na
mtoto unahitaji zaidi virutubisho wakati wa ujauzito na ulezi wa
mimba.
Ujauzito huongeza mara dufu myeyuko wa chakula mwilini,
hivyo fahamu kuwa wakati huu wa ujauzito unahitaji nguvu za
ziada -- lakini si uwingi wa vyakula ndio unahitajika, bali ni ubora
au thamani ya chakula. Unahitaji kiasi kinachotosheleza na
chenye aina zote za vyakula:
Maziwa Maziwa, jibini, mtindi
Nyama Samaki, nyama, kuku, maharage
makavu au njegele, mayai, njugu,
mbegu, siagi ya karanga
Nafaka Nafaka zote kama vile Ugali, uji,
au mikate, biskuti, wali
Matunda na
Mbogamboga
Matunda yenye vitamini C jamii ya
machungwa, forosadi, mboga
zenye Vitamin A za kijani,
spinachi
Chakula chenye uwiano sahihi ndani yake kikiwa na vitamini
na madini chafaa sana na ni cha muhimu kwako na kwa mtoto. Ili
mtoto apate virutubisho katika mfululizo mahususi, ni vema kula
chakula kidogo kidogo lakini mara nyingi kuliko kula chakula kingi
sana mara mbili au tatu na ukakaa bila chakula kwa muda mrefu.
Katika sehemu ifuatayo, utajifunza mabadiliko ambayo mwili
wako utayapata wakati mtoto anapokua ndani yako. Itadhihirika na
utaona ni kwa nini lishe bora ni ya muhimu.


matumbo ya mtoto, humlinda mtoto dhidi ya maambukizi.
Baada ya nyonyo zako kutoa yale maji maji, zitaanza kutoa
maziwa ya mpita ambapo baada ya majuma mawili maziwa halisi
yataanza kutoka. Hivi haya maziwa halisi yana virutubisho gani?
Kiasi cha asilimia 88 ni maji. Virutubishi vingine ni asilimia 55
mafuta, asilimia 37 vyakula vya wanga na asilimia 8 protini.
Mtajuaje kuwa mtoto wako ana njaa? Atakujulisha tu. Njia
nzuri ya kumlea mtoto ni kumnyonyesha kila anapoonekana kuwa
na njaa.
Unapomnyonyesha mwanao, utahitaji vyakula vyenye ubora
wa juu kuliko hata wakati wa ujauzito, na utakitaji kalori nyingi zaidi
ili utiwe nguvu kuliko wakati wa ujauzito. Uzito uliokuwa nao
wakati wa ujauzito sasa utahifadhiwa kama mafuta ndani ya mwili
wako, na yatakupatia nguvu zinazohitajiwa katika kutoa maziwa au
kutengeneza maziwa. Lishe bora iliyojaa vitamini zote
zinazohitajiwa mwilini siyo tu kwamba itakuwezesha kutunga
maziwa mengi, bali maziwa yako yatakuwa yenye viinilishe
ambavyo hasa vitamnufaisha mtoto wako.
Neno kuhusu madawa: Kwa vile inafahamika kuwa dawa
nyingi zinaweza kupitishwa kutoka kwa mama hadi kwa mtoto
wakati wa kunyonyesha, mwone daktari wako akushauri juu ya tiba
zozote utakazohitaji wakati wa kumlea mwanao.
Lishe kwa Mtoto Wako
Zipo sababu nyingi kwa nini unyonyeshaji ni njia bora zaidi
ya kumlisha mtoto wako. Maziwa ya mwilini mwako hayawezi
kumdhuru mtoto wako kwa hali yoyote. Zaidi ya hayo, viini
vilivyoko katika maziwa yako huongeza kinga ndani ya mwili wa
mwanao, au uwezo wa kujikinga na kupigana na maambukizi.
Watoto wanyonyeshwao wanafahamika kuwa huwa
hawasumbuliwi sana dalili za kutokwa na makamasi, vipele au
ukurutu, kutematema mate, pumu, na mchango (msokoto wa
tumbo) au mhangaiko. Viini vilivyoko ndani ya maziwa pia vinaua
bakteria, ukungu na virusi vya magonjwa. Watoto wanyonyeshwao
na mama zao hawana matatizo ya kuhara au kushindwa
kuyeyusha chakula mwilini. Na, utafiti umeonyesha kwamba
maziwa ya mama yana uwezo wa kupambana na magonjwa kama


Nini Kinatokea Baada ya Mtoto Kuzaliwa
Baada ya mtoto kuzaliwa, mji wa mimba utaendelea
kunywea na hivyo kinachofanyika kondo la nyuma huanza
kusukumwa nje. Wakati haya yamefanyika wewe tayari utakuwa
na kitoto chako kichanga mkononi mwako bado kikiwa kimelowa
na pengine kikilia. Wakati huu unaweza kujisikia kwamba hapa
ulimwenguni hakuna mwingine isipokuwa ni wewe na kichanga
chako tu. Akina mama wengi hujisikia kuwa na mchanganyiko wa
kusisimka na mshangao na hupata nafuu ikiwajia mwilini mwao.
Wanawake wengi pia hujisikia mshituko unaowafanya
watetemeke baada ya kujifungua. Hii ni hali ya kawaida
inayojitokeza kwa wazazi lakini hupungua baadaye. Mkunga
atamsafisha mtoto na kukushona iwapo daktari aliongezea njia ili
kutoa nafasi kwa mtoto azaliwe. Tabibu atakikata kile
kiungamwana, na kile kipande kilichosalia hukauka baada ya juma
moja hapo kipande kinapoanguka hubaki na kitovu. Iwapo
kiungamwana hakijakatika ndani ya kipindi cha siku kumi basi
muone tabibu wako.
Ndani ya kipindi cha majuma sita, mji wa mimba hurejea
katika hali yake ya kawaida ya tumbo la uzazi na uzito, na urefu
wake ambao ni: sm 5 kwa sm 8, uzito wake ni kama 75g. Idadi ya
mimba utakazopata, mazoezi, kunyonyesha na hali yako ya mwili
kwa ujumla vyote hivyo vitachangia kubainisha utarejea katika hali
yako na umbo lako lini.
Kunyonyesha & Lishe kwa Mama Anyonyeshaye
Wataalam wanafikiria kuwa unyonyeshaji ni njia bora ya
kustawisha afya ya mtoto mchanga. Zaidi ya kumpatia lishe bora
mtoto na kumpa faida za kitabibu, unyonyeshaji unakufanya
kujisikia vizuri sana. Ni njia nzuri ya kukuambatisha wewe na
mtoto wako kukupatia uzoefu wa aina yake wa ukaribu baina yako
na mtoto mchanga.
Mtoto anapofyonza nyonyo zako zinatoa maziwa, ingawaje
uvujaji wa maziwa hasa huanza siku kadhaa baada ya kujifungua.
Mpaka hapo, mtoto hulishwa kwa majimaji yanayotoka kwenye
nyonyo baada ya kujifungua japokuwa si maziwa halisi. Majimaji
haya ambayo huitwa danga, yanao uwezo wa kusafisha utumbo na







Wiki ya Sita
· Unaweza kujisikia kutapika unapoamka
asubuhi au unapopika. Sehemu ya kike
**** itakuwa na rangi ya sambarau. Mji wa
uzazi umefikia vipimo kama chenza.
· Mtoto ameanza kuwa na kichwa na mwili, na
ubongo wake ni mkubwa. Ana mwanzo wa
miguu na mikono. Mwisho wa wiki hii, ana
damu na mishipa ya damu. Ana taya na
mdomo, na mwanzo wa meno kumi kila
upande wa taya. Vipimo vyake ni kama
chembe cha mchele, yaani mm 6.


Wiki ya Saba
· Unaweza kujisikia kizunguzungu ukisimama
muda mrefu. Matiti yameongezeka vipimo
na chuchu zinasimama zaidi. Labda
unajisikia kama kulia machozi kwa urahisi.
· Mtoto ana miguu na mikono, na mashimo
mwishoni ambayo yatakuwa vidole. Uti wa
mgongo na ubongo ni kamili, na kichwa
kinaonekana kama binadamu, na matundu
ya pua na mdomo. Anaanza kupata
mapafu. Mtoto ana sm 1.3.





Wiki ya Nane
· Unaweza kukuta kwamba huna hamu ya
kula vyakula fulani. Labda utatoa kama
majimaji sehemu za siri, lakini bila harufu au
maumivu.
· Mtoto ana ini, mafigo, utumbo n.k. ingawa
hazijakamilika bado. Anaanza kuwa na
macho na masikio, na uso wa binadamu.

Ana sm 2.5.
 
MAAJABU YA MIMBA HONGERA KWA KUPATA MIMBA PARTI -3







Wiki yaTisa
· Ufizi wako unaweza kuwa laini kuliko
kawaida na ni muhimu kupiga mswaki vizuri
mpaka utakapojifungua.
· Mtoto ana vidole vyake mikononi na miguuni.
Anaanza kucheza tumboni ingawa huwezi
kusikia bado. Mtoto ana uzito kama zabibu

Uchungu na Kujifungua
Uchungu hakika ni mojawapo ya mafumbo makubwa, kwa
kuwa sayansi bado haijatambua kitu gani kinachoanzisha. Hata
hivyo, yawezekana daktari wako ameshakueleza dalili za
waziwazi, japokuwa haiwezekani mama wajawazito wawili wakawa
na uzoefu ule ule wa uchungu. Kwa baadhi ya akinamama
uchungu kwao ni jambo gumu lisiloelezeka, wakati kwa wengine
uchungu ni maumivu ya kawaida.


Kabla kipindi hakijachanganya, unaweza kujisikia kubanwa
na misuli ambayo huchukuwa kiasi cha kati ya sekunde 15 hadi 20,
na kinarudia tena kila baada ya dakika 10. Kipindi hiki hujulikana
kama uchungu usio wa kweli. Wakati mtoto anapokuwa tayari kwa
kuzaliwa, mji wa mimba huanza kuwa mwembamba. Kutokana na
hali hii mtoto hujinyoosha na kuweka shinikizo katika mlango wa
uzazi. Yawezekana kukawa na kuvuja kwa ute wenye
kuchanganyika na damu kwenye uke wako, hii ina maana kuwa
mlango wa mimba unaanza kunyooka, au kutanuka, haya ni
maandalizi ya njia ya mtoto kupita.
Kwa baadhi ya wanawake, chupa hupasuka. Hii inajulikana

kama kuvunjika kwa chupa. Inaweza kusababisha kuchuruzika
kwa maji, au kumwagika maji mengi. Kubanwa kwa misuli
kunaweza kutokea (kiasi cha sekunde 40 bila tukio), na kubanwa
huko kwa misuli kunaongezeka maradufu kadri mji wa mimba
unavyojivuta na kusukuma mtoto chini, wakati mlango wa mimba
unaposukuma juu na nyuma.

Kuzaliwa kwa mtoto kunaweza kuchukua kati ya saa moja
hadi masaa 14 pengine zaidi ya hapo. Mtoto wa kwanza kwa
kawaida huchukua kiasi cha saa 14; watoto wengine wataokuja

kuzaliwa baadaye na mama huyo watachukua kiasi cha saa nane.
Kiasi cha maumivu hutofautiana baina ya wawawake.
Kuzaliwa kwa mtoto si rahisi kwake pia Pumzi ya kwanza
ya mtoto ni ngumu sasa kwake; inaweza kufananishwa na mtoto

kupuliza pulizo. Mtoto mchanga anapaswa kutumia nguvu mara
tano zaidi kuliko kawaida kuvuta hewa ndani ya mapafu yake
madogo. Wakati kiunga mwana (umbilical cord) kinapotoka na
kukatwa, hapo ndipo mwisho wake wa kufanya kazi. Sasa mtoto
anajitegemea kwa mahitaji yote.
Miezi Mitatu ya Mwanzo
Mtoto

Katika muda wa majuma sita, kiinitete (embryo), ambacho
huanza kukua kinaanza na kichwa kuelekea chini, huwa na fuvu
ambalo lina macho yaliyo katika hatua za awali na masikio,
ingawaje wakati huo kiumbe hiki huonekana zaidi kuwa kama

kijisamaki kidogo chenye kichwa kikubwa kuliko umbo la mtoto wa
binadamu. Kiumbe hiki japo bado kina vipimo kama chembe ya
mchele, ukubwa wake ni mara 10,000 zaidi kuliko yai lilipoungana
na mbegu za kiume, na ukubwa inaongezeka mara mbili kila juma.

Kiumbe hiki tayari huwa na ubongo, figo, ini, mfuko wa kuyeyusha
chakula, mkondo wa damu, moyo uliogawanyika katika sehemu
mbili unaopiga piga na vichipukizi vifupi ambavyo baadaye hukua
na kuwa mikono na miguu. Kiumbe hiki ambacho huitwa kiinitete
kina matendo hiari ambayo hujitokeza yenyewe hasa katika juma
la saba japokuwa wewe huwezi kusikia kinapo jirusha.
Waweza kutambua sura ya kiumbe hiki kuwa ni sura ya

binadamu katika kipindi cha juma la nane. Kichwa kinakuwa ni
kikubwa kuliko kiwiliwili. Macho huzibwa na ngozi ambayo
baadaye hugawanyika na hutengeneza kope. Mikono, miguu
huanza kujitokeza na kukua, nazo mbavu huchomoza. Kiumbe
hiki huwa pia kina mifupa ambayo iko katika hali ya ulaini (kama
unavyoweza kuhisi ncha ya pua yako ukiigusa). Viungo vya uzazi
ambavyo ni vidogo sana huanza kuonekana japokuwa siyo rahisi
kutambua mtoto huyu anaweza kuwa wa kike au wa kiume. Uzito
wake ni chini ya ule wa kidonge cha aspirini!
Mama

Dalili ya kwanza ya mabadiliko ya ujauzito hutambuliwa
katika matiti yako huanza kuvimba na ile sehemu ya chuchu
inayoonekana rangi ya udongo huanza kuwa nyeusi. Matiti yako
huanza kuwa laini na mazito. Mwili huanza kuwa mzito na mchovu
wakati unapokuwa unaanza kujirekebisha tayari kupokea maisha
mapya katika mwili wako hasa kama ni mimba yako ya kwanza


Vitu vingi hutokea ndani ya mwili wako katika miezi hii ya
mwanzo, hata hivyo huwa ni kwa kiasi kidogo sana kiasi
kwamba wanawake wengi hawaonyeshi.
Wanawake wengi wanaweza kupata ugonjwa wa
asubuhi kichefuchefu ambacho kinaweza kutokea wakati
wowote katika siku. Unaweza kuondoa hali hii ya

kichefuchefu kwa kula chochote mara tu baada ya kuamka
asubuhi. Ili kuzuia kichefuchefu ambacho kinaweza kutokea
wakati wowote wakati wa mchana, hakikisha unapumzika vya
kutosha kwa kuwa uchovu unaweza kuchangia katika
kukuletea kichefuchefu. Njaa pia yaweza kusababisha
kichefuchefu, hivyo ili kukizuia, pata vitu vidogo vidogo vya
kutafuna wakati wa mchana.

Katika miezi hii mitatu ya mwanzo ya ujauzito mjamzito
huwa na jazba (hasira) sana. Jazba hizi pengine
husababishwa na mabadiliko katika vichocheo ambayo
hukufanya ujisikie vibaya pamoja na kichefuchefu. Ya
kupasa pia kujirekebisha kisaikolojia (kihisia) ukijichukulia
kuwa unaye mtoto ndani yako na majukumu mapya ambayo
utayapata si tu baada ya kuzaliwa mtoto bali hata kabla.
Lishe bora, kama ambavyo tumekwisha taja hapo
mwanzo, ni moja ya wajibu wa kuchukua kabla mtoto

hajazaliwa, kwa sababu mimba husababisha ongezeko katika
mahitaji yako ya vitamini na madini. Pale tu unapojihisi kuwa
umepata mimba, unapaswa kula chakula chenye lishe bora,
kwani chakula ulacho huchangia katika makuzi na maendeleo
ya mtoto. Madaktari wengi hutoa maelekezo ya matumizi ya
multi-vitamini au madini ambayo yametengenezwa maalum
kwa ajili ya mama wajawazito na watoto walioko tumboni.

Lakini ni muhimu zaidi kupata lishe bora wakati wa ujauzito
kuliko kumeza vidonge hasa miezi mitatu ya mwanzo kwa vile
katika kipindi hiki viungo vya uzazi vya mtoto ndio
vinatengenezwa. Protini huhitajika zaidi kwa mtoto
anapoendelea kukua na vyakula vingine vya kulikuza.
Proteini inayotokana na vyakula vya asili (yaani vinavyotoka
mashambani) hutengeneza viini viitwavyo amino acid
ambavyo huleta uhai ndani ya mwili, umuhimu wa protein ni


Wiki yaKumi

· Tumbo la uzazi lina vipimo kama chungwa,
lakini bado huwezi kusikia kwa kupima
tumboni.

· Kondo inatengeneza kichocheo cha
progesterone kuwezesha mimba kuendelea.
Mtoto ana vifundo vya miguu na mikono.
Ana sm 4.5.



Wiki yaKumi naMoja
· Utaanza kupona kwa hali ya kutapika. Kiasi
cha damu yako inaongezeka kutoka sasa
mpaka wiki ya 30.
· Mtoto ana ovary au pumbu zake, na
inaonekana kama ni wa kike au wa kiume.
Sasa, mwili wa mtoto karibu umekwisha
tengenezwa -- Sasa unahitaji kukua tu.



Wiki ya Kumi naMbili
· Unaanza kusikia tumbo la uzazi tumboni.
· Mtoto ana nyukope. Ana cheza zaidi
tumboni, na anajinyosha, kupiga miayo,
jinyonganyonga vidole vyake. Ana sm 6.5
na ana uzito wa 18g.



Wiki yaKumi naTatu
· Hutatapika tena kwa sababu ya mimba.
· Mtoto anaendelea kuongezeka vipimo
vyake. Ana sm 8.5 na uzito wa 28g.



Wiki ya Kumi naNne
· Kuchoka kumepungua kidogo. Unaanza
kujisikia na afya nzuri. Chuchu za matiti
zinaweza kuwa nyeusi zaidi.
· Mtoto ana nyushi na nywele kidogo.
Anakunywa maji ndani ya chupa ya uzazi
na kukojoa.
Kumi na


Wiki ya Kumi naTano
· Utaanza kuona nguo zinabana kidogo.
Moyo wako umeongezeka nguvu wake
kwa asilimia 20.
· Nywele za mtoto zinaongezeka na kuwa
nyeusi kabisa. Anajaribu kunyonya
vidole vyake.



Wiki ya Kumi na Sita
· Unaanza kuweza kusikia mtoto akicheza
tumboni.
· Mifupa ya mtoto inaanza kuwa migumu.
Ana ulaika juu ya mwili wake wote. Ana
kucha za vidole. Angeweza kulala ndani
ya kikombe cha chai; ana vipimo kama
mkono yako. Ana sm 16 na 135g.

Ukuaji wa haraka haraka wa mtoto utakupunguzia nguvu
zako, hivyo jishibishe kwa chakula kingi chenye wanga, matunda
na mbogamboga. Usisahau vyakula vya mafuta, vyakula hivi huwa
vimejaa nishati iletayo nguvu mwilini. Mafuta pia yanakusaidia
kufyonza virutubishi, lakini kumbuka pia, mafuta yanaweza

kutengeneza calori. Mafuta yaletayo afya sana mwilini mwako ni
pamoja na yale yatokanayo na tende, karanga, mahindi, soya na
alizeti); mengine hutokana na korosho, mizeituni, njugu na
karanga. Vyakula vyenye protini pia vina mafuta, nyama, samaki,
maziwa na vyakula vyenye kutokana na maziwa kama vile jibini,
siagi ya karanga vyafaa sana
.


Miezi Mitatu ya Awamu ya Mwisho
Mtoto

Katika majuma ishirini na nane, mtoto huwa amekuwa sana
kiasi kwamba hawezi kujisogeza ndani ya tumbo lako. Ingawaje
siku zake za kujibinua huwa zimemalizika, anakuwa anatumia
muda mwingi kujinyonya dole gumba lake.
Nywele zake huwa zimerefuka. Wakati wa mwezi wa nane

(kuanzia juma la 32 hadi la 36) mtoto huongezeka uzito wake kwa
900g, uzito huu huchangiwa na mafuta ya kinga.
Kipindi fulani ndani ya kipindi cha mwisho cha ujauzito (kati
ya wiki ya 36 na ya arobaini), mtoto hujigeuza na kujituliza chini

katika nyonga, kichwa chake kikiwa kimegota sawasawa ndani ya
misuli ya nyonga zako. Hii ina maana kuwa mtoto tayari
anajiandaa na ana hamu ya kuzaliwa na wewe. Inapofika juma la
arobaini, au muhula, ukuaji wa mtoto kabla ya kuzaliwa huwa
umekamilika. Mtoto anakuwa shupavu mwenye urefu wa kati ya

sm 45 na sm 53. Mzito wa kati ya 2.5kg na 4.5kg
 
MAAJABU YA MIMBA HONGERA KWA KUPATA MIMBA PARTI -4









Wiki ya Kumi na Saba


· Unaweza kutoa jasho zaidi kuliko kawaida, na
labda pua inaziba. Unaweza kusikia tumbo la
uzazi limefika nusu njia mpaka utovu.
· Mtoto anakaa kwenye robo lita ya maji.
Anaweza kusikia kelele kubwa nje ya mwili
wako.

Wiki ya · Kama ni mimba yako ya kwanza, utatambua
akili yako tayari huwa vimeshapokea ile hali ya ujauzito na kujisikia
shauku ya uchungu na uzazi.

Katika wiki la kumi na nane la ujauzito wanawake wengi
wajawazito huanza kuvaa tenite kwa vile wakati huu mimba
huanza kuonekana waziwazi. Bila kujali kama umeanza
kuonyesha mimba au la, muda mfupi tu utaanza kujisikia mtoto
akicheza cheza tumboni, akipiga mateke na kujigeuzageuza na

hata kuwa na kwikwi. Kitoto hiki kinakuwa na uwezo wa kulala na
kuamka kama mtoto mchanga aliyezaliwa; anapokuwa ameamka,
anajisogeza sogeza ndani ya yale majimaji akiwa huru kabisa
kama mtu aliyeko angani akielea kutoka upande huu kuelekea
upande mwingine, akipanda juu na kushuka chini.
Katika miezi mitatu ya pili tangu mimba kutungwa,

unapaswa kula zaidi vyakula vyenye majimaji kwa kiasi cha
vikombe saba au vinane kwa siku. Unashauriwa kunywa maji,
maziwa, juisi ya matunda (maji ya matunda) au supu. Unahitaji
majimaji kwa sababu lile kondo la nyuma linapaswa kutoa damu

nyingi kwa ajili ya mtoto aliyeko tumboni. Ili kupata damu nyingi
unahitaji vitu vya maji maji zaidi. Vitu kama chai, kahawa na soda
si vizuri ukavipendelea kwa vile husababisha upoteze maji mengi
kwa kukojoa kojoa.

Wakati uliopita (zamani kidogo), wajawazito wengi
waliambiwa wapunguze chumvi katika vyakula vyao, lakini sasa
madaktari wametambua kuwa kitoto kichanga (au kwa lugha ya
kitaalamu fetus kimjusi) kinahitaji chumvi ili kukua vizuri. Chumvi

itakusaidia pia wewe kutunza majimaji mwilini, hivyo, weka chumvi
katika chakula chako hadi ikolee, bila kuzidisha.
Wakati wa uja uzito, kinga yako ya mwili imepungua. Ni
muhimu kujilinda dhidi ya malaria. Nunua chandalua na kukitia
dawa ya kuwaua mbu. Dalili ya malaria pia yanabadilika wakati wa

mimba. Ukijisikia ovyoovyo, nenda kupimwa damu yako mapema.
Utapewa dawa ya SP mara mbili wakati wa mimba yako
baada ya wiki 20 na wiki 30. Hizi zinawaua wadudu wa malaria
ambao wanakaa kimya mwilini, na kukulinda na kupungukiwa
damu kwa sababu ya malaria sugu.
Pia utapigwa sindano ya Tetanus (Pepo punda) kama huna
kinga, ili kulinda mtoto wakati akiwa mchanga

Mama

Sasa unaingia awamu ya tatu ya ujauzito wako. Mume
wako, jamaa zako na marafiki wanaweza sasa kujifurahisha kwa
kugusagusa tumbo lako, kwa vile sasa wataweza kuhisi mateke ya
mtoto.

Katika muda wa mwezi wa saba wa mimba, unaweza
kujisikia kutokwa na majimaji yakidondoka katika chuchu yenye
rangi ya njano haya yanaitwa danga au kwa lugha ya kitaalamu
colostrum. (Unaweza kuona tena Kolostrumi hii ikichuruzika
baada ya kujifungua, kabla ya maziwa yenyewe kuanza kutoka,
usiogope. Hii haina maana kwamba huwezi kutoa maziwa siku za
baadaye.

Katika mwezi wako wa nane, mtoto wako anakuwa na
shughuli nyingi utafikiri umebeba mwanariadha wa michezo ya

Olimpiki tumboni mwako! Hata kama mtoto wako atarudiarudia, au
hata akijirusha haraka haraka na kujigeuzageuza, usiogope. Hii
inaweza kuwa si kitu chochote isipokuwa ni kwikwi tu.
Kati ya wiki tatu na sita kabla ya kuzaliwa, kichwa cha mtoto
unaweza kukihisi kama tikiti maji kati ya mapaja yako. Unaweza

kujisikia usiye na raha ukitaka kukaa chini. Unaweza pia kujisikia
kama ni kitu cha kuchekesha na kujihisi kama kuna kengele
inagongagonga ndani ya uke wako, haya ni matokeo ya mtoto
wako kuinua kichwa chake kukishusha na kujigonga sehemu ya
chini ya nyonga zako.

Wakati huu utambue kuwa mtoto yuko tayari, kipindi hiki cha
miezi mitatu ya mwisho chaweza kuwa ni cha changamoto kwako
hasa kuhusiana na hisia zako. Akina mama wengi huanza kuhisi
shauku ya uchungu wa kuzaa, pengine huanza kuwaza juu ya
mipangilio ya kifedha itakuwaje baada ya mtoto kuzaliwa. Lakini
furaha ya matazamio na uzoefu mwingine waweza kumaliza
wasiwasi huu. Wazazi wote wawili wakizungumza kwa pamoja juu
ya kuzaliwa kwa mtoto yaweza kuleta furaha.

Kama hapo awali, lishe bora wakati huu wa miezi mitatu ya
mwisho ni ya muhimu sana. Chembe chembe za ubongo wa
mtoto huanza kujitengeneza haraka haraka, hasa katika miezi
miwili ya mwisho kabla mtoto hajazaliwa. Ule vizuri sasa, kwa

kuwa utakuwa unasaidia kuchangia upendeleo wa mtoto baada ya Wiki Mendeleo ya Mtoto na Mama Wakati wa Ujauzito



Wiki yaKumi naNane
· Kama ni mimba yako ya kwanza, utatambua
mazunguko ya mtoto akicheza tumboni.
· Mtoto anaanza kunenepa zaidi ingawa bado
unaweza kuona mishipa ya damu yake kwa
sababu ya ngozi nyembamba. Ana sm 20 na
anapenda kupiga teke.



Wiki yaKumi naTisa

· Unaona kwamba unanenepa kidogo, na tumbo
linaanza kueneza.
· Mtoto anaanza kupata jicho la meno ya pili
kwenye taya.



Wiki yaIshirini

· Unaweza kuanza kuona na macho michezo ya
mtoto, na mtu anaweza kusikia kutoka nje.
Atakuwa na kipindi anapolala, hasa ukitembea
kwa sababu unampembeza tumboni. Tumbo
la uzazi limefika utovu.
· Kuna glands kwenye ngozi ya mtoto
zinazotengeneza kama majimaji. Hii inafunika
ngozi yote ya mtoto kulainisha na kulinda.

Mtoto ana sm 25.


Wiki yaIshirini na Moja

· Unaweza kuanza kujisikia kiungulia.
(Heartburn)
· Mtoto ana 450g. Anacheza sana tumboni.



Wiki yaIshirini na Mbili

· Hutataka kusimama kwa vipindi virefu. Ufizi
unaweza kuvimba.
· Mtoto analala na kuamka tumboni.



Wiki yaIshirini naTatu

·
Unaweza kutofautisha sehemu mbalimbali ya
mwili wa mtoto tumboni. Tumboni itasikia kama
inavuta wakati fulani.
· Mtoto bado hajanenepa kabisa, lakini
anafanana na kama atakavyokuwa
atakapozaliwa.


Wiki ya · Daktari ataweza kusikiliza moyo wa mtoto



kuzaliwa, kuhusiana na ujuzi wa kujifunza na nguvu za mwili.
Haishauriwi kuruka mlo wowote wakati wa ujauzito. Baadhi
ya wataalam wanahisi kuwa hata upunguzaji wa virutubisho
vyenye ubora wa juu unaweza kuchangia matatizo kwa mtoto
wako. Hivyo, ngangania ulaji ule ule wa chakula muhimu kama
ilivyojadiliwa huko nyuma.

Baadhi ya wataalam wanaona kwamba madini ya chuma ni
virutubisho namba moja ambavyo hukosekana kwa wajawazito;

upungufu wa damu hujitokeza baadaye, hivyo hakikisha unashika
barabara ongezeko la utumiaji wa vyakula vyenye madini ya
chuma. Ulaji wa vyakula yenye Vitamini C kama vile maji ya
machungwa, utaimarisha ufyonzaji wa chuma ndani ya mwili wako.

Vyakula Vyenye madini ya Chuma
Maini
Nyama ya Ngombe
Spinachi
Maharage makavu
Ngano

Katika miezi mitatu ya mwisho, mtoto anahitaji zaidi chokaa
(calcium) kwa ajili ya utengenezaji wa mifupa na meno. Iwapo
hutapata chenye chokaa katika mlo wako ambayo huhitajiwa na
kitoto (kimjusi) na kwa utengenezaji wa maziwa, basi itatolewa
katika mifupa na meno yako mwenyewe.
Usipunguze chakula ili mtoto azaliwe mdogo kafanya
hivyo inaweza kuharibu afya yake
Wiki Mendeleo ya Mtoto na Mama Wakati wa Ujauzito
 
MAAJABU YA MIMBA HONGERA KWA KUPATA MIMBA PARTI-5




Wiki yaIshirini naNne
· Daktari ataweza kusikiliza moyo wa mtoto
tumboni.
· Mtoto ana sm 32 na 500g. (vipimo kama
risiva ya simu) Mapafu yake bado hayawezi
kuhema nje, lakini mafigo, ini na kadhilika zipo
tayari. Labda anapenda kusikiliza musiki.


Wiki yaIshirini naTano
· Labda utapata shida ya kulala usingizi.
Unaweza kutaka kukojoa mara nyingi
· Nafasi ya mtoto inaanza kupungua.


Wiki yaIshirini naSita
· Tumbo la uzazi linaongezeka kwa sentimeta
moja kila wiki.
· Ngozi ya mtoto inaanza kuwa nzito zaidi --
huwezi kuona ndani ya mwili wake sasa.


Wiki yaIshirini naSaba
· Unaweza kuanza kutoa mwanzo wa maziwa
kutoka kwa matiti.
· Mtoto anaweza kufungua macho yake.
Anaweza kuona mwanga na giza.


Wiki yaIshirini naNane
· Utaongeza uzito wako mpaka wiki ya 36.
Tumbo la uzazi limefika kati ya utovu na kifua.
· Mtoto ana sm 38 na 900g


Wiki yaIshirini naTisa
· Unaanza kujisikia kama hakuna nafasi zaidi
tumboni.
· Ubongo wa mtoto inaendeleza zaidi. Anasikia
vizuri.


Wiki yaThelathini
· Jaribu kuweka miguu juu unapokaa.
· Mikazo ya tumbo la uzazi inaanza kubana
mtoto ingawa huwezi kusikia bado. Moyo
wake inapiga kati ya mara 120-160 kila
dakika.



Wiki yaThelathini na Moja
· Unaweza kukosa pumzi ukipanda mlima au
kubeba mizigo.
· Mtoto ana 1.8kg.



Wiki yaThelathinina Mbili
· Unasikia uzito wa tumbo lako.
· Mtoto anaweza kuwa na kwikwi. Ana sm 42.
Bado anahitaji kunenepa.
· Ujisikie mtoto akicheza tumboni isipungua mara
10 kwa siku.

katika utengenezaji wa mkusanyiko wa seli mucilini na viungo vya
mtoto hasa wakati huu wa mwanzo kabla ya mtoto kuzaliwa kuliko
wakati mwingine wowote wa uhai wake.
Baadhi ya vyakula vyenye asili ya protein kama vile
maharage makavu na vile vya jamii ya njegere, (choroko, dengu,
mbaazi na kunde), mbogamboga, nafaka na ngano havina amino
acids iliyo na uwiano sawia hivyo huitwa protini isiyokamili.
Vyakula hivi vikiliwa peke yake havikupi thamani halisi ya protin.
Hivyo, wakati wa ujauzito unashauriwa kula chakula kilicho na

protini ya kutosha kama vile samaki, kuku, nyama ya minofu isiyo
na mafuta, maziwa, jibini viliwe pamoja na jamii ya kunde.
Mbali na mahitaji yako kuongezeka kuhusiana na protini,
ujauzito unaongeza mahitaji ya lishe zenye madini ya chuma,

madini ya chokaa (calcium), vitamin A, C, D, E, B6, B12, thiamini,
riboflavin, niacin, fosiforasi na magnesium. (Kwa orodha kamili ya
vyakula vilivyopendekezwa, angalia kiambatisho). Wewe na mtoto
wako aliye tumboni mnahitaji zinki ambayo ni ya muhimu katika
kuunganisha protini na madini joto kwa sababu huathiri kikoromeo
cha mtoto, ambacho ndicho huanza kutengenezwa katika miezi ya
mwanzo ya ujauzito.

Ni muhimu kwenda kliniki ya akinamama wajawazito mara
unapojihisi kuwa na mimba. Wakunga wanaweza kuhakikisha
kwamba mimba inaendelea vizuri. Pia ni muhimu kipimwa damu
yako wadudu wa kaswende. Wadudu hawa wanaweza
kusababisha mtoto kufariki tumboni wakati wowote mpaka azaliwe,
lakini mara nyingi wewe huna dalili zozote za ugonjwa. Kaswende
inatibika kwa urahisi.


Miezi Mitatu ya Awamu ya Pili
Mtoto


Katika majuma kumi na mbili, kiinitete (embryo) hubadilika
na kuwa kimjusi (fetus) na mnaweza kutambua kama ni
mvulana au msichana. Uso wa mtoto huanza kutakata na
kupendeza. Anaanza kuwa na ala za sauti (midomo, ulimi)
kama kungekuwa na hewa ndani ya tumbo sauti ya mtoto

ingesikika akilia. Wakati huu mtoto anakuwa na uti wa mgongo
na moyo ulio na vyumba vinne kama mtu mzima. Siyo tu
kwamba mtoto anaweza kupiga mateke, anaweza pia kupindisha
vidole vyake. Katika majuma kumi na sita, baadhi ya wamama
wajawazito huweza kugundua mwendo wa mtoto, kama vile
kupigapiga kama kuchezacheza ambako kunaelekea

kutambulika wazi kuwa ni mateke na kuruka kwa kusogea
mbele. Mtoto hufunikwa na vinyweleo, ambavyo baadaye
hubanduka (hunyumbuliwa). Katika mwezi wa nne mtoto hukua
na kurefuka kufikia kati ya sm 20 hadi sm 25, au tuseme urefu
wake huongezeka kama nusu ya ule atakaozaliwa nao. Uzito
wake utaongezeka mara sita japokuwa kwa sasa hivi uzito wake
utabaki kama 150g tu.

Katika juma la ishirini na nne, mtoto anakuwa na urefu wa
sm 30 na anakuwa amefunikwa na ute mzito ambao
hushikamana na vinyweleo, kazi ya ute huu ni kumlinda mtoto.
Watoto wengi huzaliwa wakiwa bado wamefunikwa na ute huu

mzito katika ngozi zao nyororo. Si tu kwamba wewe unatambua
jinsi mtoto anavyochezacheza, bali hata yeye hutambua wewe
unavyotembea na mazingira yanayokuzunguka. Mitetemeko,
sauti kubwa ya muziki au mitetemo zinaweza kumwamsha.
Katika mwezi wa sita, mtoto anaweza kufungua macho na
kuangalia vitu vinavyomzunguka. Hakika huyu ni mtu mdogo.

Mama

Katika awamu hii ya pili ya ujauzito wako, baadhi ya
mambo ya ajabu sana yatatokea. Utagundua kuwa miezi hii
mitatu awamu ya pili utajisikia kuwa na nguvu na kujisikia vizuri.
Kujisikia huku vizuri kimwili na kihisia, kunaweza kusababishwa
na kupungua kwa hali ya kujisikia kichefuchefu. Mwili wako na



Wiki yaThelathinina Tatu
· Ujisikie mtoto akicheza tumboni isipungua mara
10 kwa siku.
· Mtoto analala kichwa chini mpaka azaliwe.


Wiki yaThelathinina Nne
· Nusu ya uzito ambao umeongeza ni mtoto,
kondo na maji nusu ni mwilini wako ili uwe na
akiba ya kunyonyesha mtoto.
· Mtoto anaona mwanga ukitoa nguo



Wiki yaThelathinina Tano
· Unaweza kuzidi kuota ndoto usiku. Labda
mgongo utaumwa.
· Mtoto ana sm 44 na 2.5kg.


Wiki yaThelathinina Sita
· Mtoto atatelemka chini kidogo -- tumbo
linapungua kidogo, lakini sehemu za siri
inaanza kusikia kubwa. Kukosa pumzi kutatulia
kidogo, lakini utataka kukojoa mara nyingi.
· Mtoto ni karibu tayari kuzaliwa.



Wiki yaThelathinina Saba
· Utapata shida kulala vizuri usiku.
· Mtoto anajizoea kuhema tumboni, ingawa yuko
majini. Pumbu za mtoto wakiume zitakuwa
zimetelemka kufika mfuko zao.


Wiki yaThelathinina Nane
· Mtoto anapunguza kucheza kwa sababu ya
nafasi ndogo. Lakini bado umsikie zaidi kuliko
mara 10 kwa siku.
· Mtoto anaongeza uzito wake 28g kwa siku.


Wiki yaThelathinina Tisa
· Unajisikia uzito sana na kuchoka.
· Maji tumboni la uzazi yanabadilishwa kila
masaa matatu. Matumbo ya mtoto yamejaa
majimaji yenye rangi ya kijani au meusi. Ulaika
wake umekwisha kutoka.



Wiki yaArobaini
· Mishipa wako imelainisha kidogo tayari
kuruhusu mtoto azaliwe. Mgongo unaweza
kuumwa.
· Mtoto yuko tayari kabisa kuzaliwa

 
hakika ukuaji una mlolongo mrefu na wakutisha
Usiogope Hakika ukiwa na Mimba upo kwenye Ulinzi wa Bwana Mwenyeezi Mungu. Hakuan kitu chochote kitakacho kupata mpaka wakati wakujifunguwa onsha wasiwasi Muamini Mwenyeezi Mungu utajifunguwa salam tu.
 
Ukiongea hivo roho inaniuma wakati mimi nlitaka kupata kifafa cha mimba wakanifanyia oparation wiki 32 na mtoto akafa
 
Usiogope Hakika ukiwa na Mimba upo kwenye Ulinzi wa Bwana Mwenyeezi Mungu. Hakuan kitu chochote kitakacho kupata mpaka wakati wakujifunguwa onsha wasiwasi Muamini Mwenyeezi Mungu utajifunguwa salam tu.

amen ubarikiwe
 
nimeona niifufue hii thread![HASHTAG]#mzizimkavu[/HASHTAG] ni noma!
 
Ukiongea hivo roho inaniuma wakati mimi nlitaka kupata kifafa cha mimba wakanifanyia oparation wiki 32 na mtoto akafa
Hapo walikuwa wanasave maisha yako,na kama mtoto angeishi basi ungekuwa ni kwa kudra na Mwenyezi Mungu.Pole sana
 
Back
Top Bottom