Maalim Seif akiri kuwepo kwa ubaguzi wa ajira Visiwani Zanzibar unaosababishwa na tofauti za kisiasa

Well mmebakia na history tu lakini political capital ya CUF na ACT ishakufa na it's clear now kuwa opposition ipo moja tu. Na hata Mbowe akiamua kulift suspensions ya wawakilishi, watawaacha mbali sana in numbers. Losers mtabakia kiwa losers tu.

Btw hakukuwahi kuwa na chama cha upinzani Tanzania kilichopata walau 2 million votes in 3 consecutive elections kwa tume hii hii ya wizi. Meaning vyama vingine vyote vya msimu nje ya CHADEMA.
 
So what kama mlikua wa kwanza? Hoja ya ajabu kabisa hii. Kwanini hausemi Mbowe ndio KUB wa kwanza kuwa na wabunge 70+ wa chama chake?
Ama CUF mlikua wapi miaka yote mkashindwa kufikisha hiyo idadi?

Why usiseme CHADEMA ndio opposition ya kwanza kupata Halmashauri zaidi ya 20? Ama CUF mlikua wapi tokea vyama vingi vinaanza mnazidiwa na chama cha ''juzi''?

History masters my foot
 
Unachanganya mambo mkuu wewe unajibu in generally kumbuka mimi naongelea kwa upande wa Zanzibar haijawahi tokea Zanzibar opposition ikaongozwa ni chadema ila Tanganika tayari mara kadhaa CUF imekuwa ahead kuliko hiyo chadema ambayo ilikuja kuwa introduced baadae baada Maalim na wenzake kuanzisha chama cha cha Wananchi CUF na kama utakumbuka vizuri ni CUF peke yake ndio kwa mara ya kwanza wamekuwa na kambi ya upinzani katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tena alikuwa mwanamke akitokea pemba ambayo sasa waonyesha wazi kuidharau.

Theory yako kwamba maalim alifeli 2010-15 kwa SUK sawa, lakini kumbuka muda mfupi maalim kuingia kwenye SUK mara hii tayari tija imeanza kuonekana na kupatikana kwa wazanzibari na wazanzibari wenyewe wanasema sasa mambo sawa ni nyinyi watanganyika tu munaoishi bara chini ya Magufuli ndio munachukia hivyo hoja yako hii kwa wazanzibar it is good for nothing., maalim seif alikuwa analia na ubaguzi, alikuwa analia kwa watu kuumizwa kwenye haki zao za msingi, maalim alikuwa analia kwenye ajira, maalim alikuwa analia maendeleo makubwa kupelekwa unguja sasa haya yameonekana kukaa sawa automatically pamoja na kwamba maalim kaporwa ushindi mara kadhaa na dola lakini hakuwa na cha kufanya kama ambavyo Tundu lissu hakuwa na la kufanya huko Tanganyika ingawa alikuwa anapiga kelele kila kona hatakubali kuibiwa, hatakubali kuibiwa, hatakubali kuibiwa ingawa huko Tanganyika kama unavyodai kwamba muna wapiga kura zaidi ya milioni 28 lakini nothing you have done so far.,

Chadema kuna mpasuko mkubwa ata icho chama cha Wananchi CUF kilikuwa na afadhali by that time, ukitoa hao kina Halima mdee na wenzake, Makamo mwenyekiti wa Chadema Kule Zanzibar ni CCM na alikuwa akipigia kampeni wagombea wa CCM kwenye uchaguzi uliopita, yeye binafsi hakuwasikiliza viongozi wake kutaka kura za rais apigiwe maalim seif yeye akipiga kampeni ili awe rais yeye au angalau apate aslimia 5% ateuliwe uwaziri na serikali ya CCM Zanzibar, fomu yake ya kugombea urais zanzibar ililipiwa ni mgombea ubunge kupitia chama CCM, Kina Mbowe walipewa taarifa lakini hawakuwa na cha kufanya na hivi naandika bado huyu anakaa meza moja na Mbowe wakifanya maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA., Na sasa alikuwa akisema wazi wazi mimi Chadema wakinifukuza CCM watanaipa Ajira sina wasiwasi., wewe kwa kiasi hiki unataka mpasuko wa kiwango kipi tena CHADEMA???.,

Kama bara muna kura za kutosha na niza kuzoa tu kwa vile munaungwa mkono Mikoa mingi na asilimia kubwa ya Watanzania kwanini mumeshindwa kulinda haki yenu ya wapiga kura milioni 28., na kutaka watu laki 3 Zanzibar pamoja na maalim seif wasimame kuwatetea nyinyi huko Tanganyika., kama muna wapiga kura milioni 28 onyesheni mfano wa kudai haki zenu mulizoporwa kwenye uchaguzi halafu na Zanzibar wenye watu laki 3 watafuatia.

Mliitwa kwenye maandamo hamukutoka ata watu 3 kwenye milioni 28., so what?
 
Hoja yako ni nini hapa? Na cdm imeingiaje hapa?
CHADEMA mnajifanya top kwenye upinzani wakati sasa mnashindwa ata kulinda haki zenu chini ya wapiga kura wenu milioni 28 mnao dai walikupigieni kura 2020.,
 
Wabunge 70 kwenye wapiga kura milioni 28 munaodai walikupigieni kura kuna tofauti gani ya wabunge 23 kutoka Zanzibar kwenye wapiga kura laki 3??
 
Angeweka mgombea urais Zanzibar basi ili aje awe rais Zanzibar kwanini mlimpigia kura maalim seif
 
Chadema mnajifanya top kwenye upinzani wakati sasa mnashindwa ata kulinda haki zenu chini ya wapiga kura wenu milioni 28 mnao dai walikupigieni kura 2020.,

Honestly nashindwa kuona hoja yako ni ipi hapa, sana sana naona unataka kuleta ubishani wa kitoto.
 
Mwambieni huo mfumo upo Tanzania bara kwenye ajira za ualimi lakini Cha kushangaza wanaoajiriwa NI UVCCM na waliohonga pesa huko TAMISEMI
 
wabunge 70 kwenye wapiga kura milioni 28 munaodai walikupigieni kura kuna tofauti gani ya wabunge 23 kutoka Zanzibar kwenye wapiga kura laki 3??
Unafurahisha sana.... Nyie majimbo yenu yana wapiga kura elfu 5 mpaka elfu 10 maximum. Ila jimbo moja tu la Kibamba au Ubungu lina kura mpaka laki 2 sasa tukienda kwa proportion unadhani ACT ingekua na wabunge wangapi kma kila jimbo zenji liwe na kura kuanzia elfu 50!!

No wonder licha ya kuporwa majimbo yote ila wamepata viti 20!! Just imagine. Sababu cumulative number ya kura zao ni mara 100 ya mlizopata ACT. Na ndio maana hamjaambulia hata kiti kimoja maalum sababu kura laki 3 hazina lolote mbele ya pool ya kura million 28 za bara!!

Kajifunze hesabu kijana
 
Angeweka mgombea urais zanzibar basi ili aje awe rais Zanzibar kwanini mlimpigia kura maalim seif
Kura laki 3 pekee haikua worth it !! Afterall akishinda kawe na mbagala anazidi kura zote za ACT Zenji ssa Why msuguano kwa kura kiduchu hivo.

So ni bora alliance tu, ila ingekua zenji ina kura say million 5 trust me hakuna angewaachia zote hizo. Afterall ACT haina uwezo wa kushinda jimbo lolote bara kama CHADEMA wakisimamisha mgombea so nyie mliihitaji zaidi CHADEMA kuliko wao afterall hawakuwa na chakupoteza kisa kura laki 3!!

Come on
 
Naona umekaziaaaa upande wa kisiasa na kidin bado Sana kma kupanga nyumba kaz kwa christian
Wazanzibar waanze kujikomboa kifikra.wanamkumbatia mtu ambaye mawazo yake ni mgando.wapemba amkeni na kuweni macho na huyo mtu.
 
Hilo neno waache waseme wazanzibari wenyewe sio wewe Mtanganyika, kwanini munawashwa na pilipili musioila?
Ndio mana Watanganyika munafeli sana Tundu Lissu yuko ulaya anawaongoza kwa clip za Yotube
Wazanzibari wamefeli moja kwa moja na wamebaki kuchapa maneno tu
 
1.Na shida yako inaanzia hapa. Unataka kuseparate Zanzibar na Tanganyika. Ni hivi CHADEMA ipo Tanzania na ACT ipo Tanzania so vinapaswa vigombee nchi ya Tanzania hakuna chama ambacho kimepewa hati ya kuwa zanzibar pekee. So tuki judge performance ya ACT tutafika hadi Geita na Mpanda hatuwezi ishia wete alafu tukawasifia tu.

2. Mkuu hujajibu swali kama ilifeli 2010-15 unadhani mtafika 2025 mkiwa intact? Je CCM ya 2010 imebadilika au ni ile ile? Maana mnavyoisifia hapa ni kana kwamba sahivi imekua fair kuliko chaguzi zilizopita!! This is so weird

3. Huo mpasuko CHADEMA ukwapi? Wa Issa Mohammed ndio utakua mpasuko? Let's be serious.... Yule kawekwa pale kutimiza tu masharti ya muungano kma tu Mama Samia ila haimaanishi akitoka leo hii CHADEMA itatetereka. Mpasuko wa CUF ulikiua kabisa ila imagine Dk.Slaa, Dk. Mashinji, Lwakatare, Zitto hao wote walitoka ila chama ndio kwanza kimeimarika ndio sembuse kina Mdee. Get real. Hoja ni kwamba kimejengwa kitaasisi ila nyie ni individuals tu ndio maana leo Seif akihamia CCM wote mtamfuata. Sasa hiko ni chama au kijiwe?
 
Hiyo ACT Wazalendo iko mguu moja ndani moja nje.Likafu limeingia migogoro wakashindwa kulinusuru.
 
Hilo swali la pili akikujibu nitag
 
Kama Makamo Mwenyekiti wa Chama kukisaliti chama chake sio mpasuko sasa mimi bora nifunge mjadala, nyinyi watu ni " hardheaded"

Chadema ata iwe inawakilisha nchi 3 usajili wake, kwa Zanzibar chadema haiwezi kuwa na nguvu yeyote forever, ni afadhali kwa hicho chama cha CUF kiliwahi kuwa na Wabunge wa JMT wapato 12, mpaka leo Chadema zanzibar haijawahi kuwa na mbunge wa kuchaguliwa ata diwani haijawahi kutokea. Bado ACT na CUF ndio vyama vya upinzani vinavyowakilisha zaidi nchi 2 huko Tanganyika na kule Zanzibar. Wewe fanya tathmini utagundua.

Ikiwa Wazanzibari wenyewe wako kimya na wanaendelea maisha yao kule vizuri kwa serikali yao ya Kitaifa wewe mtanganyika unaumia nini? Zanzibar ndio kitovu cha siasa ya upinzani Tanzania na ina watu more intelligent then Tanganyika waache wenyewe wakiona SUK haifai watasema tu.,

Kwanini uko kimya na idadi yenu ya wapiga kura milioni 28 lakini mumeibiwa uchaguzi?
 
How many times CUF chini ya Mallim seif imekuwa ikishinda majimbo huko kwenu unyamwezini? 2015 wabunge 12 wa kuchaguliwa

Kama zanzibar ina wapiga kura laki 3 na hamna haja nazo kwanini kule zanzibar muna matawi na ofisi na viongozi mpaka Makamo mwenyekiti wa chama anatokea kule na mnawalipa mishahara minono? kwanini?? Are you sure huna haja ya kura laki 3? Haingii akilini
 
Idadi ya watu haiwezi kumata mkuu., muhimu ni average ya wakaazi wa nchi husika, ivi waweza linganisha Tanzania na Marekani, Algeria au China hii haina uhusiano wowote, cha msingi ni namba ya watu wanaoishi katika hilo eneo/nchi.

Mbunge anaewakilisha watu elfu 5 kwenye jimbo zanzibar ni sawa na mbunge anaewakilisha watu 15,000 kule unyamwezini bara, au umewahi sikia Ndugai analipa mishahara tofauti pale bungeni? hii huwezi kulaumu ndio maumbile ya Mungu alivyojaalia hakutuumba idadi sawa ya watu kila nchi na eneo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…