Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Msigwa kwa muda mrefu sana amekuwa na msimamo mkali dhidi ya CCM, msimamo ambao ulitokana na orodha ndefu ya mambo ambayo hakuyapenda sana ndani ya CCM, pamoja na watu wenyewe wa CCM. Lakini sasa, akakorofishana na Mbowe, au tuseme akashindwa uchaguzi ndani ya Chadema na ikawa kichocheo cha badiliko kubwa kwa Msigwa tunaemfahamu.
Sasa suala la kujiuliza, au hasa la kumuuliza Msigwa ni kwamba, yale mambo ambayo hukuyapenda ndani ya CCM, au watu ambao hukuwapenda ndani ya CCM na aliona hawafai kuwa viongozi wa Tanzania, kushindwa kwake uchaguzi ndani ya Chadema, au kukorofishana kwake na Mbowe, kumeyabadilisha au kuwabadilisha watu hao na kufanya sasa yawe mazuri wawe viongozi wazuri?
Kwa mfano, kama Msigwa hakumpenda Bashe kwa uongo kwa Bunge juu ya vibali vya sukari, kukorofishana na Mbowe kunabadilisha uongo aliosema Bashe na kuufanya uwe ukweli? Au kama Msigwa hakumpenda Samia kutokana na mkataba wa bandari kwa DP World, sasa anampenda Samia na Mkataba wa DP World kwa sababu ameshindwa uchaguzi Chadema?
Msigwa anaweza kusema kuna mambo yamebadilika ghafla ndani ya Chadema ndio maana ameondoka, lakini zaidi tungependa kujua ni mambo gani yamebadilishwa ghafla ndani ya CCM na kuanza kuipenda CCM dhidi ya Chadema, au ni unafiki na umalaya wa kisiasa tu tunaoshuhudia hapa?
Ningemwelewa Msigwa kama angeondoka Chadema na kutulia nyumabani, lakini sio kwenda kwenye CCM alikowadosoa kwamuda wote huu. Kwa kufanya hivyo hastahili hata heshima ya kuitwa mchungaji katika unafiki kama huo.