Uchaguzi 2020 Maalim Seif: ACT Wazalendo hatuna mpasuko lakini Membe anataka kuwaaminisha Watanzania hivyo. Adai Mzee wa Ubwabwa ni bora kuliko Mgombea wao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Habari wana jf, maalim seif ameongea na waandishi wa habari na kuzungumzia suala la Membe huku akimtolea maneno makali sana.

Nimeshindwa kushangaa, leo hii maalim seif unasema Membe katumwa? Mbona siku ya kumpitisha pale chamani kuwa mgombea uraisi ulimsifia sana? Membe unalo la kujifunza, pole sana

===



MGOMBEA urais wa chama cha ACT Wazalendo visiwani Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, ameeleza kusikitishwa kwake na tamko la jana la mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Bernard Membe, kuwa yeye ni mgombea halali wa urais, hivyo ataipeperusha bendera ya chama na ana uhakika atashinda.

Akifafanua Kuhusu suala hili, Maalim Seif amesema “Nasikitika sana kwa aliyoyazungumza Membe jana. ACT-Wazalendo kupitia mkutano mkuu wa Taifa tuliamua tunataka mabadiliko katika nchi yetu. Mkutano mkuu ukabariki tushirikiane na vyama makini kuiondoa CCM madarakani. Membe alipokuja tulimwambia uamuzi wa mkutano mkuu ni tushirikiane na vyama vingine. Tukamuuliza tukiamua kushirikiana utakubali, akasema “Naam.” Tulipoona kampeni zetu zimesuasua, tukaamua, na Membe akiwepo, tumuunge mkono Tundu Lissu.”

Ameongeza kuwa, “Mgombea wetu Bernard Membe haonekani. Ni afadhali mzee wa ubwabwa Hashim Rungwe anaonekana. Kamati ya uongozi kwa kauli moja pamoja na Membe tulikubaliana tumuunge mkono Tundu Lissu. Sio kwamba hatumpendi Membe. Mimi nam-challenge, afanye hizo kampeni zake tuone hizo kampeni ziko wapi. Nia yake ni kutaka kuwachanganya Watanzania.”

Kuhusu kuwapo kwa mpasuko ndani ya Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif amesisitiza kuwa “Hakuna mpasuko ndani ya ACT-Wazalendo. Membe anataka iaminike hivyo, lakini hakuna. Chama kimefanya uamuzi, wewe unaenda kinyume. Tukuelewe vipi? Si umeletwa ACT kwa mission (shughuli) maalum.”

PIA SOMA
= > Uchaguzi 2020 - Bernard Membe: Watanzania mkae macho na mkae chonjo. Nafunga bao la Ushindi dakika ya 89 kwenye Uchaguzi huu 2020
 
Fedha za Kampeni za Membe zimedhibitiwa Airport akitokea Dubai na wasaidizi wake wamekamatwa!

Sasa hizo kampeni atafanyaje peke yake bila ya sapoti ya secretariet ya ACT?

Lipumba mara zote za uchaguzi alikuwa anasimama kwa miguu yake na wajanja wenzie wa mjini, pesa zote za kampeni mnapeleka Znz kunajisi Mapinduzi mnataks Jasusi afanyaeje?
 
Kumbe! Basi wana ACT wote tusepe na Lissu.
 
Kwa nini usuburi mpaka uchaguzi upite? Tunataka kujua sasa ili tuamue kuwapigia kura au tusiwapigie
Wacha waendelee kutupiana maneno, tujue kama tuna wapinzani wa kweli
..ugomvi wao wasubiri baada ya uchaguzi.

..muda huu utumike kuwatafutia kura Maalim Seif, Tundu Lissu, wabunge, na madiwani wetu.
 
ACT hawana hela ya ruzuku, hela zilizopo ni michango toka kwa marafiki wa Maalimu ili washinde urais Zanzibar.
 
Jasusi is there to stay

Uchaguzi ukimalizika anaukurupusha mgogoro kama wa NCCR ya Mrema na Mabere marando 1995~2000

Siku nyingine CCM ikigombana na wanachama wake wapinzani wapunguze shobo
ACT hawana hela ya ruzuku, hela zilizopo ni michango toka kwa marafiki wa Maalimu ili washinde urais Zanzibar
 
Mimi huwa nashangaa sana mpaka leo vyama vya upinzani vinapokea wanasiasa kutoka CCM., Ni lazima upigwe mstari mwekundu hawa watu ata wakija vipi muachane nao, muachane nao ni virusi kuliko ata korona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…