ndio chuo kilicholifikisha taifa hapa lilipo.mafisadi wote ni product ya udsm.wahujumu uchumi ni product ya udsm hata maprofessor wenye tamaa ya uongozi wengi ni wa udsm
Ndugu yangu mpendwa. Kama kweli wewe ni Mtanzania, nakuomba kwa moyo wangu wote utafute Kitu kingine cha kutukana na kudharau.
Mimi Highlander nimeona vyuo vingi kiasi kwa kuvitembelea, na vichache kukalia viti vyake. Nitaje W(V)its Afrika Kusini, Nairobi University, na vingine nje ya bara letu la Afrika. Sifa ya usomi bado sijaifikia, lakini sifa ya ujuzi wa kuona ninayo--tena sana tu.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni moja katika Vyuo Vikuu vizuri sana katika Bara letu, na Namshukuru sana Mungu nilipata idhini ya kusoma pale katika miaka ya karibuni. Nimewaambia watoto wangu na marafiki zangu wa karibu nikipelekwa kaburini sasa, baada ya kupitia UDSM naenda kwa amani huko roho yangu itakoenda.
Kule Fillipines walikuwapo mafisadi wawili wakiitwa Marcos. Wale walisona UDSM? Pale Cairo pametokea fisadi mmoja akiitwa HOSNI Mubaarak. Yule alisoma UDSM? Kule Marekani kuna fisadi mmoja akiitwa Oliver North alikamatwa akibwiya hela katika kashfa ile ikajulikana kwa jina la The Iran Contra Affair. Yule alisoma UDSM?
Ufisadi haufundishwi katika Chuo chochote. ukweli ni kwamba roho ya wizi wa mali ya umma au mtu yeyote mwingine ni Mama yako mzazi na baba yako ndio wanaokufundisha utotoni kwa values wanazokuonesha. Wezi wa mali ya umma katika Tanzania wametokana na cultural traits za nchi, kuanzia nyumbani, jinsi ileile wezi katika nchi nyingine walivyolelewa na culture--hasa makuzi--kutokuogopa mali ya umma. Blame the culture; not UDSM. Unataka kuniambia wahitimu wote wa Sokoine, IRDP, Mzumbe, kile chuo cha mashushushu wezi kule Kigamboni, IFM na vingine hawamo katika wezi wa mali ya umma katika nchi hii? Inawezekana kabisa wewe ni mtu mwenye bifu fulani na UDSM. Pengine ulishindwa kukidhi vigezi wakakutolea nje na sasa unatafuta kuchafua chuo kwa chuki zako binafsi.
Nimepita pale nikakuta slogan moja naipenda sana: ELIMU KWANZA! Jitahidi popote ulipo jisomee upate grade nzuri watakupokea tu--Kama si katika digrii ya kwanza, kamia kuingia katika ngazi ya Uzamili, au Uzamivu.
Sema Moyoni mwako, Elimu Kwanza utapokelewa.