Mabibi na mabwana si busara sana kuukimbia ukweli. Ukweli ni mchungu na msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
Au nasema uongo ndugu zangu?
Kumekuwa na mengi kuhusu ACT na Maalim Seif hasa baada ya kujiunga SUK.
Ufuatao ndiyo ulio ukweli kuhusiana na jembe hili la Zanzibar.
Maalim Seif kaipigania Zanzibar maisha yake yote. Angali anapigana na ataendelea inshallah (mola apishilie mbali) hadi kifo kitakapo mtenga.
Kuipigania kwake Zanzibar ndipo kunakompa hii credibility au kupendwa aliko nako. Ni umaarufu huo ambao pia ndiyo iliyo sababu kuu ya yeye kuibiwa kura na mahasimu wake kila uchao.
Alipo Seif wapo!
Alikuwa CUF yuko ACT hata akienda TADEA au wapi watakuwa naye huko.
Zanzibar ni kipaumbele chake. Si Bara. "Mtu kwao" na "mcheza kwao hutunzwa."
Akiitisha Seif hata leo kule Zanzibar kitanuka. Tofauti kubwa sana ya kule na Bara. Huyu gwiji ana msingi uliojichimbia barabara chini ya ardhi.
Pana tofauti kubwa ya Maalim Seif kama binadamu na ACT kama chama. Huu nao ni ukweli mchungu. ACT ni chama imara ushukuriwe uwepo wa Maalim. ACT ni butu kama CUF bila Maalim. Profesa anaweza kuuthibitisha ukweli huu.
Maalim ni mpambanaji mzoefu. Huyu ana mbinu na uwezo wa mapambano kuliko majenerali wengi. Kumbeza Maalim ni kukosa kumtambua vyema wala kutambua agenda yake iliyokuu.
Kumhusisha Maalim na ukosefu wa haki kule Kagera au Rukwa ni kutojitendea haki sisi wenyewe.
Mambo ya Ngoswe huachiwa Ngoswe mwenyewe!
Kila mtu na apambane na hali yake. Maalim anapambania Zanzibar na anaowapigania wamempa ridhaa hiyo.
Kwenye hili si CCM wala awaye yote Bara anaweza kujidhania kashinda au kashindwa au hata kasalitiwa. Busara ni kukubali kutokubaliana.
Udumu Maalim Seif jembe la ukweli la Wazanzibari!
Kuna msemo unasema kuwa kila habari ya jambo ina pande mbili. Sasa sijui mwenzangu kwanza una umri gani lakini nataka kukumbusha tu kuwa wengine tunavyomjua Seif sharif si hivyo mnavyomjua nyinyi wengine. Nitajaribu kukueleza kwa ufupi tu lakini kwanza, naomba niweke bayana kuwa mimi si mwanachama wa chama chechote kila na wala sitaraji hata siku moja ya maisha yangu kujiunga na chama chechote kile Tanzania.
Naam, turudi kuhusu Seif Sharif. Seif Sharif sio kweli kuwa anaipigania zanzibar, seif sharif anajipigania manufaa yake mwenyewe toka ujanani kwake.
Seif aliwaendea kinyume akina aboud jumbe na wenzake pale walipofunga safari kwenda kumuona nyerere na kudai kuwepo kwa serikali tatu. Aboud jumbe, seif sharif na wenzake wote walikwenda kumuona nyerere kwa pamoja wakiamini madai yao ni kwa manufaa ya zanzibar. Matokeo yake Seif sharif aliwaendea kinyume wenzake, mara tu nyerere alimpomuahidi kuwa atampa urais wa zanzibar.
Seif sharif aliwaendea kinyume CCM na nyerere baada ya kuona kuwa nyerere hatotimiza ahadai yake ya kumpa urais yeye, pale alipopewa urais Abdulwakili baada ya ali hassan kuwa rais wa tanzania. Alianzisha manyago mpaka kufikia kufukuzwa ccm.
Ubaguzi na chuki baina ya wapemba na waunguja ilikuja juu zaidi wakati seif sharif alipokuwa kwanza waziri wa elimu na baadae waziri kiongozi. Tension ya juu sana ilikuwa juu ya nafasi za masomo nje ya nchi pamoja na nafasi za kazi kwa watu wa pemba. Jambo hili lilikuwa kama kutia petroli katika moto wakati wa utawala wa abdulwakili, mtu ambae alikuwa ni mbaguzi sana tu. Seif sharif alilijua hili na akaona hii ndio itakuwa advantage yake ya kumuondoa abdulwakil na kupata urais. Kwa bahati mbaya au nzuri gambel yake haikufanikiwa.
Sisemi mengine ila ukumbuke tu kuwa mara ya kwanza alipokubali kuwa makamo wa rais kuna watu tele walipoteza mali, maisha na hata ndoa zao katika kuhakikisha kuwa CUF inaingia madarakani lakini aliwaendea kinyume na kukubali kuwa makamo wa rais kwa manufaa yake mwenyewe na sio manufaa ya wanachama wake.
Mwaka huu amefanya yale yale tena, kuna watu tele wamepoteza maisha yao tena wengine ni viongozi au walikuwa karibu na viongozi wa ACT kwa sababu ya kutaka CCM itoke madarani na baada ya kualikwa kuchukua umakamo wa rais, seif sharif kakubali tena. Kasahau waliopigwa, waliouawa na walioharibiwa mali zao, almuradi yeye ni makamo wa rais,
Kwa hayo tu mimi sioni kama seif anapigania haki za zanzibar au za wazanzibari.