Maajabu ya Serikali ya Tanzania: Wanaopandishwa madaraja wanalipwa July hii! Wanadai malimbikizo ya misharaha miaka kibao hawalipwi

Maajabu ya Serikali ya Tanzania: Wanaopandishwa madaraja wanalipwa July hii! Wanadai malimbikizo ya misharaha miaka kibao hawalipwi

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Posts
3,436
Reaction score
7,955
Hakuna kitu kinaumiza kama kusubiria malimbikizo ambayo ni jasho la mtu kulitumikia taifa hili! Watu ni kama wanalazimishwa kukopwa bila kujua watalipwa lini!

Serikali mbona mnaonea hivyo wanaodai malimbikizo? Mnapandisha madaraja mnalipa! Ila wenye malimbikizo ya miaka wala hamlipi hii ni dhambi kubwa sana.
 
Mi naona bora msipandishwe hata hayo madaraja maana hakuna la maana mnafanya, hakuna uzalendo kwa nchi yenu mmejaa uzembe na utoro. Shame on you
Naunga mkono hoja. Kumekuwa na upandishwaji wa kisiasa zaidi katika sekta ya umma pamoja na kwamba kupandishwa vyeo watumishi siyo haki yao ya kiutumishi, isipokuwa ni hisani ya mwajiri.

Maana yake Mwajiri akiridhika kuwa mtumishi amemfanyia kazi nzuri anaweza kumpandisha cheo kama shukrani.
 
Kuna watumishi wa umma wana roho mbaya na ubinafsi sana,mmojawapo ni huyu mtoa mada!yaani watu wasipande vyeo eti kisa wewe unaidai serikali pesa ya kupanda cheo hapo awali😲!
Nashauri na wewe unyanganywe hilo daraja lako afu ndo tuanze upya😋
 
Swala la kupandishwa madaraja ni la raisi husika ila malimbikizo ya mishahara ila ni la wengi unaweza kuta raisi mwinyi anahusika kikwete na mkapa na magufuli hvyo mtu hawezi kurupuka tu ni sawa kusema mama samia anahusika na watu kufilisi hela za wastaafu wakati alikuta mambo yashavurugika tayari.
 
Mimi naona bora msipandishwe hata hayo madaraja maana hakuna la maana mnafanya, hakuna uzalendo kwa nchi yenu mmejaa uzembe na utoro. Shame on you
Uzalendo bila hela ni uchawi mkuu watumishi wa umma ni wazalendo sana sema kwasababu wanasiasa wanawatumia kuwadidimiza ili waonekane wazembe lakini wana mambo yao mengi hayapo sawa wanaishi kwa shida sana.
 
Wanasiasa wapo wangapi na wana siasa ni wangapi? huko ni kukosa akili na umoja
 
Naunga mkono hoja. Kumekuwa na upandishwaji wa kisiasa zaidi katika sekta ya umma pamoja na kwamba kupandishwa vyeo watumishi siyo haki yao ya kiutumishi, isipokuwa ni hisani ya mwajiri.

Maana yake Mwajiri akiridhika kuwa mtumishi amemfanyia kazi nzuri anaweza kumpandisha cheo kama shukrani.
Mtu anapandishwa daraja yupo maternity leave mwingine masomoni, vigezo vyenyewe ni vya hovyo mtu anasubiri miaka 3 anajua atapata hata ni mlevi na mzembe, hakuna upimaji wa wazi zaidi ya kujuana
 
Hakuna kitu kinaumiza kama kusubiria malimbikizo ambayo ni jasho la mtu kulitumikia taifa hili! Watu ni kama wanalazimishwa kukopwa bila kujua watalipwa lini!

Serikali mbona mnaonea hivyo wanaodai malimbikizo? Mnapandisha madaraja mnalipa! Ila wenye malimbikizo ya miaka wala hamlipi hii ni dhambi kubwa sana.
Pole mtumishi wa umma,
kwani malimbikizo ya madai yako ni ya tangu lini mtumishi ?🐒
 
Wanasiasa wapo wangapi na wana siasa ni wangapi? huko ni kukosa akili na umoja
Ulishawahi kuona mwanasiasa ameenda sehemu anawauliza watumishi changamoto zao kabla ya kuwawajibisha kwa mfano swala la maji DAWASA inadaiwa ni malimbikizo ya posho za wafanyakazi kwasababu asilimia kubwa pale DAWASA wanafanya kazi za kujitolea yaani vibarua hvyo wanadai pesa zao mkuu wewe unaweza ukawa na ari ya kazi kama huna pesa hakuna hata kiongozi mmoja anayewasikiliza watumishi kila mtu anawatumia kisiasa ari ya kufanya kazi unaiotoa wapi yaani mwanasiasa anakaa bungeni miaka mitano kiunua mgongo chake ni million 250+ halafu mtumishi anafanya kazi miaka 40 akistaafu anapewa million 60 what a joke mkuuu siku zote kabla ya kuhukumu jaribu kuangalia pande zote mbili watumishi sometimes na wao ni binadamu ujue sio maroboti.
 
Usingeanza kutukana na kukandia ningekusaidia upate malimbikizo yako,ila kwakuwa una roho mbaya haya baki ukiendelea kudai.
Maisha mema.
 
Hakuna kitu kinaumiza kama kusubiria malimbikizo ambayo ni jasho la mtu kulitumikia taifa hili! Watu ni kama wanalazimishwa kukopwa bila kujua watalipwa lini!

Serikali mbona mnaonea hivyo wanaodai malimbikizo? Mnapandisha madaraja mnalipa! Ila wenye malimbikizo ya miaka wala hamlipi hii ni dhambi kubwa sana.
Mkuu unapokuwa mtumishi wa umma inabidi kuwa na uelewa mpana sana kabula ya kuilaumu serikali,aliyepanda daraja mwezi wa sita,na mwengine mwezi wa saba,huyu wa mwezi wa saba hawezi dai malimbikizo ya daraja kwa kuwa hana barua ya kuthibitisha madai hayo,au wewe tayari umeshapewa barua ya kupanda cheo/daraja?

Niambie ni vielezo vipi utapeleka kwa mwajiri wako ili kuonesha ulipunjwa mshahara,kuna haja ya serikali kuanzisha somo la uelewa kwa watumishi wake.

By the way tumpe mama Samia maua yake,haiwezekani apandishe daraja watumishi ndani ya miaka mitatu tu ya utumishi wake harafu aje kulia lia kuwa kupunjwa mshara wa mwezi mmoja.

Bnafsi mwezi wa sita nilitakiwa kupanda ila sikupanda,mwezi huu ndo nimepanda ilasiwezi kulalama,maana anachokifanya mama kwetu ni zaidi ya hisani
 
Hakuna kitu kinaumiza kama kusubiria malimbikizo ambayo ni jasho la mtu kulitumikia taifa hili! Watu ni kama wanalazimishwa kukopwa bila kujua watalipwa lini!

Serikali mbona mnaonea hivyo wanaodai malimbikizo? Mnapandisha madaraja mnalipa! Ila wenye malimbikizo ya miaka wala hamlipi hii ni dhambi kubwa sana.
Acha roho mbaya wewe acha watu wapandishwe vyeo. Hivi kwa akili yako siku ukilipwa watu waandamane kupinga usilipe sio. Wewe pambania haki yako na wengine wapate stahiki zao.
 
Back
Top Bottom