Kuelekea siku ya Uchaguzi Mkuu, Mgombea Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema watasimama kwa pamoja kulinda ushindi wao
Amesema, " Sisi viongozi wa ACT-Wazalendo tunauhakikishia umma wa Zanzibar, Tanzania na dunia kwa ujumla kuwa pamoja na vitimbi vyote vinavyofanywa na ZEC na Vyombo vya Dola, tutakuwa bega kwa bega na wananchi wenzetu kuvishinda vyote"
Amesisitiza kuwa, safari hii hakuna kugomea Uchaguzi pamoja na kuwepo na maswali mengi ambayo hayana majibu kutoka Tume ya Uchaguzi