Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lugha JF inabidi uzitafakari sana zimejaa mafumbo sana mpaka sawariya ameandika hivyo ujue kuna kitu amemaanisha, kama unajua mashine za kusaga diseal zinavyofanya kazi utakuwa umemwelewaUnajua nyani huwa anaziba macho akiamini kuwa yeye haoni basi na wengine pia wanaomuangalia nao hawaoni.
Kama umeelewa ulichoandika basi AMINI wote pia wanaosoma wameamini nao.
Hivi kweli jamani mashine za kusagia unaweza kusambazia bidhaa mitaani?.
Usafiri unaotumiwa na kampuni hii ya Mohamed interpress kusambaza bidhaa zake hasa kwa hapa dar ni matrekta,caterpillar,listerpeter,au ni mashine zakusaga?
Sasa ye si ndo kaamua kwa faida zake mwenyewe. Au kavunja sheria za nchi? Mwacheni mbunge wangu
Ile ni mashine/engine ya petrol ambazo ni multpurpose, kwa hapa tanzania zinazotumika sana ni auna ya AMEC na JD, kwa sasa JD ndio inatumika. Hizo gARI ZA MOHAMED ENTPRS ni body mfano wa gari imeundwa kisha ikafungwa hizo mashine, hzo mashine zake hazina tofauti na iliyofungwa kwenye POWERTILLER, pia zinatumika kwenye SAWmills sna maeneo wanayopasua miti ya mbao,hasa MAFINGA, lakini pia mashine au hizi injini hutumika kuzalishja umeme,zinafungwa na mota kubwa za kufua umeme kisha unasambazwa,hii ilikuwa ikitumika sana pale RUAHA MBUYUNI kabla ya umeme wa REA haujafika, lakini pia hutumika vijinini kuendeshea vinu vya kusagia na kukoboa (mashine za kusaga na kukoboa. Kiufupi hizo gari za mohamedi ukizichunguza ni kuwa gear box yake inazungushwa na belt/mkanda unaotoka kwenye gurudumu kubwa lililofungwa kwenye hiyo mashine ya amec/jd, yaani haina tofauti na kama ilivyo kwenye powertiler au mashina ya kusaga;. ni hayo tu,ikizona zichunguze,chungulia kwa chini utaona hito mashine imefungwa katikati ya bodi kisha belt imeenda mbele kwenye gear box
Usafiri unaotumiwa na kampuni hii ya Mohamed interpress kusambaza bidhaa zake hasa kwa hapa dar ni matrekta,caterpillar,listerpeter,au ni mashine zakusaga?
Aisee ni kweli vile vigari vikipita kuku wote wanakimbilia mabandani, mbwa wanabweka, ng'ombe wanalia, magari yenye alarm nayo.....yani utazani parapanda inalia.
alafu yale ma power tila yanakelele kinoma, usiombe liwe pembeni yako kwenye foleni ya Dar.
Aisee ni kweli vile vigari vikipita kuku wote wanakimbilia mabandani, mbwa wanabweka, ng'ombe wanalia, magari yenye alarm nayo.....yani utazani parapanda inalia.
Huyu ndio billionea kijana lakini ana wadhifa wa mbunge tena wa kuchaguliwa, karibia vipindi viwili alivyokaa bungeni inasemekana hakuwahi kuchangia wala kuuliza swali! Kiufupi 'najipinga' mwenyewe, huyu sio mbunge bali 'mfadhili' wa jimbo la Singida Mjini.
Pia kuweka sawa kumbukumbu aliingia kwenye mgogolo wa kujitwalia kiwanja cha serikali mjini Dar es Salaam na kumsababishia lawama waziri wa fedha Mustafa Mkukulo!
mkuu,hii kitu,hizo injini ni very fuel economy,hiyo nii work machine, hapo walichochemka ni vitu viwili, moja ni kutokuweka exost ambayo ni silent kama zilivyo jenereta, lakini pia kitendo cha gear box kuendeshwa na belt badala ya shaft ni kitu cha hatari sana kwa gari inayopita mjini,maana sometimes belt hizo huwa zinachomoka au kukatika, balaa lake waulize WALIMA MPUNGA NA WAENDESHA POWERTILLER KULE UBARUKU MBARALI watakuambia mziki wa kuchomoka belt/kukatika wakati powertiler ikiwa imebeba tela lenye mzigo na imekolea speedAsante kwa ufafanuzi mzuri mkuu ila nilipotaja mashine yakusaga kuna watu povu limewatoka humu.Sasa kama nikwaajili ya powertiler,mashine ya mbao,kusaga nk.mjini tunalima mpunga au kupasua mbao? Mimi nadhani tbs huwa wanazuia magari toka japan na kwingineko hadi upate idhini kwao Sasa hapa ilikuaje ??
Ni madoido au marembo?
mbona hukuandika Balafuyamoyo?
mkuu,hii kitu,hizo injini ni very fuel economy,hiyo nii work machine, hapo walichochemka ni vitu viwili, moja ni kutokuweka exost ambayo ni silent kama zilivyo jenereta, lakini pia kitendo cha gear box kuendeshwa na belt badala ya shaft ni kitu cha hatari sana kwa gari inayopita mjini,maana sometimes belt hizo huwa zinachomoka au kukatika, balaa lake waulize WALIMA MPUNGA NA WAENDESHA POWERTILLER KULE UBARUKU MBARALI watakuambia mziki wa kuchomoka belt/kukatika wakati powertiler ikiwa imebeba tela lenye mzigo na imekolea speed