Pre GE2025 Maajabu ya Msigwa ni kwamba kukosana kwake na Mbowe kumefanya mambo yote aliyoyachukia ndani ya CCM kwa miaka mingi yabadilike ghafla na kuwa mazuri!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wizara ya Afya kila watu 4 mmoja kati yenu/Yao/yetu anatatizo la afya ya akili
 
Tanzania hatuna wanasiasa kabisa. Hawa wabunge wetu, mawaziri wetu, sioni mwanasiasa pale. Anzia Ikulu, njoo kwenye Bunge, njoo kwenye baraza la mawaziri, kama kuna wanasiasa labda ni watano au sita. Wengine wote ni opportunist tu, wapo pale kutafuta fursa, na ndio maana matajiri wa Tanzania wanapatikana kupitia siasa.

Hebu niambie nani katika hawa viongozi wa CCM sijui, ACT wazalaendo nk unamwona ni mwanasiasa? Labda mtu kama Tundu Lissu nitakubali, Kafulila ndio, Zungu sawa, Lipumba yupo, Pole Pole, Mbowe ndio, Mpina kweli, Zitto sawa, na wengine wawili watatu. Lakini mtu serious unakaa unamwona Tulia, Msukuma, January Makamba, Nape, Bashe, unawaita wanasiasa? That is a joke.
Sorry mleta mada. Umeanza hii mada vizuri lakini hapa umeharibu. Sentensi ya kwanza ni batili (fallacy). Huwezi kuhitimisha hivyo kwa taifa zima la watu >60m.

Halafu hao uliowatolea mfano ni watu wachache wanaosikika kwenye media mara kwa mara kwa nafasi walizo nazo.

Kikubwa ni muhimu ujiulize kwa nini hali ni mbaya hivyo. Jibu linarejea pale pale. Tangu awali uhuru wa kufanya siasa Tanzania umekandamizwa sana. Nchi imeshikiliwa na chama dola, uongozi ni wa Rais aliye juu ya katiba na sheria (imperial president) na mwenye kauli ya mwisho juu ya masuala yote ya kitaifa (totalitarian state). Kukosoa au kupinga kauli ya Rais/dola inahesabiwa ni uhaini na inaweza kumsababishia mtu kifungo au umauti kisheria au hata nje ya sheria (extrajudicial).

Katika mazingira hayo ya uovyo wa nchi nzima, hakuna haja ya kusumbuka sana na ubora au ubovu wa wanasiasa binafsi (individuals). Haina tija. Wakiwa ovyo, wachumia tumbo, inaeleweka. Wakiwa bora, wapambanaji, inafikirisha. Kipi kifanyike kuwe na siasa za maana nchini?
 
Msigwa kwa muda mrefu sana amekuwa na msimamo mkali dhidi ya CCM, msimamo ambao ulitokana na orodha ndefu ya mambo ambayo hakuyapenda sana ndani ya CCM, pamoja na watu wenyewe wa CCM. Lakini sasa, akakorofishana na Mbowe, au tuseme akashindwa uchaguzi ndani ya Chadema na ikawa kichocheo cha badiliko kubwa kwa Msigwa tunaemfahamu.

Sasa suala la kujiuliza, au hasa la kumuuliza Msigwa ni kwamba, yale mambo ambayo hukuyapenda ndani ya CCM, au watu ambao hukuwapenda ndani ya CCM na aliona hawafai kuwa viongozi wa Tanzania, kushindwa kwake uchaguzi ndani ya Chadema, au kukorofishana kwake na Mbowe, kumeyabadilisha au kuwabadilisha watu hao na kufanya sasa yawe mazuri wawe viongozi wazuri?

Kwa mfano, kama Msigwa hakumpenda Bashe kwa uongo kwa Bunge juu ya vibali vya sukari, kukorofishana na Mbowe kunabadilisha uongo aliosema Bashe na kuufanya uwe ukweli? Au kama Msigwa hakumpenda Samia kutokana na mkataba wa bandari kwa DP World, sasa anampenda Samia na Mkataba wa DP World kwa sababu ameshindwa uchaguzi Chadema?

Msigwa anaweza kusema kuna mambo yamebadilika ghafla ndani ya Chadema ndio maana ameondoka, lakini zaidi tungependa kujua ni mambo gani yamebadilishwa ghafla ndani ya CCM na kuanza kuipenda CCM dhidi ya Chadema, au ni unafiki na umalaya wa kisiasa tu tunaoshuhudia hapa?

Ningemwelewa Msigwa kama angeondoka Chadema na kutulia nyumabani, lakini sio kwenda kwenye CCM alikowadosoa kwamuda wote huu. Kwa kufanya hivyo hastahili hata heshima ya kuitwa mchungaji katika unafiki kama huo.
Maokoto yanahusika,alipewa offer ambayo hakuweza kuikataa.1b siyo hela ndogo kwa usawa huu.
 
Ni wachache sana watakuelewa umejenga hoja ambayo imaonyesha Msigwa hakuwa akiyasema hayo toka moyoni alikuwa akiyasema kama mwanasiasa ambaye lazima aseme kitu ili asikike na wala hakuwa anamaanisha hivyo. Ni hatari sana nchi kuwa na aina hii ya wanasiasa, hawa hawatakiwi kupewa nchi au uongozi kabisa kwani hawatakaa kwamwe kumshauri raisi
 
Wan

Wanasiasa walio wengi wa Tz hilo siyo suala linalowahangaisha sana. Wao wanachoangalia siyo walichosema (maana watasema hawakueleweka vizuri/watu walielewa vibaya), bali mambo gani/ulaji gani uko mbele yao. Hili ndilo jambo muhimu kwao.
 
Msigwa kwa muda mrefu sana amekuwa na msimamo mkali dhidi ya CCM, msimamo ambao ulitokana na orodha ndefu ya mambo ambayo hakuyapenda sana ndani ya CCM, pamoja na watu wenyewe wa CCM. Lakini sasa, akakorofishana na Mbowe, au tuseme akashindwa uchaguzi ndani ya Chadema na ikawa kichocheo cha badiliko kubwa kwa Msigwa tunaemfahamu.

Sasa suala la kujiuliza, au hasa la kumuuliza Msigwa ni kwamba, yale mambo ambayo hukuyapenda ndani ya CCM, au watu ambao hukuwapenda ndani ya CCM na aliona hawafai kuwa viongozi wa Tanzania, kushindwa kwake uchaguzi ndani ya Chadema, au kukorofishana kwake na Mbowe, kumeyabadilisha au kuwabadilisha watu hao na kufanya sasa yawe mazuri wawe viongozi wazuri?

Kwa mfano, kama Msigwa hakumpenda Bashe kwa uongo kwa Bunge juu ya vibali vya sukari, kukorofishana na Mbowe kunabadilisha uongo aliosema Bashe na kuufanya uwe ukweli? Au kama Msigwa hakumpenda Samia kutokana na mkataba wa bandari kwa DP World, sasa anampenda Samia na Mkataba wa DP World kwa sababu ameshindwa uchaguzi Chadema?

Msigwa anaweza kusema kuna mambo yamebadilika ghafla ndani ya Chadema ndio maana ameondoka, lakini zaidi tungependa kujua ni mambo gani yamebadilishwa ghafla ndani ya CCM na kuanza kuipenda CCM dhidi ya Chadema, au ni unafiki na umalaya wa kisiasa tu tunaoshuhudia hapa?

Ningemwelewa Msigwa kama angeondoka Chadema na kutulia nyumabani, lakini sio kwenda kwenye CCM alikowadosoa kwamuda wote huu. Kwa kufanya hivyo hastahili hata heshima ya kuitwa mchungaji katika unafiki kama huo.
Msigwa ni mlafi na mtu asiyejua anataka nini.
 
Ma-ndumilakuwili duniani ndivyo walivyo!
msigwa sio wa kwanza wapo wengi aina yake
 
Kwa kujiunga CCM Msigwa is not principled kabisa asidanganye watu.Vipande vya Rupia at work.Kwishney
 
Sorry mleta mada. Umeanza hii mada vizuri lakini hapa umeharibu. Sentensi ya kwanza ni batili (fallacy). Huwezi kuhitimisha hivyo kwa taifa zima la watu >60m.
Aaah. Okay, basi narekebisha. Katika hawa waliojitokeza, Tanzania hatuna wanasiasa!
 
Mleta mada umeanika hoja zote za msingi kuhusu sakata la Msigwa. Kwa upande mmoja, Msigwa amejidhihirisha kuwa mtu duni pamoja na kuwa na akili kubwa. Akiwa na nafasi ndani ya CHADEMA alitandaza hoja na misimamo yake thabiti dhidi ya mishkeli kibao ya CCM na serikali yake. Alikuwa mzungumzaji mzuri sana wa kuaminika.

Lakini majuzi kapinduka ghafla na kuanza “kuanua” aliyosimama nayo. Tumeshangaa. Historia inayoelezwa kuhusu uongozi wake ndani ya CHADEMA inanipa fikra kuwa waliokuwa karibu naye siku zote walijua “ukweli” kuhusu mtu huyu. Lakini uongozi wa chama katika mahangaiko (desperation) ya kutaka kuonyesha kuwa chama kina watu wa kila namna “kilimbeba” dhidi ya washindani wake katika nafasi alizogombea.

Wapo pia watu kama kina Polepole, Kabudi, na bashiru waliokuwa magwiji wa demokrasia na utawala bora lakini ghafla wakawa watu duni wenye akili kubwa wakapiga u-turn ya nguvu na kuukumbatia ufashisti.

Wote hawa pamoja na Msigwa huwa nawaona kama wahanga wa mazingira (victims of circumstances). Kuwa mwanasiasa wa maana, mwenye msimamo thabiti katika nchi hii naamini lazima uwe “mwehu” kama Tundu Lissu. Hakuna popular support kwa wanaopambania haki za wananchi. Naamini wakuu ndani ya dola/serikali na machawa wao wanasubiri kwa hamu kubwa siku TL atakapovunjika na kulegea washerehekee kuwa hatimaye hakuna mwanasiasa wa maana Tanzania; wote wachumia tumbo tu - kama wao!
 
Sorry mleta mada. Umeanza hii mada vizuri lakini hapa umeharibu. Sentensi ya kwanza ni batili (fallacy). Huwezi kuhitimisha hivyo kwa taifa zima la watu >60m.

Halafu hao uliowatolea mfano ni watu wachache wanaosikika kwenye media mara kwa mara kwa nafasi walizo nazo.

Kikubwa ni muhimu ujiulize kwa nini hali ni mbaya hivyo. Jibu linarejea pale pale. Tangu awali uhuru wa kufanya siasa Tanzania umekandamizwa sana. Nchi imeshikiliwa na chama dola, uongozi ni wa Rais aliye juu ya katiba na sheria (imperial president) na mwenye kauli ya mwisho juu ya masuala yote ya kitaifa (totalitarian state). Kukosoa au kupinga kauli ya Rais/dola inahesabiwa ni uhaini na inaweza kumsababishia mtu kifungo au umauti kisheria au hata nje ya sheria (extrajudicial).

Katika mazingira hayo ya uovyo wa nchi nzima, hakuna haja ya kusumbuka sana na ubora au ubovu wa wanasiasa binafsi (individuals). Haina tija. Wakiwa ovyo, wachumia tumbo, inaeleweka. Wakiwa bora, wapambanaji, inafikirisha. Kipi kifanyike kuwe na siasa za maana nchini?
Anatafuta pesa za haraka na kazipata za bureee
 
Miaka mitano tena ya uhuni huu wa kisiasa? Imenishitua sana kuona eti Msigwa anaingia ukumbuni, Raisi na Makamu wa Raisi na Waziri Mkuu sijui na nani, wanaanza kuimba tuna imani na Msigwa!

Yaani viongozi kama hawa wa kitaifa wako serious wanaimba tuna imani na mtu ambaye kila mwenye akili anaona ni ndumila kuwili asie na msimamo na huyo ndio mnaimba tuna imani naye, hivi nyie ni wanasiasa serious kweli, tuwaamini kuiongoza nchi hii kama watu makini?
Kusema kweli kitenda kile kiliwadhalilisha sana wajumbe wote wa NEC pamoja na mwenyekiti wao, yaani huyu andunjje Msigwa wiki moja tu nyuma alivyokuwa Singida kwenye ziara ya Lissu alikuwa anawapaka kinyesi kabisa lakini kwa usiku mmoja tu wamekuwa na imani naye.
 
Maokoto yanahusika,alipewa offer ambayo hakuweza kuikataa.1b siyo hela ndogo kwa usawa huu.
He kumbe huyu ngedere amevuna Tsh, 1,000,000,000/- ndiyo maana kapagawa hadi kapata kigugumizi.Ila ajue zitaisha hizo na utu wake hawezi kuurudisha tena. Angekula tartiib bila kuanza kuropoka ovyo kwani kuna wafia chama hawajawahi kupata hata 10% ya hela hiyo toka kwenye chama chao.
 
Ni wachache sana watakuelewa umejenga hoja ambayo imaonyesha Msigwa hakuwa akiyasema hayo toka moyoni alikuwa akiyasema kama mwanasiasa ambaye lazima aseme kitu ili asikike na wala hakuwa anamaanisha hivyo. Ni hatari sana nchi kuwa na aina hii ya wanasiasa, hawa hawatakiwi kupewa nchi au uongozi kabisa kwani hawatakaa kwamwe kumshauri raisi
Rais leo kasema viongozi wasiwe na ndimi mbilimbili ndilo hilo la Msigwa
 
Back
Top Bottom