Sprouts pre School
Member
- Jul 15, 2026
- 64
- 187
Hebu Fikiria mtu ambaye si Ofisa wa serikali, lakini anatembea kwa kujiamini ndani ya majengo ya Ikulu, anapokea wageni wa kimataifa, anajadiliana na wawekezaji, na kila anayekutana naye anaamini anawakilisha mamlaka ya Rais. Hicho ndicho kilichotokea nchini Nigeria, ambapo Adeniyi Adeyemi Matthew alijitambulisha kama Mkurugenzi Mkuu wa taasisi iliyoitwa Presidential Foreign Intervention Promotion Council – taasisi ambayo baadaye ilibainika haikuwahi kutambuliwa kisheria. Ni Taasisi ya Mchongo
Kwa muda, shughuli zake zilionekana kuwa za kawaida. Alifanya mikutano na wawekezaji wa nje, akatumia nyaraka zenye nembo za serikali, na akaendesha shughuli kana kwamba alikuwa afisa halali wa Ikulu. Hakukuwa na taarifa za umma kwamba alikamatwa na makachero au walinzi wa usalama wakimtambua mapema kuwa ni mlaghai. Badala yake, simulizi linaonyesha kwamba alijenga taswira ya uhalali kiasi cha kuwafanya watu wengi waamini alikuwa na mamlaka halisi. Ukweli ulianza kujitokeza baada ya taasisi za serikali kuanza kuhakiki uhalali wa PFIPC na kugundua kuwa haikuwepo katika mfumo rasmi wa serikali.
Ugunduzi huo uliishtua Nigeria. Serikali ilieleza kuwa taasisi hiyo haikuwa ya kisheria, huku Rais Bola Tinubu akiamuru uchunguzi wa kina kubaini ni kwa namna gani mtu aliweza kutumia jina la Ikulu kwa muda bila kugunduliwa mapema. Polisi walimfungulia mashtaka yanayohusisha kughushi nyaraka, kujifanya afisa wa serikali na udanganyifu, wakati yeye akiendelea kukanusha tuhuma hizo na kusema lengo lake lilikuwa kuvutia uwekezaji wa kigeni.
Lakini jambo lililowashtua zaidi Wanigeria si mtu mmoja kujifanya afisa wa serikali. Ni kile ambacho tukio hilo limefichua kuhusu mifumo ya taasisi za umma. Ikiwa mtu anaweza kujenga mamlaka kwa kutumia nyaraka za kughushi na kuendesha shughuli kwa jina la Ikulu, basi swali kubwa linabaki: je, mifumo ya uthibitishaji ilikuwa imara vya kutosha?