Maajabu ya Papa Niang dhidi ya Mwadui FC

Maajabu ya Papa Niang dhidi ya Mwadui FC

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Mshambuliaji mpya wa Simba, Papaa Niang jana alicheza dakika 45 mechi dhidi ya Mwadui FC na kuweka record ya aina yake, mchezaji huyo alifanikiwa kupiga cross moja tu, hakupiga shuti hata moja iwe off target wala on target.

Alikuwa anaogopa kukaa na mpira hata sekunde tano wakati yeye ni mshambuliaji wa mwisho. Kwakweli ni mara 100 kubaki na Maguli kuliko huyu Msenegal wa bei chee, hii ni oil chafu kutoka Senegal (Nape's voice).

Viongozi wa Simba mnaipeleka timu shimoni!
 
Mshambuliaji mpya wa simba papaa niang mdogo wa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya senegal mamadou niang jana alicheza dakika 45 mechi dhidi ya mwadui fc na kuweka record ya aina yake, mchezaji huyo alifanikiwa kupiga cross moja tu, hakupiga shuti hata moja iwe off target wala on target, alikuwa anaogopa kukaa na mpira hata sekunde tano wakati yeye ni mshambuliaji wa mwisho. kwakweli ni mara 100 kubaki na maguli kuliko huyu msenegal wa bei chee, hii ni oil chafu kutoka senegal(nape's voice). viongozi wa simba mnaipeleka timu shimoni
Nakubaliana na wewe mkuu
Ni mara 100 uwe na Maguli katika nafasi ya ushambuliaji kuliko kuwa na huyu Msenegal, hamna kitu kabisa huyu mchezaji. Usajili wa bongo magumashi tu.
 
Hivi ni kwa nini viongozi wa Simba hawataki kumludisha Kiongera, saa nyingine uongozi wetu ni kama wanakuwa wamezidiwa na ile Sigara kali maamuzi yao ni hovyo hovyo.
 
Huyu jamaa hana uhusiano wowote na Mamado Niang. Achia mbali Udugu, hata kujuana tu, hawajuani.

Simba acheni kutuhadaa mashabiki.
 
''Wabongo mnapenda mabadiliko ya haraka bila mipango'' Ndivyo tulivyo, ndio maana sishangai Taifa Stars kuendelea kuvurunda.
 
Simba bado sana
kocha yule fitness tu ndo mzuri
tactic hamna kitu
wachezaji wana kariri tu kupiga krosi

mpira wa krosi wa kiingereza haundani na mpira wa kitanzania

kulikuwa hakuna pasi zinazofika saba
washambuliaji wa kati hawapati mipira kabisa hasa beki za timu pinzani zikiwa vizuri

watawaona wachezaji wote bomu,tatizo ni kocha
 
Simba bado sana
kocha yule fitness tu ndo mzuri
tactic hamna kitu
wachezaji wana kariri tu kupiga krosi

mpira wa krosi wa kiingereza haundani na mpira wa kitanzania

kulikuwa hakuna pasi zinazofika saba
washambuliaji wa kati hawapati mipira kabisa hasa beki za timu pinzani zikiwa vizuri

watawaona wachezaji wote bomu,tatizo ni kocha

duh!! kazi ipo amekuwa kocha tena ndo sio mzuri hata kabla ya ligi kuanzaa??????
 
Back
Top Bottom