Zanzibar 2020 Maalim Seif: Huu ni mwaka wa mabadiliko, hakuna la kutuzuia

Zanzibar 2020 Maalim Seif: Huu ni mwaka wa mabadiliko, hakuna la kutuzuia

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Kuelekea siku ya Uchaguzi Mkuu, Mgombea Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema watasimama kwa pamoja kulinda ushindi wao

Amesema, " Sisi viongozi wa ACT-Wazalendo tunauhakikishia umma wa Zanzibar, Tanzania na dunia kwa ujumla kuwa pamoja na vitimbi vyote vinavyofanywa na ZEC na Vyombo vya Dola, tutakuwa bega kwa bega na wananchi wenzetu kuvishinda vyote"

Amesisitiza kuwa, safari hii hakuna kugomea Uchaguzi pamoja na kuwepo na maswali mengi ambayo hayana majibu kutoka Tume ya Uchaguzi
 
Hakika na iwe hivyo, AMINA..!

Hata YESU KRISTO angekata tamaa tu ktk vita ya kuukomboa ulimwengu huu na kutukomboa sisi wana wa Adamu toka mikononi mwa mwovu shetani, maana yake mpaka leo hii na sasa hivi, shetani angekuwa ndiye mmiliki mwizi wa uumbaji wa Mungu Yehova pamoja na sisi wenyewe wanadamu tungekuwa chini ya utawala wake..

Lakini mpapa sasa tu huru kwa sababu Yesu Kristo ametushindia KIFO na MAUTI, yu HAI milele na milele..

Kwa hiyo, anatufundisha kuwa, lolote la haki tunalopigania, ni kosa kubwa na ni marufuku kabisa kukata tamaa bila kujali utalipata wakati gani..

Ukirudi nyuma na kukata tamaa maana yake umeamua kumpa ushindi shetani..

Mungu yupo pamoja na WATANGANYIKA na WAZANZIBARI kwa sababu hiyo, TUMESHASHINDA...!!
 
"JINO kwa JINO wakipiga kura tarehe27 na sisi tunapiga wazipige tarehe28 na sisi tunapiga" Maalim Seif
 
"Majeshi na Mizinga haijawahi kuziiba Nguvu ya Umma Ndugu zetu wa Visiwani wameshatoa "Shahada" Sheikh Ponda Issa Ponda
 
CHADEMA tunafunga Kampeni za Uchaguzi Zanzibar kwa Kaswida Muruwaa.

Haki imekuwa kitu kigumu sana kupatikana tokea CCM. Wanataka kutulazimisha kuwa tunawapenda.

Maajabu ya Firauni!
 
Kuelekea siku ya Uchaguzi Mkuu, Mgombea Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema watasimama kwa pamoja kulinda ushindi wao

Amesema, " Sisi viongozi wa ACT-Wazalendo tunauhakikishia umma wa Zanzibar, Tanzania na dunia kwa ujumla kuwa pamoja na vitimbi vyote vinavyofanywa na ZEC na Vyombo vya Dola, tutakuwa bega kwa bega na wananchi wenzetu kuvishinda vyote"

Amesisitiza kuwa, safari hii hakuna kugomea Uchaguzi pamoja na kuwepo na maswali mengi ambayo hayana majibu kutoka Tume ya Uchaguzi
CCM safari hii hawana pa kutokea. Wana hali mbaya sana kwa kweli, hadi wanatia huruma.
 
Back
Top Bottom