Maajabu ya tairi mbovu na utajiri uliojificha ndani yake

Maajabu ya tairi mbovu na utajiri uliojificha ndani yake

Zingatia hapa tairi mbovu yaani ilishatumika, ikachakaa ama ikaharibika hivyo haifai kutumika tena kwenye magari

Hii ni fursa ambayo itawafaa sana vijana wetu wa JF wanaosaka ajira

Tairi moja mbovu ya gari kubwa ya mizigo unaweza kuinunua kwa kati ya shilingi 2000 mpaka 5000 kulingana na ubora . Zikiwa tairi 18 mpaka 20 zinatengeneza tani moja

Sasa tuchukulie kwa makisio ya juu.. Utainunua kwa shilingi 5000, lakini atakuja mchunaji ataichuna kwa ndani na kupata mipira kati ya 20 na 25 ..

Mipira ile ya kufungia mizigo kwenye baiskeli na bodaboda

Kila mpira utauza shilingi 500 Kwa jumla. Weka wastani wa mipira 24 kwa tairi sawa na elfu 12,000.. Toa 2000 ya mchunaji unabaki na elfu 10, toa elfu 5 ya manunuzi unabaki na elfu 5 kwa tairi. Zidisha mara 20 unapata laki 1 ffaida

Ukitoka hapo unapeleka tairi zako kiwanda ni na kwenda kuuza kwa kilo.. Tairi 20 zinazotengeneza tani moja utauza kwa bei ya chini kabisa Shilingi laki 2, kumbuka kule ulishapata laki 1 ya mipira na hiyo laki mbili ni yako yote usafiri ni malipo mengine

Sasa tairi 20 ulizonunua kwa laki 1
Zimekuletea faifa ya laki 1 kwenye kuchuna mipira na faida ya laki 2 kiwandani . jumla laki 3.. Hapo faida inaweza kuongezeka ukipata tairi kwa chini ya elfu 5 na ukauza zaidi ya laki 2
Hapo kwa wapambanaji ni fursa yenye kipato cha kueleweka
Sasa twende huko viwandani ushuhudie maajabu
Mahesabu haya sio mageni hapa mjini labda kwa mgeni wa jiji,hata kilimo cha matikiti tuliambiwa mahesabu kama haya(msalimie Dr.Manguruwe"
 
9bb47390-2f61-4863-81f7-8bf503a72c7b.jpeg
 
Niliwahi kufanya utafiti wa viwanda vinavyofanya tire retreading hapa Tz.
Nadhani kuna kuchanganyiwa tire mpya na retreaded kwenye maduka.
Mshana Jr nakuja PM
 
Back
Top Bottom