Maalim Aly Basaleh Sheikh Shujaa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MAALIM ALY BASALEH SHEIKH SHUJAA

Nimepata taarifa ya kifo cha Sheikh Aly Basaleh msikitini petu Masjid Nur leo baada ya Sala ya Maghrib.

Nilipofika nyumbani kitu cha kwanza nilichofanya ni kuingia Maktaba kutafuta kitabu alichoandika, ‘’Kwa Nini Waislamu Walalamika,’’ kilichotolewa na Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania.

Nimekifunua kitabu na kusoma, ‘’Yaliyomo.’’

Kitabu hiki kina mengi yanayomfaa kila Muislam kuyajua, mambo ambayo kwa hakika ni mazito kupita kiasi na si ajabu kuwa aliyekuwa na ushujaa wa kuyasema alikuwa6 marehemu Sheikh Aly Basaleh.

Hawezi mtu kuisoma dhulma iliyoelezwa katika kitabu hiki ila moyo wake utahuzunika.

Kwa lugha nyepesi sana Maalim Aly Basaleh katika kitabu hiki anawapitisha Waislam katika yote yaliyowasibu kuanzia uhuru upatikane mwaka wa 1961 na bado yanaendela hadi hivi sasa.

Katika kitabu hiki Maalim Aly Basaleh kama ilivyokuwa taaluma yake ya ualimu sheikh anasomesha kwa rejea ya vitabu vilivyoandikwa na watu maarufu wanaojua mambo mfano wa Dr. John Sivalon mwandishi wa kitabu, ‘’Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985," (1992).

Kitabu hiki kwa uzito wa yale yaliyomo kimetolewa katika soko kimya kimya kunusuru umoja wa taifa letu.

Maalim Aly Basaleh akitoka hapo katika kitabu hicho anakuingiza katika kitabu cha Aboud Jumbe, ‘’The Partner-Ship,’’ (1994).

Sheikh Aly Basaleh kwa ushahidi wa waandishi hawa wawili ambao kauli zao zinajitosheleza anaeleza hali na matatizo waliyonayo Waislam na vikwazo vinavyowakabili katika kujiletea maendeleo na kueleza wepesi waliokuwanao wenzao kusonga mbele katika maendeleo yao wakitumia nafasi zao katika serikali.

Maalim Basaleh katufanyia wema mkubwa kwa kuandika na kutuachia kitabu hiki.
Maalim Aly Basaleh kafariki katika kipindi nchi yetu imegubikwa na sakata la bandari.

Naamini Sheikh Aly Basaleh kama si maradhi kumweka kitandani hadi umauti wake asingekosa la kusema kuhusu kadhia hii na kama mwenyewe alivyopenda kusema kila alipohadhiri kuwa yeye hasemi jambo ila kwa ushahidi wa nukuu kiasi wanafunzi wake wakampa jina, ‘’Mzee wa Kunukuu.’’

Katika suala la bandari kelele nyingi zinapigwa kuhusu kinachdaiwa yamo ndani ya mkataba wa Serikali na Waarabu.

Neno, ‘’Waarabu,’’ hakijapata kupewa uzito kama linavyopewa hivi sasa katika suala la bandari.

Hata pale wanaolitumia neon hili wanapoonywa kuwa wanajipiga risasi ya mguu wenyewe kwa kutumia neno hili akili imewaruka wanashindwa kuliacha limekuwa neno muhimu kati msamiati wao wa kibaguzi.

Msome Sheikh Aly Basaleh anavyozungumza katika kitabu chake, ‘’Kwa Nini Waislamu Walalamika,’’ kuhusu mkataba wa Maelewano ya Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mabaraza ya Makanisa (Christian Council of Tanzania (CCT) na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania Episcopal Conference (TEC).

Sheikh Aly Basaleh anaandika katika kitabu hicho kuwa, ‘’Serikali ya Tanzania ilikubali kuwarejeshea Wakristo shule za sekondari na hospitali zilizotaifishwa mwaka wa 1970 na pia kuahidi kutozitaifisha tena shule na hospitali hizo au zile zitakazojengwa na makanisa kutoka kwa wahisani wa nje, na hasa serikali ya Ujerumani, kwa ajili ya kuendeleza hujuma za kijamii zinazotolewa na Makanisa.

Chini ya muafaka huo Serikali ilipaswa kutenga nafasi maalumu katika vyuo vyake vya ualimu kwa ajili ya waalimu na makanisa kwenda kusomea ualimu kwa lengo la kuimarisha ubora wa shule za Kikristo.’’

Hiki ni kipande tu katika mkataba wa Serikali na Makanisa.

Kalamu ya Maalim Aly Basaleh naisoma na kama vile namuona katika uhai wake anazungumza au namsikiliza Radio Kheri.

Kitabu hiki kina hoja, simulizi, takwimu na mengi muhimu kufahamika na wananchi.

Allah kwa mapenzi yake amemchukua Maalim Aly Basaleh katika kipindi hiki ambacho serikali ya Tanzania inashutumiwa kwa kile kinachoeleza ‘’kuridhia mkataba mbovu na kuuza bandari kwa Waarabu.

Kama hili halitoshi serikali imesimamishwa kizimbani kujitetea.

Allah kamchukua Sheikh Aly Basaleh katika majira haya kukiwa na shutuma kuwa Waarabu hawa kutoka Dubai wameingia Tanzania kwa malengo ya kuunufaisha Uislam na Waislam wa Tanzania.

Namsoma Maalim Aly Basaleh kisha najiuliza hawa wanaotoa shutuma hizi hawajui kuwa Kanisa lifaidi mabilioni ya fedha kutoka Hazina ya Taifa sasa miaka 30?

Namsoma Sheikh Aly Basaleh najiuliza hawa wanaotoa shutuma hizi wanajua kuwa Wengine hawana haya waliyonayo wao na wametulia tuli?

Ali Basaleh alikuwa mzungumzaji wangu na kila tukikutana tutakuwa na mengi ya kujadili.

Namkumbuka Maalim alipokuwa na duka lake Mtaa wa Tandamti karibu na Soko la Kariakoo nikipita mitaa ile nitampitia kumsalimu na hapo tutazungumza mengi.

Laiti Maalim Aly Basaleh angekuwa hai na tukatana wakati huu wa hili joto kali la Waarabu kuuziwa bandari na Serikali kusimamishwa kizimbani mahakamani bila shaka tungelizungumza mengi moja likiwa kwa nini Waislam hawajafikisha madai yao mahakamani kupinga mkataba wa

Serikali na Makanisa?
Hapa nimesimama kuandika.

Nimekaa nafikiria na fikra nyingi zinanipita kichwani kwangu.

Namuona kama vile sheikh yuko hai na naisikia sauti yake Maalim Aly Basaleh akinipa nasaha ya faida gani itapatikana kwetu sisi wakati kama huu kufanya jambo kubwa kama hilo?

Kama vile namuona Maalim Aly Basaleh na namsikia akiniuliza, ‘’Hebu niambie Sheikh Mohamed tija gani itapatikana?

Tutakuwa tunajenga udugu baina ya wananchi au tunaiamsha fitna iliyokuwa imelala?
Haiwi kwa kuwa wao wamefanya nasi tufanye.

Sisi Allah katusifia kasema ni watu wenye akili.’’
Maalim Aly Basaleh alikuwa mtu fasaha kwa lugha zote Kiswahili, Kiarabu na Kiingereza.

Nimejiinamia najiuliza nazungumza na nafsi yangu huku nikimkumbuka Sheikh Aly Basaleh, kuna ukimya ambao si wa kawaida kama vile Waislam hawapo.

Hali hii imeleta utulivu mkubwa nchini na imeondoa taharuki katika jamii.
Nakumbuka mengi katika kesi za Waislam Mahakamani Kisutu miaka mingi iliyopita.

Kulikuwa na kesi ya Mwembechai na kesi ya Dibagula.
Ulinzi mkali na barabara kufungwa kwa muda mrefu.

Kesi kama hiyo wakati huu hakika ingezua taharuki kubwa.

Kuwa Allah kamchukua Sheikh Aly Basaleh katika majira haya yanayohanikiza nchi yetu ni ibra tosha ya kutufanya tufikiri mengi na kumshukuru Allah kwa subra aliyotujaalia, subra iliyoleta utulivu na kudumisha amani nchini petu.

Tunakuomba Mola Wetu umsamehe dhambi zake Maalim na Sheikh wetu na umtie peponi.

Amin.


 
Inna li Llahi wa Inna Ilayhi Rajiun.

In shaa Allah awe na warithi kwa mamilioni.
 
Inawezekana neno waarabu linaweza kuwa kero kwa sababu linahusianishwa mkataba unaopigwa vita ingawa bado imeshauriwa nafasi ya kurekebisha vipengele vyenye utata.

Lakini kama mkataba usingekuwa na makandokando na ungekuwa unapigiwa chapuo na kila mtu basi waarabu wangetajwa kwa aina nyingine na wala pengine isingekuwa kero kwa wanaopata kadhia hii.

Na hata ungesikia vigelegele vya mama anaupiga mwingi.
 
Makala nzuri sana na fikirishi sana.

Mzee MS, mimi ni mfuatiliaji sana wa Makala zako na pia kiimani mimi ni muislam, lakini tatizo kubwa ninalo liona ni namna unavyoitazama historia-unaitazama historia kidini.

Tatizo kubwa la Tanzania ni Chimbuko na mwenendo wa ukoloni. Jamii za kaskazini, nyanda za juu kusini na kanda ya ziwa-kwa sababu za kijiografia ziliwafanya wazungu(kama wakoloni wetu) wakae huko na kuyaendeleza maeneo hayo kiuchumi na kielimu. Matokeo yake, wachaga, wahaya na wanyakyusa wakashika serikali and by default hawa wakawa wakristo sababu ya mzungu ni mkristo.

Hata baada ya uhuru wao walijikuta ndio wamehodhi serikali hivyo yawezekana walitumia nafasi zao kupendelea dini zao, lakini haikuwa sera rasmi ya serikali kudhulumu waislam kama ilivyokuwa kwa serikali ya Habyarimana dhidi ya watusi.

Lakini kwa kweli, Nyerere alijitahidi sana idhibiti 'jamii tawala kristo' na kuweka usekyula.
 
MOU YA JMT & CCT.

Bahati nzuri nimeisoma haya makubaliano na kumsikia Dr Slaa sababu za kuingiwa. Nia elezwa ilikuwa ni nzuri, lakini Kosa lililofanyika haukuwa Jumuishi. Makubaliano haya yalipaswa kuijumuisha BAKWATA pia ili kuleta utangamano. Lakini hebu tujiulize tunaye mlaumu ni nani? Costa Mahalu? Dr Slaa? Rugambwa?

MOU hii iliingiwa wakati Mkuu wa Usalama wa taifa, Serikali na Nchi akiwa Muislam- Alhaj Mwinyi. Sasa tuwalaumu Wakristo au tumlaumu Muislam mwenzetu aliyekuwa na nafasi ya kulirekebisha hili?
 
Hili lizee bn haya toa mashudu yaliyobakia kichwan
 
Issue ya 'Waarabu' na Bandari.

Watawala wote nchi hii wamekosolewa. Na katika kukosoa, yametumika maneno na lugha tofauti kulingana na aina ya Mtawala.

Magufuli aliitwa Msukuma. Na kuelezwa wasukuma wameiteka hii nchi na kuambiwa anaihamishia chato. Wazungu tuliwaita mabeberu. Mikataba ya hovyo mf ya Madini ilikosolewa na kuitwa ya mabeberu.

Sasa Mzee MS, unaona shida Watu wa dubai kuitwa waarabu? Tuwaite wazungu wakati ni 'waarabu'? Kwa hoja ni kuwa Mkataba unakosolewa kwa kuwa ni waarabu? Wale watu wa Barrick ni waarabu?

Kuwatetea DPW kwa sababu sisi waislam na wao ni 'waarabu', huo ni utumwa na fikra dhariri. Hawa waarabu ni mabepari hivyo ni wanyonyaji(mabeberu) kama walivyo wazungu. Bepari awe mzungu, mwarabu au mweusi, muislam, mkristo, shinto, budha, ismailia, ahmadia, sabato, mchina, mzaramo, shia au sunni, ni nyonyaji tu, ndio asili yake.
 
Brothers...
Historia ya uhuru wa Kenya haikamiliki bila Mau Mau na Wakikuyu.

Huku si kuiangalia historia hiyo kikabila.

Ndiyo ukweli wenyewe.

Historia ya uhuru wa Tanganyika haikamiliki bila kutaja mchango wa Waislam.

Huu ndiyo ukweli wenyewe.
Iko wewe unachukizwa na ukweli huu ni bahati mbaya.
 
Brothers...
Jifunze historia ya Tanganyika kwanza ndipo utaelewa mengine.
 
Brothers...
Muhimu kwanza kujifunza historia ya Tanganyika.
 
Iko wewe unachukizwa na ukweli bahati mbaya.
MS..

Mimi sichukizwi na huo 'ukweli', kinachonipa tabu ni namna unavyoperceive historia hii.

Watu wote ni lazima wawe Kabila fulani au dini fulani. So wanaposhiriki jambo fulani wanashiriki kwa sababu ya kuguswa lakini si kwa sababu ya kabila au dini zao.

Mfano, ulieleza kisa cha yule mwanaharakati wa uhuru waliomfuata nyerere kutokea pwani wakitaka kufunguliwa tawi la TANU-Jina simkumbuki. Sasa huyu hakufanya hayo sababu yeye ni muislam.

Sasa, tunaposema wamesalitiwa, maana yake kuna makubaliano ya kitaasisi na Nyerere kuwa 'sisi waislam tunapigania uhuru, ukipatikana tunataka kadha wa kadhaa kifanyike'. Kama uhuru unapatikana na serikali inaweka fursa sawa kwa wote, napata shida kuelewa dhana ya 'Waislam kuonewa'.

Pia labda unisaidie, EAMWS-TANGANYIKA ilikuwa na Utaratibu rasmi kitaasisi kupigania uhuru au ni wanajumuiya wake wao binafsi kwa utashi wao walipambana?
 
Kila kinachoandikwa na Mohamed Said hapa jukwaani lazima kiwe na chembe za udini. Lakini zaidi, ni aonyeshe malalamiko jinsi gani Waislamu wamekuwa wakinyanyaswa na kutengwa na mfumo. Kuna maswali mawili matatu hapa...
1. Wakati awamu ya 5 inawapa Waturuki kujenga SGR, kilichowapa edge ni udini au terms za mikataba? Wakati Magufuli anawakataa Wachina na proposal ya bandari ya Bagamoyo, aliwakataa kwa udini au terms za mkataba? Hata sasa tunapoongelea mchakato wa DPW na bandari zetu, kinachopingwa ni nini? Ni uislamu wa bidders au vipengele vibovu kwenye mkataba na bidders? Hapa haihitaji akili za Sheikh Basaleh au malaika, kuuaminisha umma, kwamba nyeusi ni nyeupe.
2. Basi tukubali kuwa Nyerere aliwabagua Waislamu kwenye nyanja zote, na hasa kwenye elimu, kwa kuwapendelea wakristo. Lakini tujiulize, Unguja na Pemba zimeanza kuwa na shule zao lini? Iweje kwenye matokeo ya jumla, bado shule zao kwa kiasi kikubwa hazing'ari kama za makanisa, au nyenginezo za bara? Je, kuna namna mtihani wa muislamu unasahihishwa tofauti na wa mkristo? Mlishafanya tafiti mkalinganisha utofauti wa jinsi elimu kwenye hizi kambi mbili ulivyo? Inavyotolewa? Je, leo hii tungeipa computer isahihishe mitihani ya kidato cha nne, ufaulu wa Waislamu ungepaa?
Haya tuseme tubadili historia, tuwatambue Waislamu wote waliopigania uhuru wa Tanganyika na Zanzibar, will it change anything on the ground? Itaongeza nini kwenye maisha tunayoishi? Itaongeza nini kwenye namna ninavyoishi na majirani zangu wakristo kwa waislamu? Hii nguvu ya kulalamika, endapo ingeelekezwa sehemu nyingine, kama ujenzi wa seminari bora za kiislamu, ambazo zingeshindana na za kikristo, zingekuwa zimetumika kwa faida.
 
Brothers...
Jifunze historia ya Tanganyika kwanza ndipo utaelewa mengine.
Labda uniambie nijifunze historia ambayo umeitafiti wewe.

Nimeisoma kwa kiasi kikubwa. Blog yako nimekuwa nikiisoma sana. Posts zako YouTube zote nimeziona. Nimesikiliza sana Al Marhum Ilunga, Barwan n.k.

Sina shida na historia 'ngeni' inayoelezwa, nisichokubaliana na wenye 'shule hii ya mawazo' ya historia ya uislam na uhuru, ni hitimisho lao kuhusu kupambania uhuru, kusalitiwa baada ya uhuru n.k! Ni kuipaka rangi na kujimilikisha historia.

Leo nikitafiti makabila ya kina Tewa, Waikela, Chembera, Badi kisha nikahitimisha kuwa wazaramo, wanyamwezi wamedhulumiwa uhuru, sintokuwa tofauti na hitimisho lako juu ya wapigania uhuru wenye dini ya kiislam.
 
Huyu mzee side boi,hapiganii uislamu wala waislamu hicho ni kichaka tu cha kujifichia,lengo la huyu mamruki ni kuhalibu umoja na mshikamano wa watanzania na kuvuruga amani iliyopo,tambuweni huyu mzee sio mtanganyika ni mkimbizi kutoka congo,hivyo hauoni shida wala hasara kuvuruga amani na umoja walio nao watanzania kwa kuingiza chembe za udini na chuki baina ya jamii hizi mbili,

Huyu mzee ni mamrudi twende naye taratibu kwa akili,uzuri mamlaka zinamulika vyema kabisa,hayuko mbali sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…