Maalim Seif: Misimamo ya Kisiasa isitumike kuwafarakanisha Wananchi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Seif Sharif Hamad amesema misimamo ya vyama vya siasa isitumike kusababisha mifarakano na kuwagawa wananchi wa Zanzibar.

Amesema jamii nyingi zimefarakana na kutengana kwa sababu ya misimamo ya kisiasa na amewataka wananchi wabadilike na waendane na kasi ya Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais Dk Hussein Mwinyi katika kuwaunganisha wananchi.

Soma, Pia: Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan: Hadi sasa sijaona dalili yoyote ya utashi wa kuwepo kwa maridhiano ya kisiasa nchini

Maalim Seif ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini B, Bumbwini, Unguja akiwa katika ziara za kuhimiza mshikamano wa maridhiano ya kisiasa visiwani hapa.
 
Ukisikia kuchanganyikiwa uzeeni, ndio huko sasa. Juzi tu hapa liliingiza raia mtaani kwasababu ya itikadi ya kichama na kisiasa, leo linageuka eti misimamo ya kisiasa isitumike kufarakanisha wananchi.

Huyu mzee amekosa urais, na atakosa mpaka pepo ya mungu huko mbinguni. Duniani failure, Akhera failure.
 
UPUUZI MTUPU! Kama watu wanadhulumiwa haki zao za kikatiba kuchagua viongozi wawatakao Jamii zitaachaje kufarakana?
MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Seif Sharif Hamad amesema misimamo ya vyama vya siasa isitumike kusababisha mifarakano na kuwagawa wananchi wa Zanzibar...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…