Maalim Seif, jembe la Zanzibar

Usitufokee jombi. Kila mtu anaufahamu wake.

Ndipo dhana ya kukubali kutokubaliana inapokuja.

Kama tunavyotambua uwepo wao hata walio mashimoni.
Ni kwasababu unaemuongelea humfahamu, unamjua kwa jina tu!
 
Unafiki Mkuu ni kitu kibaya sana.
 
Ni kwa sababu unadhani kuwa na hati miliki ya kumfahamu. Au wewe ni mkewe?
Huko unakokwenda ni mbali sana, naona umeingia wivu basi tufanye wewe ndio mkewe! Vipi umeridhika? Au umekasirika kuwa nimemuongelea vibaya basha wako?
 
Unafiki Mkuu ni kitu kibaya sana.

Mkuu ninakusoma kama nilivyomsoma bwana kunguru :



kwenye uzi huu:


Kukubali kutokubaliana ni mwanzo mkubwa sana wa kheri.
 
Reactions: BAK
Mkuu utaona rangi za Maalim za kuweka mbele maslahi yake badala ya yale ya Nchi na kuikana kauli yake. Hana jipya huyu zaidi ya kutunisha bank accounts zake.
 
Mkuu utaona rangi za Maalim za kuweka mbele maslahi yake badala ya yale ya Nchi na kuikana kauli yake. Hana jipya huyu zaidi ya kutunisha bank accounts zake.

Mkuu ninakuelewa kuumia kwako. Bila shaka wengi wetu ni hivyo hivyo. Tumpe muda. Muda huwa mwalimu mzuri. Kuisaliti Zanzibar bado namwona kuwa mtu wa mwisho kufanya hivyo.

Nisiache kukumbusha wale wenye kile chama chenyewe huwezi kuwaona hapa.

Kumbuka wanataka kutuona tumenyong'onyea. Wanapotuona tupo ngangari kinoma, wanaumia sana!
 
Reactions: BAK
Historia yake huyu Mkuu kwenye kusimamia maslahi ya Nchi ina mushkeli ndiyo sababu sitegemei abadilike na kapewa masharti ya kulinda wadhifa wake mpya, vinginevyo wanamtosa. Kama angekuwa si msaliti angeweka hadharani malengo yake kwa miaka hii mitano wakati akiwa meza moja na wauaji. Ukweli ni kwamba hana lengo hata moja zaidi ya kuufurahia UNGUNGE.
Mkuu ninakuelewa kuumia kwako. Bila shaka wengi wetu ni hivyo hivyo. Tumpe muda. Muda huwa mwalimu mzuri. Kuisaliti Zanzibar bado namwona kuwa mtu wa mwisho kufanya hivyo.
 

Mkuu maoni yako nayaona na nakuelewa.

Hata hivyo usisahau kuna uwekazaji mkubwa sana unawekwa ku tarnish efforts zozote za ukombozi wa hii nchi.

Ndiyo maana kuna hadi hao wa buku 7.

Kiwango ambacho wangependa kumchafua Maalim, Lissu na labda hata wewe hapo wanakijua wenyewe. Kwa ufupi watajaribu na watafanya kila kitu.

Wanapoendelea na juhudi hizo usishangae likarushwa dongo kuwa BAK ni TISS. Mbona hata Lissu wameshajaribu hayo yakadunda?

Ninadhani ndani ya magumu yaliyopo na bila ya kupendelea upande wowote mizani ingali inalala upande wa Maalim kuwa ni jembe unless proven otherwise and beyond reasonable doubts.

Hawa jamaa wanapigika na tulikuwa karibu sana na hapo. Tusisambaratishiwe hapa.

Tukubali kutokukubaliana.

Ninaamini mtu wa mwisho kuisaliti Zanzibar atakuwa Maalim. Huyu jamaa kapambana mkuu na sote tuna mengi ya kujifunza kwake.
 
Reactions: BAK
Kama ulichoandika hapa ndio dhana ya Seif kujiunga SUK, basi ki mantiki huo muunganiko wa ACT na CCM kwenye hiyo serikali unakosa maana, kwasababu inaonekana wazi hawakujiunga kwa utashi wao bali kwa uoga wa matendo ya kinyama waliyofanyiwa viongozi na wafuasi wao na jeshi la polisi.

Hivyo bado sioni sababu ya maana toka kwako kwanini umuite jasiri mtu alie surrender na kujiunga na waonevu, huyo kwangu ni muoga.
 
Huyo ndio basi tena , yeye na Zitto they are politically finished like Lipumba , nobody could listen to them again .
Nikuonyeshe kitu kiduchu tu kwamba maalim ni jembe kweli kweli., kama maalim seif kuingia SUK kakosea sana akina Lipumba, Hamad Rashid na wenzake ambao waliisaliti CUF kipindi kile sasaiv kwa hatua hii ya maalim seif wangelikwisha kuja juu sanaa yaani sanaa lakini ukimya wao ni wazi kwamba wao ni big looser, big looser, waliitegemea ccm kuwa ndio itakuwa baba yao na mama yao sasa ona walipoangukia, it is terrible.

Maalim seif ameingia SUK na kujiunga kwenye serikali ya kidhalim sawa, lakini angalia benefits, Wazanzibar sasa wataishi bila ubaguzi kwa mpemba na muunguja, chochote cha maendeleo kitakuwa sawia hakutakuwa na ubaguzi wa kimaendeleo, ajira, vitambulisho, lakini tetesi zinasema kwamba hata wale masheikh wa uamsho wamehamishwa kule bara sasa wapo kwenye ardhi ya nchi ya Zanzibar, zoote hizi ni juhudi za maalim seif kukubali kuingia SUK lakini kama haitoshi maalim seif atapata uteuzi pia kwa watu wake ambao watakuwa ndani ya serikali.

Mwisho Ivi tuseme kwa mfano Magufuli akatangaza kwamba anataka kuunda serikali ya Kitaifa Kule Tanganyika achague mawaziri kutoka Chadema labda na members wa Bunge unafkiri fursa hii ingetokea Chadema wangeiacha?? Nadhani wangekubali tu kuwemo ndani ya serikali labda wangehisi ingewepesisha ata kuweza kudai hiyo tume huru na baadhi ya shida shida zenye mkwamo
 
Mkuu hakuwezi kuwa na ukombozi katika Nchi iliyojaa DHULUMA kila kona. Na watu wengine kama akina Zitto wanaiona dhuluma hiyo lakini wanaamua kuikumbatia baada ya kununuliwa. HAKI ndiyo msingi mkubwa wa ukombozi na siyo siri kwamba Nchi yetu HAKI inazidi kupotea siku hadi siku tena kwa Watanzania walio wengi tu Wafanyakazi, Wakulima, Wafanyabiashara, Wastaafu n.k.
 
Kuna msemo unasema kuwa kila habari ya jambo ina pande mbili. Sasa sijui mwenzangu kwanza una umri gani lakini nataka kukumbusha tu kuwa wengine tunavyomjua Seif sharif si hivyo mnavyomjua nyinyi wengine. Nitajaribu kukueleza kwa ufupi tu lakini kwanza, naomba niweke bayana kuwa mimi si mwanachama wa chama chechote kila na wala sitaraji hata siku moja ya maisha yangu kujiunga na chama chechote kile Tanzania.

Naam, turudi kuhusu Seif Sharif. Seif Sharif sio kweli kuwa anaipigania zanzibar, seif sharif anajipigania manufaa yake mwenyewe toka ujanani kwake.

Seif aliwaendea kinyume akina aboud jumbe na wenzake pale walipofunga safari kwenda kumuona nyerere na kudai kuwepo kwa serikali tatu. Aboud jumbe, seif sharif na wenzake wote walikwenda kumuona nyerere kwa pamoja wakiamini madai yao ni kwa manufaa ya zanzibar. Matokeo yake Seif sharif aliwaendea kinyume wenzake, mara tu nyerere alimpomuahidi kuwa atampa urais wa zanzibar.

Seif sharif aliwaendea kinyume CCM na nyerere baada ya kuona kuwa nyerere hatotimiza ahadai yake ya kumpa urais yeye, pale alipopewa urais Abdulwakili baada ya ali hassan kuwa rais wa tanzania. Alianzisha manyago mpaka kufikia kufukuzwa ccm.

Ubaguzi na chuki baina ya wapemba na waunguja ilikuja juu zaidi wakati seif sharif alipokuwa kwanza waziri wa elimu na baadae waziri kiongozi. Tension ya juu sana ilikuwa juu ya nafasi za masomo nje ya nchi pamoja na nafasi za kazi kwa watu wa pemba. Jambo hili lilikuwa kama kutia petroli katika moto wakati wa utawala wa abdulwakili, mtu ambae alikuwa ni mbaguzi sana tu. Seif sharif alilijua hili na akaona hii ndio itakuwa advantage yake ya kumuondoa abdulwakil na kupata urais. Kwa bahati mbaya au nzuri gambel yake haikufanikiwa.

Sisemi mengine ila ukumbuke tu kuwa mara ya kwanza alipokubali kuwa makamo wa rais kuna watu tele walipoteza mali, maisha na hata ndoa zao katika kuhakikisha kuwa CUF inaingia madarakani lakini aliwaendea kinyume na kukubali kuwa makamo wa rais kwa manufaa yake mwenyewe na sio manufaa ya wanachama wake.

Mwaka huu amefanya yale yale tena, kuna watu tele wamepoteza maisha yao tena wengine ni viongozi au walikuwa karibu na viongozi wa ACT kwa sababu ya kutaka CCM itoke madarani na baada ya kualikwa kuchukua umakamo wa rais, seif sharif kakubali tena. Kasahau waliopigwa, waliouawa na walioharibiwa mali zao, almuradi yeye ni makamo wa rais,

Kwa hayo tu mimi sioni kama seif anapigania haki za zanzibar au za wazanzibari.
 
Seif ndiye huwa anaharibu pindi Zanzibar inapokuwa kwenye junction nzuri ya kujinasua kutoka kwenye makucha ya Tanganyika.
Alimsaliti Jumbe kwa kumsnitch kwa Nyerere pindi Jumbe alipokuwa anataka kuleta ishu za serikali serikali tatu ambapo Zanzibar ingekuwa huru zaidi
 
πŸ™πŸ½πŸ‘πŸ½
 

Maalim kaiweka ACT na kina Zitto kwenye picha. Ashukuriwe Maalim kwa mengi.

Hata hivyo kila siku ni muhimu kupalilia umoja badala ya utengano.

Pamoja na yote kama ulivyo wewe, mimi na yule tunahitajika sote kwenye ukombozi wa nchi hii.

Maridhiano kama yaitiwavyo na kamanda Mbowe na tukayaweke kwa vitendo baina yetu na hata baina ya vyama.

Palikuwa na hili mkuu:



Tokea hapa:


Maridhiano bandugu!
 
πŸ™πŸ½πŸ‘πŸ½
 

Naam kaiweka rasmi ACT kwenye picha ya wachumia tumbo na wasaliti wa upinzani Nchini.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…